Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 34,668
- 40,916
Bila shaka sote tunafahamu namna Taifa letu lilivyopitia katika kipindi kigumu sana cha rasilimali zake kutumika kiholela.
Ni katika kipindi hicho ndipo neno fisadi lilipozaliwa katika kamusi Yetu.
Bila shaka mpaka sasa sote tumeshuhudia namna awamu hii ya tano ilivyowekeza katika kupambana na ufisadi.
Mafisadi wamejulikana na kushughulikiwa.
Ingawa yote hayo yamekua yakifanyika Kelele za kuonewa kwa baadhi ya watu bado haziishi maskioni mwetu.
sote tnahitaji maendeleo, na maendeleo huja kwa juhudi za wote.
Naamini sote tunafahamu kuwa ufisadi ndio kansa ya maendeleo na ndicho kizuizi kikubwa kabisa.
Naamini pia sote tunakumbuka baada ya mauaji ya kimbari kule Rwanda ili kuhakikisha umoja wa kitaifa unarejea na kuharakisha maendeleo ziliundwa mahakama za kijamii, na mbinu za kuwataja na kuwaaibisha wahalifu badala ya kutumia mahakama za kawaida ambazo zingechukua muda zilitumika.
Je kwakua ufisadi umekua janga la kitaifa, na badala ya kutumia muda mwingi wa mahakama kupambana na hawa watu..
kwanini kama Taifa tusiamue tu kuwataja wote, tukawafahamu, na tukaanza upya???
Najaribu tu kuwaza.