je ubepari ndio mfumo sahihi kwa nchi yetu?

maganjwa

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
2,774
2,297
wanajf habari za asubuhi. nimependa tutafkar kidogo kuhus mfumo sahihi unaotakiwa kwa nchi yetu kwa sababu ninavyoona nchi inaenda bila dira inayoeleweka. je sis watanzania kweli ni wabepari? je tunaposema ubepari tunamaanisha nini? je ni kudhulumu wanyonge wa nchi hii na kujikusanyia mali ya udhalim ndio tuseme ubepari? najua kuna watu wazuri hapa jf wanaofikiri kwa bidii sana, leo naomba tuangalie mfumo unaostahili kwa sababu ujamaa tupende tusipende umetuathiri kwa kiwango kikubwa na wanaopinga hilo ningefurah watoe ushahidi ili twende kwa pamoja bila kumwacha hata moja wetu anayetaka kuelewa kinachoendelea hapa nchini.

sasa naomba nitoe maoni yangu mafup.sis watanzania sio wabepari wala sio wajamaa kwa sababu viongoz wanaamini ktk ubepar wakati wananchi weng hasa vijijini bado wana mentaliti ya ujamaa mfano sera ya ardhi ya nchi yetu ni ya kijamaa ambapo kila moja ana haki ya kumiliki ardhi. sasa hivi kuna vuta nikuvute kati ya wananchi na serikali yao kwa kitu kinachoitwa uwekezaji. nionavyo mimi falsafa ambayo nchi inatakiwa kufuata ni lazima watu wake waelezwe na waelewe ili kushikana pamoja kwenda kuelekea tanzania yenye neema. pendekezo langu tanzania inastahili neutral socialism. kwa maana ya kuchukua mazuri ya ujamaa na mazuri ya ubepari na kuchanganya kwenye kapu moja kupata neutral socialism. naomba tujadili ubepar ndio mfumo sahihi kwa nchi yetu? na je pendekezo langu linaweza kuwa sahihi?
 
[h=2]
icon1.png
Watanzania tunataka nchi gani? Bila kujibu hili swali kamwe hatutafanikiwa!![/h]
Watanzania tumechukua utamaduni wa waingereza wa kupenda kulalamikia kila kitu. Mara nyingi tunapenda kutumia maneno kama wao, wale kuimanisha sio mimi. Ukweli ni kwamba nchi hazibadilishwi na viongozi pekee bali wanannchi ndiyo wanaotaka maendeleo na viongozi wazuri wanafuata matakwa ya wananchi. Ni lazima Tanzania tujibu maswali yafuatayo kama kweli tunataka mabadiliko. Je ni nchi gani tunaitaka?

1. Mfumo kama wa Marekani: Mfumo wa Marekani ni kwamba serikali kwenye katiba inatakiwa kufanya vitu tu ambavyo watu hawawezi kufanya wenyewe!. Jeshi, Barabara, mifumo tu kwenye elimu, Afya, kodi, madeni ya nchi,uhamiaji, usalama wa anga,usalama wa airports, polisi, Fire, uangalizi wa maji safi, hewa safi na kutoa vibali vya hifadhi za uchimbaji wa mafuta na kulinda hifathi za wanyama vilevile wana mahakama huru. Serikali ni ya vyama vingi na kuna ushindani wa haki. Serikali haijihusishi kwenye biashara. Kwenye Mfumo huu huwezi kusingizia au kutegemea serikali ifanye kila kitu na huwezi kulalamikia serikali kwenye kila kitu

2. Mfumo wa China: Serikali ndiyo inatoa madaraka yote na ni mfumo wa chama kimoja. Uhuru wa habari unachujwa na serikali inafanya biashara kama kampuni za ujenzi, usafirishaji, ndege, banks, shule, hospitali, ni za serikali. serikali inajihusisha na ulinzi wa nchi, mahakama. Kwenye mfumo huu faida zake ni kwamba utekelezaji wa agenda ni mrahisi lakini kama agenda na viongozi ni wa zuri. Kama agenda na viongozi ni wa baya wananchi hawana jinsi ya kuwabadilisha viongozi kwasababu hakuna demokrasia ya vyama vingi. Hakuna demokrasia ya huru ya vyombo vya habari. Mfumo huu kama tunautaka inabidi tuwape uwezo serikali na sisi wananchi tufuate wanachofanya na kuwaamini kwamba wanachofanya ni sahii na ni kwa manufaa ya nchi. China haina mchanganyiko wa utamaduni kama Tanzania hivyo inaweza ikawa ngumu na vilevile tunapenda sana demokrasia. hivyo mimi sijui kwenye hii system kama itawezekana au la

3. Mfumo wa Rwanda: Mfumo wa Rwanda unafanana na wa China lakini tofauti ni kwamba China nguvu iko kwenye chama na Rwanda nguvu iko kwenye uraisi wa nchi. Hatuwezi kuwa na mfumo huu na kuwa na demokrasia wakati huohuo! hatuwezi kutaka na kupata vyote!. Huu mfumo ni kwa raisi kama una raisi mzuri nchi inaweza kwenda kwa kasi lakini kama unaraisi mbaya nchi inaweza kwenda chini kirahisi.

Mimi kwa mawazo yangu Watanzania tunajichanganya tunataka demokrasia ya Marekani lakini mfumo wa China na hii haitawezekana. Je Watanzania wenzangu ni lazima tufanye uamuzi na kama unamawazo ya system nyingine tueleze​
 
Mkuu nimekuelewa sis ni jamii inayopenda sana uhuru na democrasia na kiukweli hatujui tunataka nin ila moja nahisi ndilo sahihi watu wanaupenda sana ubepar na hawajui madhara ya mfumo huo upande mwingine serikali imeupokea kwa pupa sana bila tahadhri yoyote badala yake mambo ni vurugu tupu. ninavyoona kwa sasa sis ni ubepari mchanganyiko kwa kuwa watu wanafanya mambo mengi. Angalia mambo yafuatayo mfumo wa ruzuku,shreria ya ardhi, mfumo wa vijiji,mashirika ya uma, elimu ya msingi bila malipo hayo ni mambo ya ujamaa au yaliyofanywa na sera ya ujamaa na mpaka leo yapo na yanapendwa.


Ubinafsishaji,NGOs, uwekezaji, biashara huria nakadhalika ni mambo ya kibepar.Sasa ukichunguza hayo mambo watanzania wanapenda nchi ya ubepari mchanganyiko. ushauri wangu ni kuboresha mambo hayo kisheria na tena sheria kali sana mana maoni ya watanzania wengi adhabu ya kifo wanapenda iendelee. hiyo maana yake ni kwamba sheria kali za mfumo wa kijamaa watu wanaipenda iendelee kutumika mfano hao mafisad wanyongwe mpaka wafe watu wanalilia sana mitaani na kila kona huku wakisifiasifia mambo ya china kwa watu wa aina hiyo. kwa hiyo inabidi utulie kidogo kuchunguza kwa undani wanachotaka na wanataka nchi ya aina gani? Nadhani sasa kuna mwanga kidiogo kwamba tunataka nchi ya aina gani. hayo niliyosema ndio mambo wanayotaka watanzania na kutoka hapo ndipo tunaweza kubaini watanzania wanataka nchi ya aina gani. wadau nawaomba tukune vichwa tufanye uchunguzi mimi nimeyaona hayo na nadhani ndio tunayoitaka kinachotakiwa ni kufikr kama na sio kusaidiwa kufikir wakati wa azimio la arusha tulijaribu kufikir kama watanzania turud kwenye asili ya watu wetu malalamiko hayo yatapunguza kama sio kwisha kabisa
 
Back
Top Bottom