Je,uchaguzi wa spika anne makinda ulichakachuliwa?

makoye2009

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,638
1,218
Wana JF sikuwa kwenye net kwa kitambo kidogo.
Ninachotaka kuzungumzia leo ni matokeo ya Uchaguzi wa Spika Anne Semamba Makinda ambao umepokelewa kwa hisia tofauti toka kila pembe ya nchi hii na hata nje ya mipaka .
Kwamba katika kura zote zilizopigwa tokana na Wabunge 327 Anne alipata kura 265 sawa na 74.2% huku Mabere Nyaucho Marando akiambulia kura 53 sawa na 16.2% na kura 9 zikiharibika sawa na 2.7%.
Hoja yangu ni kuwa siamini kama kweli Watanzania hatujui Hesabu au ni wavivu wa kufikiri. Nitaeleza.Kwa kutumia simple arithmetic :Ukichukua kura 265 na kuzipa asilimia kwa kura 327 itakuwa hivi:265/327 x 100 =81.03%. Ukikokotoa 74.2% kwa idadi ya Kura 327 utakuta kwamba kura 243 ndiyo zitakupa 74.2%.
Kama kweli huyu mama alipata ushindi wa ASILIMIA 74.2% basi alipata kura 243 na siyo 265. Kwa hiyo kura 22 hazijulikana ziko wapi! Labda tuambiwe ama zilikwenda kwa Mabere Marando au ziliharibika.
Mchanganuo ulipaswa uwe hivi:
1. Anne Semamba Makinda…………………… kura 243………………………….asilimia 74.3%.
2. Mabere Nyaucho Marando………………… kura 53………………………… asilimia 16.2%.
3. Zilizoharibika………………………………………..kura 31…………………………asilimia 9.5%.
4. Jumla…………………………………………………KURA 327……………….…………..asilimia 100%.
Au
1. Anne Semamba Makinda………………… kura 243………………………….asilimia 74.3%.
2. Mabere Nyaucho Marando……………… kura 75………………………… asilimia 22.9%.
3. Zilizoharibika…………………………………...kura 9…………………….........asilimia 2.7%.
4. Jumla………………………………………………KURA 327……………….………asilimia 100%.
Au
1. Anne Semamba Makinda…………………… kura 265………………….asilimia 80.03%.
2. Mabere Nyaucho Marando………………… . kura 53………………… asilimia 16.2%.
3. Zilizoharibika………………………………………...kura 9…………………asilimia 2.7%.
4. Jumla……………………………………………………KURA 327………………asilimia 99.9%.
Je,ukweli uko wapi kwenye uwiano huu?Je,kulikuwa na sababu za makusudi kuyatoa matokeo haya ili kuficha kura 22 za Wabunge wa CCM waliompigia Anne kura za hapana na wakampa Mabere Marando?
Jambo la kushangaza ni kwamba hakuna mtu aliyehoji uwiano huu wa kura zilizopigwa na asilimia tajwa.Si vyombo vya habari wala wabunge au wagombea husika. Siamini kama kweli Watanzania wote hatujui Hesabu kiasi hicho unless mtu aniambie kuna special Formula ya kukokotoa matokeo ya kura za usipika!
 
Shida CCM hawajui kuwa ukitaka kuwa mwongo inabidi uwe very smart. Sasa ndo wanaumbuka!!! inawezekana walichakachua kura wakasahau kuchakachua kukokotoa asilimia. Waliacha % ileile ya awali wakati wameshachakachua idadi ya kura. Nadhani ni sababu ya haraka waliyokuwanayo maana ingewezekana kuwaambia wabunge kuwa matokeo yatatoka kesho yake.

Au walitumia calculator za tume ya uchaguzi ambazo zimenanihiiii
 
Back
Top Bottom