Je tunamuhitaji Nostra Damus atabiri hatima ya Tanzania?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je tunamuhitaji Nostra Damus atabiri hatima ya Tanzania??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Giro, Apr 1, 2009.

 1. Giro

  Giro JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2009
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 360
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kutokana na hali halisi ya sasa inayoendelea Tanzania husani katika nyanja ya siasa na uchumi kwa ujumla.
  Je tunamuhitaji Nostra Damus atutabirie hatima ya inchi yetu??

  Kila siku mambo mapya yanazuka kiasi kwamba Wananchi na Taifa limeanza kugawanyika hatuelewi tushike lipi tumsikilize nani tumuamini nani,huku maisha yanazidi kuwa magumu kadiri siku zinavyokwenda na hatuna juhudi zozote za makusudi za kuumiza vichwa vyetu kutatua matatizo yetu ya kuichumi.Kila siku saisa siasa tu,kuchafuana ndio umekuwa wimbo.Labda tumuite Nostra Damus japokuwa ameisha kufa aje hata katika njozi amtabiriwe muheshimiwa JK kule tunapokwenda na hatima Taifa letu.

  Maswali haya pamoja na mengine mengi, yanavuta hisia zangu kufanya nipende kupitia na kuchambua utabiri wa mnajimu mashuhuri wa Ufaransa, Nostra Damus

  Utabiri wa Nostra Damus juu ya mambo ya kimataifa ulianzia na nchi yake, Ufaransa. Alitabiri mapinduzi ya Ufaransa ya 1789.

  Serikali ya Ufaransa tangu utawala wa Mfalme Louis wa XVI, ilijengeka juu ya mhimili wa udikteta wa kifalme (absolute monarch). Licha ya kuenea kwa mawazo mapya ya kimapinduzi yaliyopendwa na wengi juu ya kupunguzwa kwa mamlaka ya watawala kwa njia ya mgawanyo wa madaraka, haki za asili na utawala kwa misingi ya utashi wa walio wengi, mfalme aliendelea kuwa mhimili wa madaraka yote na asiyehojika.

  Kama walivyokuwa wafalme Belshaza wa Babeli na Julius Kaizari wa Roma ya kale, mfalme Louis alilewa madaraka kiasi cha kujiona kuwa mtu asiyeweza kutishwa wala kuguswa na kitu chochote chini ya mbingu. Mfalme huyo alizoea kusema "mimi ndiye taifa la Ufaransa na taifa ndilo mimi."

  Udikteta huo ulizua manung`uniko katika jamii yake, hasa kutoka kwa wanyonge juu ya haki za msingi za binadamu, demokrasia na utawala wa sheria, hali iliyojenga chuki kubwa dhidi ya tabaka la watawala.

  Nostra Damus zaidi ya miaka 160 kabla ya mapinduzi ya 1789 alitabiri uasi dhidi ya mfalme kwa sababu hizo akisema: "Mume (mfalme) akiwa mwenye huzuni pekee atatawazwa na kuondolewa. Mgogoro utaanzia kwenye kiwanda cha vigae na watu 500. Muasi mmoja atavikwa taji.

  Huu ulikuwa utabiri sahihi na wa kweli kwani maasi ya 1789 dhidi ya utawala wa Mfalme Louis wa XVI yalianza na walala hoi 515 kwenye kiwanda cha kutengeneza vigae na matofali. Na mapinduzi yalipoanza, yalikuwa mapinduzi ya wanyonge dhidi ya marupurupu ya watawala.

  Na pale Mfalme Louis alipoita jeshi kwa ushauri wa mkewe, mama Marie Antoniette kuwatawanya walala hoi waliozingira majengo ya bunge, ni Count Mirrebeau (muasi), msemaji wa walala hoi aliyeunguruma akisema: "Tupo hapa kwa ridhaa ya watu, hatuondoki hata kama ni kwa mtutu wa bunduki mpaka hapo tutakapoipatia ufaransa katiba yake halali."

  Mfalme Louis alisalimu amri kwa madai ya wanyonge na kufungua njia ya mapinduzi ya taifa hilo.


  Hivi JK unataka watu wafike huko?? basi tuambie dhamira yako nini katika Taifa letu,Kila kitu umekaa kimya kama Taifa halina Kiongozi.
  Au unatushawishi tukubali ule msemo mbwa akimuoa chatu anafyata mkia??
   
 2. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35

  Hilo wala JK halimgusi ng'o!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 3. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mkuu Giro,

  Heshima mbele; soma alama za nyakati ndugu yangu, tunaelekea 2010 kuna uchaguzi mkuu na watu wanajipanga kwa maandalizi ya mchuano huo.

  Kama ni michezo, huu ni wakati timu zinakwenda kambini. na siasa kama ilivyo michezo mingine, kuna mbinu za hapa na pale nje ya uwanja; kama kwenda mlingotini, kumuhonga mwamuzi, kuhujumu wapinzani wako; yote haya ni sehemu ya mchezo. Wengine hushindwa hat kabla ya mechi kwa visingizio mbalimbali.

  Kamw, hatumuhitaji huyo Nostra Damus, ifikapo January 2011 hutayasikia tena haya. Au ndiyo maana yule Manajimu mashuhuri Afrika Mashariki akazushiwa kifo?
   
 4. m

  mkurugenzi1 Senior Member

  #4
  Apr 1, 2009
  Joined: Mar 22, 2009
  Messages: 122
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hatma ya Tanzania zamani ikiitwa Tanganyika iko mikononi mwetu wa Tanzania. Tusibweteke kwa starehe za muda mfupi. Hatma ya tanzania itajulikana baadaya muda kufika na si kutabiri. Hatutaki kudanganywa tena na wanasiasa na watabiri hewa.
   
Loading...