JE Tundu Anti Pasi LISU analichafua TAIFA au anaichafua SELIKARI?JE serikali ni Taifa?

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,014
8,364
Ndugu zangu kwanza kabsa nianze kwa kutoa pole ya kimaandishi kwa Mh mbunge wa Singida ndgu yetu raia mwenzetu kwa yote anayopitia!

Pia nitoe pole kwa wale wote wanao umizwa na madhira anayopia raia mwenzao,nisisaau kutoa pole kwa Rais wa awamu ya Tano kwa kukutwa na lawama ambazo mpaka sasa kwa kweli haijaweza jitoa au jitenga nazo nazo si nyingine ni zile zinazo husu kifo cha ALFONSI MAWAZO, KUPOTEA KWA BEN SAA NANE, kupotea kwa mwandishi wa habar Azovor na watanzania wengine wengi akiwemo LISSU kushambuliwa kwa risasi.


Niende kweny mada yangu hapo juu, je ni kweli Lissu analichafua Taifa au serikali ambayo yeye anadai ndiyo iliyousika kutaka kumtoa uai?

Je serikali ni Taifa?
Je Taifa ni serikali?
Je Taifa linapita kama zipitavyo serikali?
Je raia anae ichafua nchi anatakiwa aseme nini dhidi ya Taifa?
Je Raia anae ichafua serikali anatakiwa aseme nini?
Kwa nini Raia afike hatua ya kulichafua Taifa lake?
Je Raia anaweza ichafua serikali?
Je kipimo.cha kuchafuliwa serikali ni kipi?
Je Raia wa Tanzania anayo haki kuikosoa na kuiponda serikali iliyopo madarakani?

Je walio na kiapo cha kulinda bendera wanatakiwa kuchukua hatua gani dhidi ya mtu anae chafua serikali?

Je ukichafua serikali unaweza pelekea nchi kuchafuka?

Maswali hayo hapo juu ndio msingi wa andiko langu!

Kuhusu swali la kwaza je serikali ni Taifa?kiukweli hivi ni vitu viwili vyenye tofauti kubwa sanaa hasa kweny taifa lenye mfumo wa vyama vingi! Ila kwa ufupi serikali haiwez kuwa taifa hata siku!

Vivyo vivyo, Taifa haliwezi kuwa serikali,kwani taifa ni kitu kikubwa kuliko serikali!

Serikali uchaguliwa kulingana na kura za wananchi, ila Taifa halichsguliwi na wananchi lenyewe liliumbwa na MORA!

JE MTU ANAWEZA LICHAFUA TAIFA! Ni kweli kabsa mtu anaweza lichafua taifa lake kwa kufanya yafatayo!

Kwanza kwenda kuimba nchi ya jirani akikamatwa basi wale jirani ujua kuwa raia wote wa taifa fulani alikotoka mwizi wote ni wezi

Pili kwa kufanya vitendo vya kigaid na matendo mengine yote mabaya!

Je Tundu lisu analichafua TAIFA kwa ufupi jibu lake nionavyo mimi ni HAPANA.

Je Tundu Lisu anaichafua serikali ya awamu ya TANO? JIBU LAKE NALO NI JEPESI ni HAPANA!

Kwa nini nasema hapana ni kwa ssbabu zifatazo;

Yeye anasema walio taka kumuua, walitaka kumuua sehemu ambayo serikali ugharamia ulinzi wake, ila siku hiyo hapakuwa na ulinzi je walinzi walikuwa wapi?

Anasema kulikuwa na Cctv camera ila siku hiyo ziliomdolewa je aliyeziondoa ni nani?

Anasema hata majirani zake hawajaojiwa na jeshi la police na police wapo na wanalipwa na serikali kwa kazi hipi kama ilo jambo alifanyiwi kazi?

Mwisho;

Maswali niliyouliza hapo juu kila msomaji ayatafakar na kujiuliza nini ambacho LISU alitakiwa afanye baada ya kupona mauti?

Mungu akupe nguvu Lissu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anajidhalilisha mwenyewe kimataifa kwa kujivua nguo hadharani bila kujua....anahitaji msaada wa kisaikolojia tukio lake lilikuwa kubwa sana na kupona ni Mungu mwenyewe anajua.
 
Anajidhalilisha mwenyewe kimataifa kwa kujivua nguo hadharani bila kujua....anahitaji msaada wa kisaikolojia tukio lake lilikuwa kubwa sana na kupona ni Mungu mwenyewe anajua.
Kwa kusema ukweli kuwa amepigwa risasi, sehemu kulikotakiwa walinzi hawakuwepo, mageti yalikuwa wazi, CCTV zimenyofolewa baada ya kupigwa risasi, hebu nielekeze katika maelezo hayo kajichafua wapi?
 
Ndio hoja za kijinga na mfu zilizomfanya Masilngi amuumbue yule Mwamoyo wa VoA. Mwandishi alisema wapinzani wanawekwa ndani akataja majina. Masilingi akamjibu wapinzani hawako juu ya sheria kama wakivunja sheria watashughulikiwa na wala sio hao tu uliowataja ndio wapinzani Tanzania. Mtangazaji akawa mdogo.

Na wewe na TL mjue serikali ni watu na hakuna taifa bila watu. TL aache mara moja kuchafua watu wa Tamzania na Kiongozi wao Mkuu Rais JPM wakati akisubiria hatima yake kwa kosa la uhaini.
 
Lumumba wakiona uzi huu ni kama unawaweka mbolea ya chumvi chumvi kwenye kidonda
 
mkuu..., taifa ni mtu na anaweza kutembea nayo mtu, mf, israeli ya abraham, na serikali ni kikundi cha wanaotembea na taifa kuunda muongozo wa kujiongoza, kwa hio lissu anawasema wanaotuongoza!
 
Anajidhalilisha mwenyewe kimataifa kwa kujivua nguo hadharani bila kujua....anahitaji msaada wa kisaikolojia tukio lake lilikuwa kubwa sana na kupona ni Mungu mwenyewe anajua.
Wanaodhalilika ni wale waliommiminia risasi magazine nzima.... Hawalali, wanambembeleza arudi wafanye yao....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi unasema serikali gani? Serikali ya Mtaa, serikali ya kijiji? Serikali ya wanafunzi? Au serikali kuu ya Mh. Magufuli.

Toka lini serikali ikawa Taifa? Ukisema serikali, Mi simo! Kwani wewe ni serikali?
Mimi ni Taifa, lakini sijachafuka! Nashangaa kila nikisikia serikali imechafuka mimi Taifa, mwanachi Najisikia kutakata zaidi! Kwa lugha ya kimahesabu kuchafuka kwa serikali ni kutakata kwangu -Taifa. ni inversely proportional! Serikali ikichafuka, mimi natakata. Kumbuka sijasema ni serikali gani kati ya hizo nilizoorodhesha, hivyo basi wasiojulikana msinifuate!
 
Back
Top Bottom