Je tutafika ?

aminiusiamini

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
3,577
2,221
Ndugu Watz na JamiiForum,

Leo nimeona nitoe maoni yangu binafsi ambayo yanatokaana na maono yangu sambamba na duru za siasa zinazoendelea nchini kwetu na katika bara la africa.

Kwanza,mada yangu fupi itaongelea kuhusu approach zetu,siasa na uchumi sambamba na wapi wenzetu wanaenda,hapa nikimaanisha nchi zilizoendelea.

Nathani Kwanza mimi niwe muwazi sio kwamba namfagilia raisi JPM kwa hulka alizonazo kama mwanadamu lakni mengi aliyofanya hasa kuzibua na kun'goa mirija ya watu wachache hilo nampa heko.

Lakini tusisahau kuwa JPM hatakuwa pale maisha milele. Ningepata nafasi ya kumshauri JPM ni kuwa inatupasa sasa kubadili MFUMO. Anachofanya JPM ni kufukia mashimo na sio kuanza upya na kusuka upya taratibu na mwenendo wa kufanya kazi.Sasa ni wakati wa kutengenganisha ubunge na uwaziri nikimaanisha hawa watu kama mawaziri lazima waweeke siasa pembeni na kuajiri watu wenye wenye kufahamu na wasio na maslahi binafsi yanayopingana na nchi na kazi yake.

UCHUMI. Natamani kuona wote kama nchi nikimaanisha taasisi za benki na wadau wote muhimu wa uchumi wakubwa na wadogo tukiwa na vision moja ambayo itatufanya nini tufanye na tunaenda wapi. Hatuwezi kusema uchumi wa viwanda wakati hatuja chagua viwanda vipi,kupunguza viwanda ambavyo vinaproduce same product ambayo ina inhbit healthy competition lakini pia tunaweza kujaribu kuangalia ni vitu gani tuanze kwanza kutengeneza hapa kwetu na vipi vinaruhusiwa kuingizwa ndani ya nchi.
Tukiongelea EAC basi tuwe na trade agreements ambazo tukianza kuuzia vitu na sisi wenywe kwa wenyewe itakuwa pia ni bora zaidi kuliko kutoa kwa wazungu.

BANKS. Mabenki ni sehemu muhimu sana ya uchumi wa nchi. Nathani mabenki ya Tanzania ni watu wavivu wa kufikiri,wanaotaka faida kubwa kuliko inavyowezekana,hawataki risk.Nathani mabenki kazi yao kubwa ni kutoa mikopo yenye riba kubwa badala ya kuka na incentives ambazo zinaweza kusaidia watu. Hatuwezi kukalia fedha tu na kutoa mikopo yenye riba kubwa. Lazima tufikirie upya kuhusu consumer bureau,kurahisha borrowing and lending otherwise tusahau kuendelea mbele.

Mwisho ni kwamba Watanzania ni wavivu kufikiria.Unaweza kukuta mtanzania atafungua duka ingali mwenzake anaduka hapo hapo alipo. Bongo kila mtu anataka kufanya biashara fulani anafanya. Wapo wachache wameamua kuwa na biashara zao wenyewe na wamefanikiwa ambazo sio kla mtu anazo.

Pia hulka ya upiga dili na rushwa imekuwa culture yetu. Nathani hili ni jini linatumaliza taratibu. Wenzetu nchi zinaendelea karibu watamtoa mwanadamu katika kazi muhimu nyingi na kuweka mashine sisi hata kuweka mtu bado tunashindwa,nathani tuko kwenye crisis na tunahitaji maamuzi ya haraka.
 
Una hoja kwa kiwango fulani ila mtiririko wako haufanyi kueleweka vizuri. Jitahidi kuweka mada yako vizuri.
 
Back
Top Bottom