Je tunajua Kenya inanufaika zaidi na Kiswahili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je tunajua Kenya inanufaika zaidi na Kiswahili?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by kinetiq01, Jun 10, 2009.

 1. kinetiq01

  kinetiq01 Member

  #1
  Jun 10, 2009
  Joined: Aug 25, 2006
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huenda si hoja mpya, lakini najiuliza endapo tunajua kwamba Kenya inanufaika zaidi na Kiswahili licha ya kuwa na wazungumzaji wachache kuliko Tanzania?

  Nasema hayo kwasababu kibiashara au kiteknolojia inaonyesha Kenya inapata miradi mingi na mikubwa zaidi kuliko Tanzania kwa kigezo cha lugha ya Kiswahili.Nitatoa mfano:-

  1. Jumapili ijayo Facebook watafanya sherehe Nairobi ya kuzindua mradi wa Facebook kwa lugha ya Kiswahili. CEO na founder Mark Zuckerberg ndiye atakuwa mgeni rasmi.

  2. Microsoft wamekuwa na ofisi kubwa Nairobi kwa muda mrefu, ambapo project yao ya OS localisation imepata mafanikio makubwa.

  3. Google wana ofisi ya kanda Nairobi, wanafanya shughuli mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuunda translation tool ya Kiswahili.

  Mashirika yote haya yanaajiri wataalam wa Kiswahili ambapo kwa asilimia kubwa ni wakenya. Sisi wa kwetu wanaishia kulalamika kuwa Kiswahili kinachotumika siyo fasaha, lakini hawachukui hatua kuwavutia hao wenye miradi kuiendeleza ndani ya Tanzania.

  Nimetoa mifano hiyo michache, lakini yako mambo mengi ambayo naona hatuyachangamkii. Kama kuna kitu watanzania tungeweza kufanikiwa kwa urahisi ni ku-export Kiswahili kama product, hakuna wa kutubabaisha. Lakini wapi bwana. Najiuliza tatizo ni nini? Zifuatazo zaweza kuwa baadhi ya sababu.

  - Hatuna sera ya kitaifa kujenga na kutumia Kiswahili kama biashara
  - Huenda ikawa sisi hatujui kutumia fursa zinazojitokeza.
  - Huenda jamaa wakiwasilisha mawazo ya kufanya kazi zao kwetu hawapati ushirikiano.
  - Huenda mawasiliano duni ya teknolojia yanawakatisha tamaa
  - Hatuna wataalam wa Kiswahili ingawa tuna wazungumzaji wa Kiswahili
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,544
  Likes Received: 18,184
  Trophy Points: 280
  Hoja yako ni kweli tupu na sababu zako pia zina ukweli, Watanzania tumelala, sijui ni ile sera ya Ujamaa enzi za shule bure, matibabu bure na kipindi cha njaa, chakula bure.
  Miaka ya 60, Tanzania ndio ilikuwa nchi ya kwanza duniani kutangaza rasmi Kiswahili ndio lugha yake ya Taifa. Mataifa ya nje yalichukua watangazaji wa Redio Tanzania kuwa waanzilishi wa Idhaa za Kiswahili za redio hizo. Godfrey Mngodo alikwenda kuanzisha Idhaa ya Kiswahili ya Voice of America, Elli Mboto na David Wakati wakaenda kuanzisha BBC kule London, Erasto Mbwana akaenda Sauti ya Ujerumani, nchi nyingine nyingi zikafuatia ikiwemo Japan-Florian Kaiza, India, Radio Moscow, Sauti ya China, Abdala Mbamba wa Sauti ya Umoja wa Mataifa, New-York, hata nchi kama Afrika Kusini na Rwanda walichukua watangazaji toka Tanzania kuanzisha idhaa za Kiswahili.
  Jirani zetu Kenya walikuwa na Kiswahili kibovu. Tido Mhando alipoondoka RTD na kujiunga na Sauti ya Kenya, ndiye alikuwa super star wao kabla ya kuhamia BBC.
  Sasa Kiswahili kinatawaliwa na Kenya, idadi ya watangazaji wa Kiswahili kutoka Kenya, wametupiku vibaya!.Nairobi ndio makao makuu ya BBC Swahili kanda ya Afrika. Mabosi karibu wa redio zote za kimataifa za Kiswahili sasa ni Wakenya, ukiondoa Sauti ya Ujerumani ambako bado ni Mtanzania.
  Nilitembelea chuo kikuu cha Sweeden, kinafundisha Kiswahili, malecture Wakenya!.
  Nikiwa Uswisi, kuna jamii kubwa ya Watanzania na demandi ya wanaotaka kujua lugha ya Kiswahili ni kubwa, karibu tuition zote za Kiswahili, zinafundishwa na Wakenya!.

  Kulala kwetu sio kwenye Lugha tuu, hata katika ajira za kimataifa, Tanzania hatuna sera yoyote ya job-export, ukifika Makao Makuu ya UN pale New York, waswahili kibao ila wengi ni Wakenya, Waganda na Wasomali, nilipomuuliza ofisa mmoja akasema nafasi zinatangazwa mtandaoni, Watanzania hatuziombi, Wakenya wao wanazichukua na kuzitangaza nchini mwao ikiwemo juhudi mahsusi kuwasaidia Wakenya wenye sifa, kuziomba nafasi hizo, Watanzania kimya.

  Mipaka ya soko la ajira ikishafunguliwa na kuwa huru, kama serikali yetu haitafanya juhudi za makusudi za kulinda ajira za sekta binafsi, kazi zote za wajanja (decent jobs) na zile za akili, zitachukuliwa na Wakenya, na sisi tutabakia na kazi za wajinga wajinga na zile manual.
  Baadhi ya Watanzania sijui tuna nini!?, kama vile tumelogwa!. Mimi binafsi ni miongoni mwa waliojaribu life, Uk, US na nchi kibao ughaibuni lakini niliambulia patupu na kujirudia bongo kuendelea na kukurukushana na kukurukakara za kazi za kijungu jiko katika lindi la umasikini uliotopea.
   
 3. a

  agika JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 381
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  asanteni kwa kuleta hiii mada jukwaaani yaaani huo ndio ukweli wenyewe ,umefika wakati watanzania tujikwamue kiamawazo kwanza maana wengi wetu tuko busy kujikwamua kimaisha huku hatujui kwamba unatakiwa uanze kujikwamua kimawazo ili ujikwamue kimaisha.
   
 4. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #4
  Jun 10, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kinetiq01 na pasco katika hoja mlizowahi toa hapa jamvini wakuu hapa mmegusa penyewe....saa ingine sisi wa tz tuko kama sikio la kufa...sijui dawa itatoka wapi tunalala sana, hizi post zenu almanusura zinitoe chozi
   
Loading...