ZEE LA HEKIMA
JF-Expert Member
- Aug 10, 2015
- 1,417
- 1,839
Hivi kweli, hapa nchini tunao wataalamu wa compyuta walio mahiri vya kutosha kuweza kuzuia uharibifu (hacking) katika ile mitambo ya kukusanya kodi ambayo Mhe Rais aliizindua siku chache zilizopita? Ni wiki iliyopita tu tulisoma kwenye vyombo vya habari namna ambavyo nchi zilizoendelea zenye wataalam wa hali ya juu zimejikuta zimeshaingiliwa kwenye mifumo yake ya compyuta. Kwenye sehemu nyeti kama kukusanya mabilioni ambayo ni kodi iliyolipwa haiwezi ikatokea ukafanyika uingiliaji wa mfumo (hacking) ambao unaweza kuiletea serikali hasara kubwa sana? Je, serikali imejiaandaa kwa hili?