Je, tunahitaji Tume huru au tunahitaji Tume 'Zalendo na Adilifu' ya Uchaguzi?

Abdalah Abdulrahman

JF-Expert Member
Aug 29, 2019
222
201
Kawaida ya mfumo wa kidemokrasia ni kuheshimu na kuyapa nafasi mawazo ya wananchi hata yakiwa ni ya watu wachache. Ni katika msingi huu Tanzania mwaka 1992 iliingia katika mfumo wa siasa za vyama vingi japo maoni ya wananchi wengi yalipinga mfumo huu.

Ni wachache wanafahamu kuwa Tanzania tofauti na nchi zingine iliingia katika mfumo huu kwa umakini na tahadhari kubwa ikiwa na lengo la kulinda uhuru wake na kuwalinda wananchi wake.Hii ndio sababu kubwa ya madhara hasi ya demorasia kwa nchi yetu kuwa madogo ukilinganisha na madhara ya mfumo huu katika nchi zingine duniani.Ni wazi kuwa viongozi wetu walifuata msemo wa ”Akili za kuambiwa…..”

Ni wzi kuwa mfumo wa kidemokrasia nchini umepitia changamoto nyingi na umekua ukiimarika kuanzia awamu ya Pili ya Raisi Mstaafu Ali Hassan Mwinyi,awamu ya tatu ya Raisi Mstaafu Benjamin Mkapa,awamu ya nne ya Raisi Mstaafu Jakaya Kikwete na awamu hii ya tano ya Raisi John Magufuli.

Kawaida ya mifumo hii ambayo huletwa na nchi zilizoendelea ina kuwa na malengo ya wazi na yale yaliyo fichikana ambayo ni yanafaida na hasara kwa nchi,ndio maana yapo mazuri na mabaya ya mfumo wa vyama vingi ambayo kila mmoja wetu anaweza kuya ainisha.Yapo pia yale ambayo yamefichikana na yanahitaji akili kubwa kuweza kuya ainisha kwani madhara yake hayaonekani haraka au hayatabiriki.

Kwa mfano,maadui wa Tanzania ambao hawatakii mema watanzania wanaweza kuja na hoja ya kuwepo kwa Tume huru katika kipindi hiki kifupi kuelekea uchaguzi mkuu October 2020 kwa lengo la kukatisha wapinzani tamaa kushiriki katika uchaguzi ujao ili wananchi wasipate viongozi wanaowataka,au kuleta machafuko ili taasisi ambazo zinashughulika na wakimbizi zipate kazi ya kufanya na kuturejesha nyuma kimaendeleo.

Mitego kama hii kwa serikali inahitaji akili kubwa kuweza kujua makusudio ya viongozi hawa ukizingatia hatua ambazo Tanzania imepiga katika maendeleo.

Sote tunafahamu kuwa Tume ya Uchaguzi Tanzania imeundwa kwa mujibu wa katiba ya Tanzania ambayo inaelezea wazi juu ya uhuru wa Tume hii.Sio Raisi wa Jamhuri ya Muungano au Raisi wa Zanzibar anaweza kuingilia majukumu na maamuzi ya Tume hii. Hivyo basi nina imani kuwa Tume ya Uchaguzi iliyopo ni tume huru na yenye watendaji waadilifu na wazalendo ambao watatenda haki kwa maslai ya Taifa.

Pili, muundo wa tume ambao baadhi ya wapinzani wanaulaalamikia kwamba wasimamizi wa uchaguzi wanakuwa wakurugenzi wa halmashauri za miji, manispaa na wilaya ni hoja pofu kwani ni viongozi hawa wenye uadilifu mkubwa wamefanya kazi kubwa ya kizalendo kuleta maendeleo makubwa ambayo kila mtazania anayafurahia.

Ni vigumu kwa serikali makini kuweza kuweka watu ambao sio wazalendo ambao wamekuwa wakitumika na wanaendelea kutumika na maadui wa Tanzania.Ipo mifano anuai ya viongozi wa upinzani na ushiki wao katika kuhujumu ndege zetu,madini yetu na kadhalika.

Tunataka Tume Adilifu na zalendo kwa mustakabali mwema wa Tanzania.

Mungu ibariki Tanzania
 
Hapo kwenye para ya 3 umesema demokrasia nchini imekua ikikua kuanzia awamu ya 3 hadi ya 5, embu nisaidie awamu ya 5 demokrasia imekua kivipi?
 
Kuna Uhuru wa time zaidi ya uliopo?

Kwenye post yako namba moja, bado unaamini tunaishi kwa kuamini hizo propaganda za kizee hivyo? Kuna raslimali za nchi hii ambazo wapinzani wameingia mikataba na hao wazungu? Au wapinzani wakiingia madarakani, watakuwa na wazungu wao ambao ni tofauti na hawa waliopo hivi sasa? Ni hivi tunataka tume huru ya uchaguzi, msidhani kuwa hatujui ccm mnaitetea tume hii maana inawafanya muendelee kukaa madarakani kwa shuruti, bila ridhaa ya wananchi. Tafuteni sababu zozote mtakazo, lakini tunajua nyie sio wazalendo, ila uzalendo wenu ni pale mnapokuwa madarakani.
 
tunataka tume huru.
Ambayo watendaji wake wakuu hawachaguliwi na kiongozi aliyepo madarakani.
 
Tunataka tume adilifu na zalendo kwa mustakabali mwema wa Tanzania.Mungu ibariki Tanzania
Mi nasema tume huru isiogopwe kwani ni jambo jema kabisa litakalo ondoa vinyongo mioyoni mwa watu baada ya uchaguzi.

Tusiogope kwani si lazima ccm kuendelea kutawala. Tunajijengea hofu utadhani ACT wakitawala basi nchi itaingia vitani kitu ambacho si kweli. Chama chochote kikitawala maisha yatakuwa ni haya haya tu.

Madhara ya watu kubaki na vinyongo moyoni ambavyo pengine vinatokana na fikra tu huwa ni mabaya sana. Nadhani ni moja ya vyanzo vya ugaidi duniani.
Tukikabdhiana vijiti kwa amani hakuna vurugu zozote zitakazotokea.

Unaweza kukuta watu wamekuchoka tu pamoja na mzuri yako yote, sas ukilazimisha kuendelea kuwatawala ni dhahiri ni kama unawaambia "mimi hapa sitatoka kwa njia za kawaida. Hili ndilo ninalohofia mimi na hilo ndilo linaloweza kuzalisha wakimbizi.

Gadaffi alifanya mazuri mengi lakini watu wake walimchoka.
 
Mkuu mwenyewe amesha kuwa tume kwa kumtangaza Kabudi kuwa Mbunge sasa mnataka tumeipi tena zaidi
 
tunataka tume huru.
Ambayo watendaji wake wakuu hawachaguliwi na kiongozi aliyepo madarakani.
Watachaguliwaje? Na nani? Ni nani atakayeratibu zoezi hilo? Umefika wakati tuache kung'ang'ania vitu vya kufikirika visivyowezekana. Tupiganie uwazi (transparency) kwenye mchakato wa uchaguzi. Tumeona juzi hapo tume "isiyo huru" ikimtangaza mpinzani Malawi.
 
Kwenye post yako namba moja, bado unaamini tunaishi kwa kuamini hizo propaganda za kizee hivyo? Kuna raslimali za nchi hii ambazo wapinzani wameingia mikataba na hao wazungu? Au wapinzani wakiingia madarakani, watakuwa na wazungu wao ambao ni tofauti na hawa waliopo hivi sasa? Ni hivi tunataka tume huru ya uchaguzi, msidhani kuwa hatujui ccm mnaitetea tume hii maana inawafanya muendelee kukaa madarakani kwa shuruti, bila ridhaa ya wananchi. Tafuteni sababu zozote mtakazo, lakini tunajua nyie sio wazalendo, ila uzalendo wenu ni pale mnapokuwa madarakani.
Tindo hii tume ipo huru ila kinachowafanya msingizie kuwa haipo huru ni sababu ya wasimamizi wa uchaguzi kuwa wateule wa Rais. Lakini mnajisahaulisha kuwa huwa wanakula kiapo kufanya kazi bila upendeleo. Na nafasi zao huwa wanaziweka kando na kuwa returning officers.
 
Ninaposema tume haiko huru sikosei. Kwanza kabisa rais mwenyewe sio muadilifu, je hao anaowateua watakuwaje waadilifu? Kiapo ni kufuata formalities tu na wala sio kigezo cha kumfanya mtu awe muadilifu. Ukifuatilia vizuri hawa waapaji wanamtii rais zaidi kuliko wanavyoitii katiba. Haya ni mambo yaliyo wazi wala hayahitaji utaalamu kuyaona.
 
Kwani wabunge wanachaguliwa na nani?.
Na nani atakayeleta HUO UWAZI?
Watachaguliwaje? Na nani? Ni nani atakayeratibu zoezi hilo? Umefika wakati tuache kung'ang'ania vitu vya kufikirika visivyowezekana. Tupiganie uwazi (transparency) kwenye mchakato wa uchaguzi. Tumeona juzi hapo tume "isiyo huru" ikimtangaza mpinzani Malawi.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom