Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,691
- 149,913
Hivi huu utata(kama kweli unastahili kuwepo kwa mujibu wa sheria ya kodi) wa hili swala la kodi ya VAT kwenye miamala ya kibenki na huduma za Mpesa,tigopesa,n.k, yanaweza kurekebishwa bila Bunge kufanyaia marekebisho Bajeti hii na pengine hata finance act?
Mbali na swala hilo,swala la VAT kwenye utalii haliwezi kuchangia ulazima wa Bajeti hii kupitiwa upya iwapo taarifa za watalii kufuta safari za kuja nchini ni za kweli na swala hili likawa endelevu?
Je,serikali inaweza ku-afford kusitisha makusanyo ya hii kodi mpaka Bunge la mwezi November lije likae?
Serikali ikiamua kusubiri mpaka Bunge hilo la November, itakuwa imepoteza mapato kiasi gani na yatafidiwa vipi?
Haya ni maswali ninayoanza kujiuliza.