Je, uamuzi wa Jaji Rumanyika unathibitisha kuwa Mbowe alikuwa mfungwa wa kisiasa?

jmushi1

Platinum Member
Nov 2, 2007
24,987
22,515
Wanajamvi,

Kutokana na ukweli kuwa kina Mbowe na mwenzake Esther Matiko, hawakuwa na makosa yoyote kunyimwa dhamana na hata kufutiwa dhamana, Je siyo uthibitisho wa kuwa aliwekwa ndani kwa sababu za kisiasa?

Je hakuna chombo cha kumwajibisha huyo hakimu ambaye alipewa zawadi na mwanasiasa ya kuwa jaji?

Kwa wenzetu, huyo jaji lazima angeitwa na kuhojiwa na kamati maalum ya bunge ili kuweza kujuwa sababu zilizomfanya kufikia maamuzi yale ambayo ni kinyume cha sheria za nchi?

Kupandishwa cheo kwa hakimu Mashauri kwenda kwenye ujaji, na mwanasiasa, ni ushahidi wa “quid pro quo”, lugha ya kisheria inayooyesha kuwa kulikuwepo na manadilishano, yani yeye kumweka ndani Mbowe kinyume cha sheria, na kupatiwa cheo, ni ushahidi tosha wa “quid pro quo “

Wana JF nadhani katiba mpya ni muhimu kupita kiasi! No checks and balances! Hii katiba haina tofauti na ile ya enzi za Joseph Stalin au Mao Zedung!

Jaji Rumanyika sio tu amewaachia huru Mbowe na Matiko bali pia amefuta masharti ya dhamana ya kuripoti Polisi kila wiki.
Akisoma uamuzi huo leo, Jaji Sam Rumanyika amesema ushahidi uliowasilishwa mahakamani unaonesha Mbowe na Matiko hawakuruka masharti ya dhamana kama ilivyoelezwa na upande wa Jamhuri. Mahakama kuu imejiridhisha kwa nyaraka kuwa Mbowe alikwenda Afrika kusini kwa matibabu na akatumia kipindi chake cha mapumziko ya matibabu kwenda Ubelgiji jambo ambalo si kosa kisheria.

Pia Ester Matiko hakufika mahakamani siku ya kesi yake kwa sababu alitumwa na Spika kwenda Burundi kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya mabunge ya Afrika mashariki. Ester aliwasilisha mahakamani barua ya Spika lakini ilikataliwa na kufutiwa dhamana.
 
Katiba haifuatwi, sheria zinapindishwa kiasi kwamba hata sisi ma-layman tunaona makosa ya implementers.

Bunge limejaa vichaa wa fisiem wao kazi yao ni "ndioooooo" na hapo ndipo bunge limeonekana kama mbwa koko tu.

Hawa wabunge wa namna hii waondoeni 2020, shenzi kabisa. Yani nchi inaendeshwa kijinga kabisa lakini bunge lipo tu kama jengo na halina watu wenye kufikiri.

Ukihoji unaitwa msaliti eti umetumwa na mabeberu.
 
Kisheria kuwa rumande sio sawa na kuwa mfungwa. Hakuna wakati wowote ambapo Mbowe amewahi kuwa mfungwa.
Kusema alikuwa rumande kisiasa ndo utafurahi? Walikaa huko kwa muda gani? Je haikuwa kinyume cha sheria?

Kwenye taifa lenye kufuata demokrasia na checks and balances, hii issue lazima ingetinga bungeni na angekuja kujieleza! Kwasababu kila kitu ni siasa, sitoshangaa upinzani ukilibebea hili jambo bango!

Whatever he did, is totally uncalled for and absolutely despicable!
 
Wanajamvi,

Kutokana na ukweli kuwa kina Mbowe na mwenzake Esther Matiko, hawakuwa na makosa yoyote kunyimwa dhamana, Je siyo uthibitishonwa kuwa aliwekwa ndani kwa sababu za kisiasa? Je hakuna chombo cha kumwajibisha huyo hakimu ambaye alipewa zawadi na mwanasiasa ya kuwa jaji?

Kwa wenzetu, huyo jaji lazima angeitwa na kuhojiwa na kamati maalum ya bunge ili kuweza kujuwa sababu zilizomfanya kufikia maamuzi yale ambayo ni kinyume cha sheria za nchi?

Wana JF nadhani katiba mpya ni muhimu kupita kiasi! No checks and balances! Hii katiba haina tofauti na ile ya enzi za Joseph Stalin au Mao Zedung!

Mao Zedong
 
Absolutely YES.
 
Back
Top Bottom