Je, tunaokoa uchumi au ndio tunakwenda kuangamiza uchumi kwa maamuzi haya?

M'Jr

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,697
2,000
Juzi Rais Magufuli ametoa hotuba iliyoonyesha dhamira ya Serikali kutokuwa tayari kufunga baadhi ya mikoa (lockdown) yenye maambukizi makubwa ya Covid19 hapa nchini. Sababu kubwa ya raisi ni kwamba mikoa hii (hasa Dar es salaam) ndio source kubwa ya mapato yabserikali kwahiyo kuilockdown ni kulockdown pia mapato ya serikali.

Mimi sitaangalia sana kibinadamu kwa maana ya mapato vs uhai kwasababu hili limeongelewa sana. Nitaangalia kwa muktadha rahisi kabisa wa kiuchumi.

Kwa sasa serikali imeacha mipaka yetu wazi ili kutofunga njia za kiuchumi (kasoro uwanja wa ndege pekee) hii imeelezwa pia na rais kuwa kama tukifunga mipaka kuna hatari ya nchi nyingine 8 kuathirika kama tutafunga mipaka yetu (ingawa nyingi ya hizo nchi wamefunga mipaka yao kwahiyo tunawahurumia watu ambao hawatuhurumii bali wanajihurumia wao)

Sasa hofu yangu iko hapa
Baada ya muda janga hili litakwisha na tutarudi kwenye maisha ya kawaida. Hata hivyo effect zake zitakaa kwa muda mrefu kidogo na ndio hizo ninazozohofia kuwa zinaweza kuja kuwa na athari hasi kubwa kwenye uchumi wetu.

Mfano baada ya janga hili, nchi nyingi zitachukua tahadhari ya watu wanaoingia na kutoka nchini mwao na zile ambazo zilichukua hatua madhubuti za kuzuia ugonjwa huu zitapata ahueni ya kiuchumi haraka kuliko zile zilizobaki kushangaa kutegemea rehema za Mungu.

Mfano tunaweza kujikuta tunazuiliwa kuingia nchi nyingine kwasababu itaonekana kuna possibility yabkuwapelekea Corona na hivyo kujikuta hatuwezi kufanya biashara zetu nje ya nchi yetu. Pia tunaweza kujikuta hata bandari yetu inapoteza biashara kubwa kwankigezo hicho na baadhi ya nchi kuamua kupitishia bidhaa zao bandari za Beira, Mombasa au hata Africa kusini ambako watakuwa na uhakika na afya zao.

Tunajua tunategemea sana utalii ili kuingiza fedha za kigeni. Sasa hao wazungu ambao ndio wanakuja kutalii hapa kwetu wakiambiwa tu kwamba wasije kwetu wasababu tulihandle vibaya Covid19 cases na kuna possibility ya kuwa na wagonjwa huko, hawatakuja na hii itakuwa a big blow for us.

Kwa haya machache tunaweza kuhusi tunaokoa mapato kidogo kwa sasa huku tukiwa tunaua kabisa uchumi hapo baadae.

Tuwe makini
 
Bia yetu

JF-Expert Member
Apr 14, 2020
4,991
2,000
Umeandika vitu vingi hata havina uhalisia

Mtafute mtaalamu wa uchumi akueleze kabla hujaandika
 
momaka

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
414
500
Mleta mada, na mimi naliona hilo unaloliongelea hapo. Tunaweza kuja kuwa locked out nikiwa na maana kwamba wenzetu waliokuwa wamejipiga lockdown wakawa wamefanikiwa kuondoa gonjwa hili kwenye nchi zao. Lakini nasisitiza kupanga ni kuchagua tutavuna kile tunachopanda.
 
lbaraka

JF-Expert Member
Feb 24, 2014
378
250
M'Jr,
Umeongea point kubwa sana mkuu ambayo nami yanikereketa nafsini kwa kweli. Serikali inaposhindwa kuutumia muda vizuri katika kupambana na kuuzuia huu ugonjwa kama nchi zingine zinavyofanya, ndivyo mambo mengi ya kiuchumi na kijamii pia yaliyosimama kwa sasa yatakapozidi kusimama zaidi. Mfano, biashara nyingi zimefungwa, taasisi za elimu nazo zimefungwa, hoteli karibia zote zimefungwa nk.

Donald Trump anahangaika usiku na mchana kubuni chochote kuokoa muda ili watu warudi makazini. Na billionaires wa pale ndo wanaompa pressure, yeye mwenyewe biashara zake za hoteli zimedoda sana.

So, iwapo tutaendelea kufanya mzaha na kutoweka strategies zetu wazi na kuepuka ndimi mbili za kuwachanganya wananchi, kwa kweli itakuja kutugharimu. Swali kuu la kujiuliza ni hili, " WHEN AND HOW SHALL WE GO BACK TO OUR NORMAL LIFE THAT WE HAD BEFORE?"
By the way, kwa hali ilivyo sasa, jipambanie mwenyewe tu, don't wait for the government to save your ass!
 
sblandes

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
4,583
2,000
1.White list itakuwa compliance states.
2.Transitional list state ni zile ziko njiani kukidhi vigezo.
3.Non compliance states zitakuwa zenye mapungufu mengi lakini kichwa ngumu kufanya mabadiriko.
Sisi tutakuwa kundi lipi?
 
Benny Haraba

JF-Expert Member
Dec 7, 2012
5,322
2,000
Juzi Rais Magufuli ametoa hotuba iliyoonyesha dhamira ya Serikali kutokuwa tayari kufunga baadhi ya mikoa (lockdown) yenye maambukizi makubwa ya Covid19 hapa nchini. Sababu kubwa ya raisi ni kwamba mikoa hii (hasa Dar es salaam) ndio source kubwa ya mapato yabserikali kwahiyo kuilockdown ni kulockdown pia mapato ya serikali.

Mimi sitaangalia sana kibinadamu kwa maana ya mapato vs uhai kwasababu hili limeongelewa sana. Nitaangalia kwa muktadha rahisi kabisa wa kiuchumi.

Kwa sasa serikali imeacha mipaka yetu wazi ili kutofunga njia za kiuchumi (kasoro uwanja wa ndege pekee) hii imeelezwa pia na rais kuwa kama tukifunga mipaka kuna hatari ya nchi nyingine 8 kuathirika kama tutafunga mipaka yetu (ingawa nyingi ya hizo nchi wamefunga mipaka yao kwahiyo tunawahurumia watu ambao hawatuhurumii bali wanajihurumia wao)

Sasa hofu yangu iko hapa
Baada ya muda janga hili litakwisha na tutarudi kwenye maisha ya kawaida. Hata hivyo effect zake zitakaa kwa muda mrefu kidogo na ndio hizo ninazozohofia kuwa zinaweza kuja kuwa na athari hasi kubwa kwenye uchumi wetu.

Mfano baada ya janga hili, nchi nyingi zitachukua tahadhari ya watu wanaoingia na kutoka nchini mwao na zile ambazo zilichukua hatua madhubuti za kuzuia ugonjwa huu zitapata ahueni ya kiuchumi haraka kuliko zile zilizobaki kushangaa kutegemea rehema za Mungu.

Mfano tunaweza kujikuta tunazuiliwa kuingia nchi nyingine kwasababu itaonekana kuna possibility yabkuwapelekea Corona na hivyo kujikuta hatuwezi kufanya biashara zetu nje ya nchi yetu. Pia tunaweza kujikuta hata bandari yetu inapoteza biashara kubwa kwankigezo hicho na baadhi ya nchi kuamua kupitishia bidhaa zao bandari za Beira, Mombasa au hata Africa kusini ambako watakuwa na uhakika na afya zao.

Tunajua tunategemea sana utalii ili kuingiza fedha za kigeni. Sasa hao wazungu ambao ndio wanakuja kutalii hapa kwetu wakiambiwa tu kwamba wasije kwetu wasababu tulihandle vibaya Covid19 cases na kuna possibility ya kuwa na wagonjwa huko, hawatakuja na hii itakuwa a big blow for us.

Kwa haya machache tunaweza kuhusi tunaokoa mapato kidogo kwa sasa huku tukiwa tunaua kabisa uchumi hapo baadae.

Tuwe makini
Swali fikirishi je tutaweza kuuficha ugonjwa wa covid -19
 
Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
12,248
2,000
Hao watalii walio handle vizuri suala la corona wamekuwa wakifa maelfu kwa maelfu kila siku. Hawana ufahari wa kumtazama mtu aliisimamia vipi corona.

Cha muhimu ni kunawa mikono katika maji yanayotiririka na kuwa na tahadhari katika kila tunalolifanya. Hayo ya mbeleni hakuna ajuaye yanafanana vipi, kesho ni fumbo ambalo mwanadamu hana uwezo wa kulifumbua.
 
Mzee hii sio thread ya propaganda, na wala sio ya kukurupukia. Ulitakiwa ufikirie kidogo then ujibu kama mtu mwenye nia ya kusaidia nchi

Sent using Jamii Forums for Iphone App
 
Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
12,248
2,000
Hakuna nchi iliyoweza kuizuia corona kwa asilimia mia moja. Ni mtihani mkubwa kwa taasisi kubwa kama IMF.

Hakuna uwezekano kwa nchi moja moja kujihami kiuchumi, ulimwengu wa utandawazi umejaa biashara zenye kuvuka mipaka hazitegemei kufanikiwa kwa kutegemea tu soko la ndani.
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,325
2,000
Mfano tunaweza kujikuta tunazuiliwa kuingia nchi nyingine kwasababu itaonekana kuna possibility yabkuwapelekea Corona na hivyo kujikuta hatuwezi kufanya biashara zetu nje ya nchi yetu.
Usiwe na wasiwasi, Corona ni virus, ikiisha imeisha na huku nyuma inakuwa imeacha kinga, haiambuliziki tena!. Hivyo don't worry!.
P
 
Marwa_J_Merengo

JF-Expert Member
Aug 6, 2018
4,236
2,000
Kiukweli corona inachanganya sana kichwa hebu fikiria kule US watu zaidi ya laki 8 wameambukizwa licha ya tahadhari zote zilizochukuliwa halafu eti Kenya ni watu mia 3 tu wameambukizwa licha ya uzembe mkubwa wanaoufanya
 
May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
2,989
2,000
Kiukweli corona inachanganya sana kichwa hebu fikiria kule US watu zaidi ya laki 8 wameambukizwa licha ya tahadhari zote zilizochukuliwa halafu eti Kenya ni watu mia 3 tu wameambukizwa licha ya uzembe mkubwa wanaoufanya
US hawakuchukua tahadhari yoyote mapema. Yaani kama wana raisi basi ni awamu hii, maana sasa hivi kapendekeza watu wapigwe sindano za disinfectant kama tiba ya corona.
 
M'Jr

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,697
2,000
Usiwe na wasiwasi, Corona ni virus, ikiisha imeisha na huku nyuma inakuwa imeacha kinga, haiambuliziki tena!. Hivyo don't worry!.
P
Kaka Paskali, we unajua kwamba economic muscles zinatofautiana baina ya nchi na nchi so athari za 2 months zinaweza kuwa na different impact kwa nchi tofauti pia kulingana na strengths za muscles zake.

Lakini pia tafiti za sasa hivi zimeonyesha kuwa virus hawa nao wanajibadilisha badilisha kulingana na resistence wanayokutana nayo so namna walivyokuwa last 2 years ni tofauti na sasa so kumbe wanaweza wakatuchukua kama miezi kadhaa mbele kuweza kupambana nao.

So its wise to take precautions

Sent using Jamii Forums for Iphone App
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom