Je, tutakuwa tumechelewa mama tukiiomba serikali ya awamu ya sita ianzishe uchunguzi dhidi ya tukio la kushambuliwa kwa mh Tundu Lissu?

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
14,403
2,000
Friends and Enemies,

Niwasalim kwa Jina la JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA KAZ IENDELEE,

Katika jambo ambalo kila nikikumbuka naishiwa kutokwa na machozi basi ni tukio la kinyama kabisa la kushambuliwa nusura auwawe Mh Tundu Lissu.

Siyo speaker wa Bunge, siyo jeshi la polisi, siyo mahakama Wala serikali walilitolea majibu ya kueleweka suala lile, lakin sote tunajua kuwa tukio lile lilitokea punde tuh baada ya hotuba ya mwendazake ikulu alipokuwa anahutubia kuhusu mambo ya madini na kuwananga aliowaita wasaliti katika harakat zake mwendazake.

Tunajua mama aliumizwa na kitendo kile na alithubutu kupita hospital Nairobi kumjulia hali Tundu Lissu, sema tuh alikuwa Hana jinsi,

Sasa,kwa kuwa mwendazake hayupo na wengi waliitaka sana haki itendeke Ila wakaingiwa na ubarid wa hofu,je tutakuwa tumechelewa tukiomba hilo suala la uchunguz lianze upya Tena kwa vyombo huru?

Tuwajue hawa wasiojulikana,wametutesa sana.
 

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
14,403
2,000
Tungepata majibu ya kueleweka kwa kupotea kwa watu kama Ben saa nane,azory na wengineo,ule unyama haukuwa wa kawaida,Ili iwe fundisho hata kwa viongoz wengine watakaokuja huko mbeleni kuwa you can't go away with innocent blood hivi hivi
 

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
13,531
2,000
Ni sahihi ili mbivu na mbichi zijulikane;
1. Alishambuliwa na walioko serikalini/CCM.
2. Alishambuliwa na wenzake katika CHADEMA.
3. Alishambuliwa na waliojipendekeza kwa Mwendazake.
4. Alishambuliwa na maadui wa nchi ili kuvhonganisha?
 

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
14,403
2,000
Ni sahihi ili mbivu na mbichi zijulikane;
1.Alishambuliwa na walioko serikalini/CCM..
Inasikitisha sana, even though mungu mkubwa Sana hajauwawa Ila just look at tundu lisu jins anavyotembea, amepewa ulemavu wa kudumu, af Ndugai alivyokosa utu akamvua ubunge, unyama wa kiwango gani?
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
40,747
2,000
Tungepata majibu ya kueleweka kwa kupotea kwa watu kama Ben saa nane,azory na wengineo,ule unyama haukuwa wa kawaida,Ili iwe fundisho hata kwa viongoz wengine watakaokuja huko mbeleni kuwa you can't go away with innocent blood hivi hivi

Iwapo ccm wako madarakani uchunguzi waka ushahidi wa hayo hauwezi kuwekwa hadharani, tuombe chama kingine kiingie madarakani, ndani ya nusu saa ukweli wa kila uchafu utawekwa hadharani. Huyu mama anaonekana ana imani kidogo kwa kumlinganisha na mtangulizi wake, lakini yeye ni muunda tu bila utekelezaji.

Mfano aliunda tume kuchunguza pesa zilizotoka BOT Jan- March 2021, mpaka leo kimya. Ameunda tume ya Covid mpaka leo hakuna maelezo. Na sasa amemuweka muovu Sabaya pembeni, lakini nayo mtindo wa kulindana utamaliza suala hili. Kwa ujumla unachoomba hakiwezekani, kwa chama chenye mfumo wa kulindana kwenye maovu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom