Je tunaweza kuanzisha/ kukuza viwanda kwa kasi kama wachina? Kama ndio ebu nifuate hapa

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,367
3,778
Mchina alianzaje
Mchina alifanyaje biashara na dunia
China alikuwa anauza kwa kiasi gani (Soma kwa chini utaona biashara ilivyokua mwaka hadi mwaka kuanzia 1988- 2018)

Mchina alizungukia database inayozungumzia usajili wa bidhaa mbali mbali zinazotengenezwa ulimwenguni, huko kuna ufafanuzi kuhusu mchanganyiko wa kemikali mbalimbali ili kupata hadi kuwa bidha inayoitwa flani pamoja na kwamba wanaficha mchanganyiko mwingine ila kwa kiasi kidogo. (mfano wa kupata deodorant iitwayo Nivea pearl walichanganya: Aqua, Aluminium Chlorohydrate, PPG-15 Stearyl, Ether, Steareth-21, Hydrolized pearl, Persea Gratissima Oil, Trisodium Edta BHT, Geranol, Benzyl Alcohol. Halafu wakamalizia kusema kuwa NO Ethyl Alcohol). Huo ndio mfano sijaweza asilimia ya hivyo vitu kwenye kila gr au mg.

Mchina alimpata mkemia ambaye atamsaidia kutambua kemikali ya aina flani inavyo patikana (kemikali kupatikana kwenye mmea, miti, viumbe n.k.

Chemikali ni kama nitric acid, hydrochloric acid. N.k, sasa kazi ya mchemia ni kumsaidia kujua hizo kemikali zinapatikana kutoka wapi, kutoka kwenye nini, au kitu gani, kama ngumu basi mchina alianza kuchukua kemikali iliyo tayari na kuanza kuchanganya ili azalishe bidhaa kama ile iliyotolewa pamoja na kuwa anaweza akashtakiwa maana imesajiliwa kimataifa, ila anachofanya anatoa toleo ambalo lina mapungufu kidogo au imezidi kidogo ili kuepuka kushtakiwa kwa kutoa kitu/ bidhaa kama kama ile ile maana ni ngumu kdg kupatia, kumbuka nilisema huwa wanaficha mchanganyiko mwingine. (mfano ni Coca cola hakuna aliyweza kupatia ladha ya Cocacola wote wanajaribu).

Mchina mwingine kazi yake ilikuwa buzy sana kutengeneza muundo wa kitu (design) mfano muundo wa, meza, gari, chuma, bati, plastiki …. Wapo wengi sana hata huku kwetu tunao.

Serikali ya china na wadau mbalimbali ndani na nje ya China walitoa mikopo yenye riba nafuu kwa wanao tengeneza bidhaa na kuwapa ruzuku ili waweze kuanza kuzalisha bidhaa ambazo zitauzwa kwenye masoko ya ndani na nje. Hii ni sambamba na wanaopokea tenda za ujenzi wa majumba, barabara, madaraja… huku Africa nao wanapewa mikopo huko kwao kuhakikisha pesa inarudi kwao na wanatumia bidhaa za kutoka kwao kwa asilimia kubwa ili kufanya kazi walizopewa huku Africa na bara zingine, kwa wachina haya ndio sehem ya masharti ya mikopo ya serikali yao kwa wazawa. Tukumbuke tenda wanazozipata huku Tanzania ukiangalia vizuri sana, kuanzia magari na material wanazotumia wanasafirisha kutoka kwao.

Mchina aliendelea sana na juhudi zake za utengenezaji na kuboresha mazingira na miundombinu ya kutengenezea bidhaa,

Viwanda vingi kutoka mataifa mengine walienda china kufungua viwanda maana hata upatikanaji wa material/ rawmaterial, thamani ya kutengenezea vitu vyao huko china ilikuwa ni rahisi na kwa bei rahisi sana, maana wanajituma kuhakikisha wakemia na wafanyakazi wengine wanapata mishahara mizuri na wanasimamia zoezi vizuri la kuchanganya kinacho hitajika kutengeneza bidhaa na ma designer wanafanya kazi kwa bidii sana.

Serikali ilisimamia swala la malipo ya vibarua na wafanyakazi na kuweka viwango pamoja na kuwa wengine wanapandisha zaidi sio mbaya, mataifa wanavutiwa sana kuweka viwanda vyao china kwakuwa sio gharama sana kuwalipa vibarua na wafanya kazi wengine ila wanakuwa na muda maalum wa kufanya kazi ili kama wataweza wanaweza wakafanya kazi zaidi ya moja ndio warudi kupumzika na huku wanakuwa wamepata pesa za kutosha.

( UTANI na NIWACHEKESHE KIDOGO: hivi mnajua wajapani wasichana wengi sana ni bikra zaidi ya mataifa mengine? Ni kwa sababu wao wanaona muda wa kushinda wanafanya tendo la ndoa ni wa kupoteza bure na kuchosha sana hivyo inaweza ikasababisha akashindwa kwenda kazini au kufanya kazi kama inavyo takiwa. Tendo sio priority sana kama chakula cha kila siku tunavyokula huku kwetu maana kwetu ni lazima sasa sijui kuendekeza sana kuna tusaidia nini badala ya kazi kwanza, tendo ni wakati wa mapumziko).

LEO SISI WATANZANIA TUNATAKA TUJARIBU KUWA NA NCHI YENYE VIWANDA VINGI TUNATAFUTA NJIA IPI ILI TUFIKE WAPI AU TUNAMTEGEMEA NANI AJE AANZISHE VIWANDA VINGI HAPA NCHINI?

Mchina aliona kuwa yeye ndiye mwanzilishi wa hivyo viwanda kwa msaada wa serikali yake ili kufika hapo walipofika walikubaliana na hatimaye walifika na wanaendelea.

Yapo mambo kadhaa ambayo lazima tuyaangalie/ tuyafanyie kazi na penye kasoro parekebishwe maana wengine wanayasikia, wanayaona na wanayaishi yote hayo yamo ndani ya: MIUNDO MBINU, UTENDAJI WA SERIKALI, HALI YA SIASA NCHINI, UENDESHWAJI WA MASHTAKA MAHAKAMANI, MAZINGIRA YA KUWEKEZA, URAHISI WA KUISHI, AINA YA MIKOPO NA RIBA, AINA YA ELIMU ITOLEWAYO, MSAADA WANAO UPATA WANAFUNZI ILI WAFIKIE MALENGO YAO…., Yote Haya/ baadhi au vichache sana hudhoofisha sana juhudi ya viwanda.

Niongeze sauti au inatosha?

Kwa maelezo zaidi

Reporter: China
Product Codes: Total Trade
Nomenclature: HS 1988/96
Level of Aggregation: Sub-Heading all 6 Digits HS-Codes
Partners: World
Trade Flow: Export
Years: 1988 -2018

CHINA TOTAL TRADE TO THE WORLD

YearTrade Flow NameTrade Value in 1000 USD
1992​
Export 84,940,013.57
1993​
Export 91,743,944.70
1994​
Export 121,006,260.22
1995​
Export 148,779,499.52
446,469,718.02
1995​
Export 148,779,499.52
1996​
Export 151,047,454.72
1997​
Export 182,791,585.79
1998​
Export 183,808,983.04
1999​
Export 194,930,778.54
2000​
Export 249,202,551.02
1,110,560,852.63
2000​
Export 249,202,551.02
2001​
Export 266,098,208.59
2002​
Export 325,595,969.77
2003​
Export 438,227,767.36
2004​
Export 593,325,581.43
2005​
Export 761,953,409.53
2006​
Export 968,935,601.01
2007​
Export 1,220,059,668.45
2008​
Export 1,430,693,066.08
2009​
Export 1,201,646,758.08
2010​
Export 1,577,763,750.89
2011​
Export 1,898,388,434.78
2012​
Export 2,048,782,233.08
2013​
Export 2,209,007,280.26
2014​
Export 2,342,292,696.32
2015​
Export 2,273,468,224.11
2016​
Export 2,097,637,171.90
2017​
Export 2,263,370,504.30
2018​
Export 2,494,230,194.97
26,660,679,071.92
Source: UN COMTRADE

*​
 
Back
Top Bottom