Je twaweza shinda vita ya ukombozi wa Tanzania dhidi ya mkoloni mweusi wa ndani bila uwepo wa Mungu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je twaweza shinda vita ya ukombozi wa Tanzania dhidi ya mkoloni mweusi wa ndani bila uwepo wa Mungu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yericko Nyerere, May 22, 2011.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  May 22, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,232
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Kila upatapo nafasi ya kumuomba na kumshukuru mungu wako yafaa ufanye hivyo, kwani kila andiko lenye pumzi ya mungu linamafaa kwa muamini.

  Harakati zozote zile za ukombozi wa mnyonge ili zifanikiwe yafaa jina la bwana liwe juu yao!!!

  Ma thinker kila mtu kwa imani yake amuombe mungu! Twendeni makanisani na misikitini!!!!!!!!!!!!!!
   
 2. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Ukoloni wa mzungu una mazuri yake mengi !
  Ukoloni wa mzungu ulituachia shule bora na tunazitumia hadi leo, barabara, reli, bandari, majengo mengi makubwa na mengine mengi mazuri.
  Lakini pia ukoloni wa mzungu ulitupatia ustaarabu mpya, mfumo wa elimu, mfumo bora wa maisha na zaidi mfumo wa kujitawala.
  Sasa kuna huyu mkoloni mweusi aka watawala wengi wa kiafrika.
  Mkoloni mweusi ni mroho, mbinafsi, yuko tayari kuua ndugu zake kwa ajili ya madaraka, huku akiishi kama kibaraka kwa kutorosha utajiri wa nchi yake nje ya nchi.
  mkoloni mweusi hayuko tayari kuona mweusi mwenzake akifaidi raslimali alizopewa na Mwenyezi, anajisikia fahari kuwa na urafiki na mkoloni mweupe.
  Mkoloni mweusi hajitambui, hajui dhamana yake, wala wajibu wake, zaidi ya kujisikia fahari kuwa juu ya weusi wenzake.
  Mkoloni mweusi yupo tayari kutoa mabilioni kwa ajili ya hujuma za kisiasa, kushindana na weusi wenzake, lakini hayupo tayari kutoa kiasi hicho ili kuboresha elimu au afya au miundombinu !
  Huyo ndio mkoloni mweusi !
  Tumjadili!
   
 3. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Ni mtazamo tu !
  Nafungua mjadala.
  [h=2]Aidha nilipata kusoma kwa ufupi makala by Dr Chinweizu, a Nigerian scholar - Black Colonialists: The Root Of The Trouble With Africa.[/h]Naye ameelezea kwa ufasaha
   
 4. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,739
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Viongozi barani afrika hawapo! wapo watawala wao hupenda sana kunyenyekewa,kuabudiwa,na kusifiwa hata kama hakuna zuri lolote walilo ifanyia Nchi.naam,wanapenda sana sifa.ukichunguza sana baada ya uhuru hakuna cha maana zaidi ya kushuhudia watu wakigawana utajiri wa nchi na kufilisi nchi zao. watala wa mara baada ya uhuru walijitahidi walikuwa na morals,lakini baada ya hapo ni vituko tu.
   
 5. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Ni kweli. Watawala wa baada ya uhuru walijitahidi kuimarisha misingi bora ya kujitawala.
   
 6. Bartazar

  Bartazar JF-Expert Member

  #6
  Oct 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 805
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Mkoloni mweusi ni hatari zaidi kuliko mkoloni mweupe kwa kuwa si rahisi kumjua katika hali ya kawaida! Ni kama HIV kwenye mwili wa binadamu!
   
 7. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2013
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,994
  Likes Received: 37,697
  Trophy Points: 280
  Kwakweli mambo yanayoendelea hivi sasa hapa nchini,chini ya awamu hii ya kisanii, yamenifanya nifikie hatua ya kuamini na kuunga mkono kauli ya mwanasiasa mmoja wa upinzani kuwa ni "bora vita kuliko amani inayopumbaza".Amani hii ambayo tumekuwa nayo tangu uhuru sasa imegeuzwa mtaji na watawala kwa kutufanya sisi kama makondoo kwa kuendelea kuvumilia udhalimu na ukatili wao ambao sasa unaelekea kuwa wa kupindukia na kutokuvumilika tena!

  Vitendo vinavyofanywa hapa nchini kwa sasa na kufumbiwa macho na hawa watawala dhalimu ni vitendo vya kudhalilisha utu wa mtu,ni vitendo vya unyanyasaji mkubwa,ni vitendo vya uonevu wa hali ya juu,ni vitendo vya kukera,ni vitendo vya kuudhi,ni vitendo vya kuamsha hasira na chuki dhidi ya watawala.

  Tujiulize tulidai uhuru ili kuondokana na nini na je, ni kweli hakuna element za utawala wa kikoloni kwa sasa?Hivi tulidai uhuru ili watala waje watung'oe kucha,watutoe macho,watupige mabomu ya machozi tumboni,watumwagie tindikali na kutupiga risasi za moto?!Hili ndio lilikuwa lengo la uhuru?Inasikitisha na inauma sana!Wanaosema bora mkoloni mzungu kuliko mkoloni mweusi wana sababu na haki ya kusema hivyo!

  Nashawishika kusema ni bora kupigania haki na usawa hata kwa kumwaga damu kuliko huu uvvumilivu tulionao ambao hata hauthaminiwi na watawala bali unapuuzwa tu kwa kutuona sisi wajinga!

  Ni bora vita kuliko amani inayopumbaza!
   
 8. sokwe

  sokwe JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2013
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 2,010
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  Give me liberty or give me death.
   
 9. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2013
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Anza sasa kuchukua hatua.. kwa ndg zako woote.. wape elimu ya kujitambua.. Wakijitambua tu basi tutapiga hatua dhidi ya uonevu wa ccm
   
 10. Chris Lukosi

  Chris Lukosi Tanzanite Member

  #10
  Mar 20, 2013
  Joined: Aug 23, 2012
  Messages: 4,587
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Aisee,
  Tunaomba address yako tuje kukujoin kwenye hiyo vita basi, ikiwezekana na jina kamili ili tumjue kiongozi wetu
   
 11. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #11
  Mar 20, 2013
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,994
  Likes Received: 37,697
  Trophy Points: 280
  Umetumwa na Rama wa magogoni?
   
 12. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2013
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,832
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  wewe ndugu utu uzima wako hauna maana kabisa .....NI HERI UNGEENDELEA KUWA MTOTO MILELE
  Usipumbazwe na vijisenti uvipatavyo leo ndugu yangu!
   
 13. rayun

  rayun JF-Expert Member

  #13
  Jun 11, 2013
  Joined: Mar 19, 2013
  Messages: 240
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  leo hii nataka kujua kuna tofauti gani kati ua mkoloni mwesi( tanganyika) na mkoloni mweupe(wakoloni wetu tuliowzoea ktk historia)
  kwa muhtasari ukiangalia tofauti za watu hawa utakuta
  1) mkoloni tanganyika anaamini zanzibar ni yake na wazanzibar ni ndugu zake wa damu, wimbo huu umekua ni kinanda cha kuwabembeleza wazanzibar hususan masamaki(magamba), hii imetofautiana na wakoloni weupe (wamaghrib) kwani wao walijijua kua zanzibar si kwao na ina wenyewe ambao ni wazanzibar.
  2) wakoloni hawa weusi (tanganyika) wanaamini watadumu na ukoloni wao milele na hamna siku ukolini wao utaisha, bt wakoloni weupe wqmaghrib wao walijijua kua kuna siku wataondoka na watatoa uhuru kwa watu wake

  wanajamvi naomba maoni yenu na tofauti zaidi
   
 14. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #14
  Jun 11, 2013
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hata muungano uvunjike, historia itabaki pale pale, kama Tanganyika ni mkoloni mweusi, dhane kuna kipindi aliitawala Zanzibar
   
 15. Nsabhi

  Nsabhi JF-Expert Member

  #15
  Jun 11, 2013
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 1,096
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Jiondoe kwenye Muungano kama una ubavu!
   
 16. d

  duchi JF-Expert Member

  #16
  Jun 11, 2013
  Joined: Oct 22, 2012
  Messages: 1,766
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hakuna chochote ni ubinafsi tu unakusumbua
   
 17. rayun

  rayun JF-Expert Member

  #17
  Jun 11, 2013
  Joined: Mar 19, 2013
  Messages: 240
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hata wakoloni weusi ni wabinafsi, kwa nin muwatawale wazanzibar?
   
 18. rayun

  rayun JF-Expert Member

  #18
  Jun 11, 2013
  Joined: Mar 19, 2013
  Messages: 240
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  wana jukwaa, naomba mnitowe utata, juu ya ukoloni wa tanganyika dhidi ya zanzibar, jee zanzibar ni koloni la tanganyika?
  ningependa ufafanuzi juu ya maana halisi ya istilahi zifuatazo:-
  Nini maana ya ukoloni?
  Nani mkoloni?
  Koloni ndio nini?
   
 19. w

  wadabali Member

  #19
  Jun 27, 2013
  Joined: Jan 20, 2013
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu watanzania wenzangu haitaji elimu ya chuo kikuu kusema serikali ya CCM imeshindwa kuongoza nchi ya Tanzania ambayo imejaliwa utajiri mkubwa kama vile madini,mbuga za wanyama,misitu,bahari,maziwa ,mito,mabwawa,mabonde,ardhi yenye rutuba na watu wenye vipaji vya kila aina swali muhimu la kujiuliza kwani tumefika hapa ;majibu yake ni kwamba watu tumesahau nukuu muhimu ya baba wa taifa mwalimu(NYERERE) naomba nimnukuu"Ili taifa liendelee linahitaji mambo makuu manne watu,ardhi,siasa safi na uongozi bora" leo hii hakuna majanga ambayo yanaligharimu taifa kama kukosa siasa safi na uongozi bora haya yote tumeka madarari waongoze nchi kwanini niseme madarari;
  (1)2007 DK Slaa alitaja orodha ya mafisadi 11 Kikwete akiwemo kupitia mkataba mgodi wa lusu huko Nzega akiwa waziri wa nishati na madini ambapo takwimu zinonyesha tangu 1998-2012 dhahabu iliuzwa nje tz trioni 7.7 TANZANIA TULITOZA KODI BIL26 lakini KIKWETE NI RAIS?
  (2)Tumeshudia wizi kupitia RICHMOND,DOWANS,SIMBION,PAN AFRICA ENERGY,MABILION USWISIS n.k. nani amechukuliwa hatua?
  Ndugu zangu watanzania tushirikiane kumuondoa darari ccm
   
 20. kahtaan

  kahtaan JF-Expert Member

  #20
  Dec 27, 2013
  Joined: Jul 11, 2009
  Messages: 16,783
  Likes Received: 1,662
  Trophy Points: 280
  the sokwe just spoke!!

  teh teh teh teh!
   
Loading...