Je, tunahitaji kufundisha shule za msingi na sekondari hizi Slave Trade na Colonialism?

SOMO KUPITIA WIMBO JUU YA HISTORIA ZA UKOLONI, UTUMWA, UBEBERU, UKOLONI MAMBOLEO AFRIKA KAMA KATIKA VIDEO YA VIJANA HAWA WA BAGAMOYO, TANZANIA

People singing a african choral ''Bara la Afrika'' in Bagamoyo, Tanzania

Bara la Afrika, Lahitaji Ukombozi
Ukoloni Mbaya, Na Ubaguzi Wa Rangi
Mataifa Haya Ya Ulaya Ndiyo, Afrika Kuivamia x2

Wahenga Wetu Zamani Walikataa, Ubeberu Walikataa, Ukoloni Walikataa, Utumwa Walikataa, Waarabu Waliwatesa
Ni Vigumu Sana Kusahau Kweli Walivyowaatendea X2

Wahenga Wetu Zamani Walikataa, Ubeberu Walikataa, Ukoloni Walikataa, Utumwa Walikataa, Wazungu Waliwatesa
Ni Vigumu Sana Kusahau Kweli Walivyowaatendea X2

Bara La Afrika LaHitaji Lilia Ukombozi
Umoja Wa Afrika Unatutia Moyo
Kufagia Huo Ukoloni Wote Na Ubeberu Wote
Wahenga Wetu Zamani Walikataa, Ubeberu Walikataa, Ukoloni Walikataa, Utumwa Walikataa, Wazungu Waliwatesa
Ni Vigumu Sana Kusahau Kweli Walivyowaatendea X2........

Waafrika Wote Tujipange Kupambana Rasilimali Zetu Zituletee Maendeleo
Ama Sivyo Tutabaki Tegemezi, ....

.........



Source: D'jarell Messa
 
Nianze kwa kuuliza, binadamu unaweza kudai kuwa mapungufu yako si sehemu ya ubinadamu wako? Labda jibu ni ndiyo, lakini ni kweli kuwa mapungufu si sehemu yako? Nadhani kufuta mada za "slave trade" na "colonialism" inawezekana lakini naona kama vile hoja za kufanya hivyo bado ni dhaifu. Historia yako ni historia yako tu, hata kama ni mbaya ulishaipitia tayari. Kwa hiyo ipo tu hata kama utafanya binti kuipuuza ni kazi bure. Ndiyo maana hata Wajerumani wameamua kuchapisha upya kitabu cha Adolf Hitler (Mein Kampf) licha ya kuwa aliwaingiza katika misukosuko na aibu. Na kumbukumbu zake zinatunzwa hata sasa. Hivyo nadhani mama za biashara ya watumwa ukoloni, ukoloni mambo leo n.k. zifundishwe tu mkono ukiwa kumfanya mwanafunzi aje tulikopitia (si kumfanya duni).

Kuhusu hoja ya kutumia Kiswahili kama lugha ya kufundisha hadi chuo kikuu nadhani kuna mjadala inaendelea mingine mwa wasomi na wanasiasa na matamko yanatolewa. Kwa jinsinionavyo mimi safari hiyo bado ni ndefu. Nadhani wenzangu watalizungumzia zaidi.

Nawasilisha.
 
Wewe jamaa ni mtu wa ajabu sana!
Yaani uikatae historia yako kweli??
Hayo mazungu yalikuja huku yaka pora malighafi na kuua nguvu kazi ya bara la Afrika Na ni lazima watoto wetu Na vijukuu vyetu wafahamu hayo kwasababu ndio ukweli wenyewe!
Mazungu ni majitu makatili Na yasiyojari utu wa muafrika, watoto wetu lazima wafahamu hayo! Wakue wakijua wanaowajibu wa kuibadilisha historia hii!! Huwezi kuibadilisha historia usiyoifahamu!!
Mazungu ni yakupiga vita popote yalipo!!
Mazungu ndiyo yameleta chanjo zinazoua waafrika kwa kuwapandikizia magonjwa Kama vile Ukimwi, ebola nk kwa lengo la kupunguza idadi ya waafrika Na kudumaza fikra Za mtu mweusi!!
 
Nilichosema si kufuta izo topics bali ni kuziondoa kwa watoto wetu huko msingi na sekondari wasipoteze kujiamini na tuzisome tukiwa wakubwa chuoni, matured! mimi ni muathirika wa hizo topics ndo maana nilipigana kufika ulaya! na sasa napigana kurudi nyumbani baada ya kuionja ulaya tunayoipigania kufika!
Naona wengi hamjamuelewa dada yetu. Hamaanishi zisifutwe kabisa, anachosema zifundishwe wakati vijana wako well matured. Na hapa ni ktk higher learning institutions.

naamini one day hizi topics zitafutwa na tutapata pure African scholars si kama sisi tulioumizwa na kutukuza uzungu![/QUOTE
Nilichosema si kufuta izo topics bali ni kuziondoa kwa watoto wetu huko msingi na sekondari wasipoteze kujiamini na tuzisome tukiwa wakubwa chuoni, matured! mimi ni muathirika wa hizo topics ndo maana nilipigana kufika ulaya! na sasa napigana kurudi nyumbani baada ya kuionja ulaya tunayoipigania kufika! naamini one day hizi topics zitafutwa na tutapata pure African scholars si kama sisi tulioumizwa na kutukuza uzungu!
Nikiri kuwa sikukuelewa vizuri mwanzoni. Lakini hata sasa baada ya ufafanuzi wako
Nilichosema si kufuta izo topics bali ni kuziondoa kwa watoto wetu huko msingi na sekondari wasipoteze kujiamini na tuzisome tukiwa wakubwa chuoni, matured! mimi ni muathirika wa hizo topics ndo maana nilipigana kufika ulaya! na sasa napigana kurudi nyumbani baada ya kuionja ulaya tunayoipigania kufika! naamini one day hizi topics zitafutwa na tutapata pure African scholars si kama sisi tulioumizwa na kutukuza uzungu!
Sawa. Lakini nadhani hoja yangu bado ni "valid" hata baada ya ufafanuzi ulioutoa.

Nikukumbushe tu kuwa bado idadi kubwa ya wanafunzi hawaendi ngazi ya sekondari. Na hata wakifika huko wana uhuru wa kuchagua kama wasome historia au la (wake wa options za science hawatasoma). Na wanaobahatika kufika vyuo vikuu ni wachache zaidi na huko pia wana uhuru wa kuchagua kusoma historia au la. Kwa hivi utaona kuwa kwa hoja hii wanafunzi wengi bado watakosa kuzisoma hizi mada. Ngazi pekee ya elimu ambayo walau ina "guarantee" ya kusoma historia ni shule za msingi.

Pili, sijaelewa kabisa ni jinsi gani mada hizi zimekufanya wewe binafsi ujisikie mnyonge mbele ya watu weupe. Au kwa namna nyingine, ni kwa namna gani zinaendeleza unyonge? Labda tatizo ni namna ulivyofundishwa. Na kama ndiyo, basi suluhisho si kufuta mada bali ni kuboresha namna ya ufundishaji.

Naamini kuwa watu waliofundishwa vizuri mada hizi wanafaida zaidi kuliko wake ambao hawakufundishwa kabisa au waliofundishwa vibaya. Waliofundishwa vizuri watakuwa na hoja madhububuti za kupambana na dhana potofu za unyonge wa Mwafrika.

Hata hivyo nakusifu kwa kuleta mada moto kama hii. Nadhani mjadala wa kina unahitajika. Asante.
 
Unaposema zifundishwe chuo, ziwekwe kwenye somo gani hasa kama mtu anasoma udaktari au enginering? As u go higher u specialise ndo maana mambo general yanasoma level za chini
 
Historia ni mwalimu mzuri wa kutukumbusha tusije bweteka tena hivyo historia ya ukoloni na utumwa lazima kufundishwa toka shule ya msingi, 'O-level n.k ili kutunusuru tusiishie katika mikono ya ''Ukoloni Mambo Leo'' kupitia ''soft power'' ambao ni kinyume na njia ya zamani ya ukoloni mkongwe wa kuchapwa mijeledi, utumwa, ubaguzi wa rangi, dini za kuja kwa mashua na majahazi.

Ukoloni mambo leo unakuja kwa njia hiyo ya ''soft-power'' kama vituo vya televisheni vya kimataifa kutaka tujione wanyonge, hatufai, hatuwezi kukamilisha jambo, ''dini zetu za asili ni za kishenzi''., tamaduni, mavazi na sanaa zetu kama hadithi, mashairi, ngoma, muziki, lugha ya kiswahili n.k hazifai na pia ktk upande wa uchumi ukoloni mamboleo unakuja kama ''wawekezaji feki'', Wahujumu wa Uchumi wa Taifa Kimataifa.

Hili linanirudisha nyuma na kupekua hazina ya nyimbo ambazo wazee wetu walikuwa nazo katika maktaba za miziki yao kama huu wa Afro 70 Band ya miaka ya 1970's ukombozi kamili wa mwafrika yaani kutoka uhuru wa bendera na kuwa uhuru wa kifikra, kujiamini, kuthubutu na uhuru wa kiuchumi kupitia uwezo wetu wa sayansi/teknolojia/uhandisi, viwanda, kilimo, uvuvi/mifugo na kujitegemea bila 'mjomba'':

Wimbo UKOMBOZI WA AFRIKA wa Afro 70 Band

Mapinduzi ya Afrika Ambayo Lengo lake,
Ni Ukombozi Kamili wa Mwafrika,
Yanapingana na Siasa za Unyonyaji,
Ukoloni Mambo Leo Na Ubeberu,
Shabaha Kuu ya Mapinduzi ya Afrika,
Ni Kumkomboa Mwafrika Mwenyewe,
Wataalamu wa Ukombozi,
Ni Sisi Wenyewe Tunaonyanyaswa na Kuonewa,
EEh Afrika Bado Bara la Watu Waliomo Katika Unyonge wa Kunyonywa na Kunyanyaswa
Kutakuwa Hakuna Taifa Lolote Ulimwenguni la Kutufundisha Afrika jinsi ya Kujiokoa
Tabu ma Mashaka ya tatupata
Lakini Mwisho wa Siku Afrika Nzima itakuwa Huru
Wajibu wa Kujikomboa Tunao Sisi
Na Utaalamu na Mbinu za Mapambano ya Kujikomboa
EEh Mama Eeh Mama EEh Afrika Siku Moja Afrika Itakuwa Huru

Source: Afro 70 Band
Sikiliza wimbo wenyewe Bonga Linki :Patrick Balisidya and Afro 70 Band-UKOMBOZI WA AFRIKA
 
Kukwepa kufundisha somo la historia inayojumuisha '' ukoloni na utumwa'' ni sawa na kupiga marufuku m-Tanzania asifunguke kifikra:

the colonial government decided to regulate ''beni'' because they thought it could bring political consciousness as it contained abusive elements and those which question the legitimacy of colonial administration (Chachage, 1986). For the colonialists, beni became a communist society (Lihamba, 2004, p. 238). Hence the colonial government started to charge tax for each performance so as to discourage people from dancing. As was expected, some members of beni associations were part of the nationalist movement which gave birth to the Tanganyika African National Union –TANU, the party which fought for independence (Lihamba, 1985a, pp. 29-30).

The establishment of the Ministry of Culture and Youth could be traced to 1962 President’s Inaugural Address. In this speech, Nyerere outlined the roles of the ministry, including facilitating the process of enabling Tanzanians to regain their cultural pride (Nyerere, 1966, p. 187). In the same speech to the parliament, Nyerere indicated his concern on how colonialism dehumanised African arts. His speech became the blueprint of Tanzania’s ‘cultural policy’ and led to various art reformations. This included the ‘institutionalization’ of National Art Groups (NAGs). The aim of institutionalizing NAGs was to fulfil Nyerere’s quest for the renaissance of Africanness in the arts and culture (Bakari and Materego, 2008).

From the beginning of TANU formation, decolonization movement started and Hiari ya Moyo was forced to put forward nationalism and liberation concepts that is, to fight against colonialism and (cultural) imperialism. Amka Msilale (Wake up, don’t sleep) was their first recorded performance in 1954.

Amka Msilale (Wake up don’t sleep)
Msiwe wajinga mu Tanganyika (Don’t be stupid, you are in Tanganyika [territory])
Tanganyika ni mali yetu (Tanganyika is our property)
Tukidai tutapewa (If we demand it, we’ll be given)
(Semzaba, 1983, p. 22)

Soma zaidi: Source Mwalimu Nyerere: The artist | Pambazuka News
 
Nakubaliana na mleta mada kabisa. Kabla ya watoto kufundishwa udhaifu na masaibu waliyopitia babu zao waanze kwanza kufundishwa fahari yao, tamaduni na historia yenye mlengo chanya.

Ukiangalia vitabu vya shuleni vimejaa picha za watawala wa watumwa, waafrika wakiwa wamefungwa minyororo na story kibao za kuwapamba akina Livingstone, Stanley nk. Waafrika wanachorwa kama watu wasiojiweza kiakili na kinguvu. Hii ina inaimpose inferiority complex kwa watoto ukizingatia wanakuwa Bado hawajapevuka kiakili. Kuna muda najiuliza hivi vitabu vilitungwa na wazungu au watanzania wenzetu
 
Apo uliposema kuwa hizi topics zinamfanya mtto mdgo anakua akijua wazungu na waarabu ni bora kuliko waafrika nahis hujakosea big up__________
 
Nilichosema si kufuta izo topics bali ni kuziondoa kwa watoto wetu huko msingi na sekondari wasipoteze kujiamini na tuzisome tukiwa wakubwa chuoni, matured! mimi ni muathirika wa hizo topics ...
Sasa wewe Marry; Universities watu wana specialize unless uniambie zisomwe na wanaochukua BA's an the like. Sioni umuhimu wa mtu anayesomea Engineering, IT, Electronics, Medical and Natural Sciences, and the like eti asome habari za Tip Tipu. Huo ni zaidi ya mzaha unatuletea hapa. By the way zitakuwa Core au Elective?
 
Apo uliposema kuwa hizi topics zinamfanya mtto mdgo anakua akijua wazungu na waarabu ni bora kuliko waafrika nahis hujakosea big up__________
Basi kuna tatizo katika uandaaji wa hizo topics. Muhimu flow iwe in such a way that watoto hawatajihisi dhalili bali iwe chachu ya wao kujiamini zaidi.
 
Naona wengi hamjamuelewa dada yetu. Hamaanishi zisifutwe kabisa, anachosema zifundishwe wakati vijana wako well matured. Na hapa ni ktk higher learning institutions.
Ziwe core courses kwa Engineering, IT, Medicine? Sijaelewa hapa. Tena kwa kuwa maturity ni kigezo muhimu anachopendekeza, basi zifundishwe level ya PhD kabisa au post doctoral.
 
Ziwe core courses kwa Engineering, IT, Medicine? Sijaelewa hapa. Tena kwa kuwa maturity ni kigezo muhimu anachopendekeza, basi zifundishwe level ya PhD kabisa au post doctoral.
Nadhani anachojaribu kukitetea mleta mada ni kwamba liwe kama somo la ziada ngazi ya chuo. Ni kama kwa wanafunzi wa somo la GS ngazi ya Advanced Level. Tatizo ameukimbia mjadala na kushindwa kuitetea hoja yake.
 
Mimi nafikiri tusisahau wala kuacha somo hili la ''utumwa na ukoloni mkongwe /mambo leo'' kwa kuwa tunaona ''haya'' yaliyotutokea ! Mimi nauga mkono historia ya ''utumwa/ukoloni'' iendelea kufundishwa shule za msingi, sekondari na hata ngazi za Chuo Kikuu kwa wale wapenzi wa shahada ya Historia.

Tumsikilize Prof. Noor anasema lazima vijana kufahamu kweli kuwa utumwa umefanywa na wote ''wa-afrika, wa-arabu, wazungu''. Mie pia naafiki maoni ya Prof. Noor somo la historia liendelee kufundishwa kwa ukweli wote.

Bandiko hili Kwa hisani kubwa ya Mohamed Said wa Jamiiforums
Mahojiano ya DW na Prof. Ibrahim Noor Shariff Mwandishi wa Tanzania na Propaganda za Udini

Prof%2BIbrahim%2Bphoto.jpg


Prof. Ibrahim Noor Shariff

Mwanachuoni wa Chuo Kikuu Cha Rutgers, New Jersey, Marekani, Ibrahim ni msomi wa Sanaa, Tarikh (Historia) na Fasihi ya Kiswahili.

Prof. Ibrahim Noor Sharif ameandika kitabu maarufu ''Tanzania na Propaganda za Udini,'' Kitabu hiki kimezusha mjadala mkali katika mitandao ya kijamii kiasi kuwa wakati mwingine yeye mwenyewe Prof. Noor alikuwa akiingia kujibu maswali khasa kuhusu historia ya utumwa unaoegemezwa Zanzibar ambayo yeye mwenyewe ndiko kwao.

Yasikilize mahojiano yake na DW:

://soundcloud.com/mohammed-k-ghassani/mahojiano-na-mwandishi-wa-tanzania-na-propaganda-za-udini-prof-sharif
 
Leo nimeamua kufunguka na ninaomba Mungu sana Mh Waziri wa elimu na taasisi ya ukuzaji mitaala Tanzania isome hii comment yangu thread yangu, ni hivi, mimi ni mwalimu ( nina diploma ya ualimu na nimefundisha somo la historia kwa shule kadhaa za sekondari O and A level kwa miaka kadhaa na nina BA ya Mlimani na Masters ya Social Welfare ya ulaya! na ninaishi ulaya miaka kadhaa now! iko hivi huku ulaya hawasomi kuhusu historia ya Afrika kwenye level za chini ni hadi ufike University ndo unaanza kusoma habari za Afrika! wanajua umuhimu wa historia zao na mila na tamaduni zao! watu wengi hawajui kwa undani kuhusu Afrika zaidi ya jina tu! kuna wazee wa kizungu ukiwaambia unatoka Tanzania wanakuuliza hiyo nchi iko wapi! ninapenda sana kuanzisha mjadala wa kufuta Topics mbili za somo la historia kwa shule za msingi na za sekondari!

Ninapendekeza Topics za Slave Trade na Colonialism zifutwe kwenye mtaala wa shule za msingi na sekondari Tanzania.

Hizi topics ni miongoni mwa topics zinazoendeleza unyonge wa Mwafrika na kufuta historia ya Afrika na kuondoa kujiamini kwa mwafrika, zinapoteza kabisa mila na desturi zetu!

Hizi topics zinamfanya mtoto mdogo washule ya msingi anaposoma , kukua akijua wazungu na waarabu ni bora kuliko waafrika na wana nguvu na weledi kuliko mwafrika na kumfanya mtoto angali mdogo kutamani kila kitu cha ulaya!

Hizi topics zinashusha thamani ya mwafrika na kumfanya kuabudu ulaya! ni topics zinazobeba sehemu kubwa ya somo la historia na kupoteza ufundishwaji wa historia yetu kama nchi na makabila yetu na mashujaa wetu na sayansi yetu na civilization ya yetu ya mwafrika!

Ukweli ni kuwa ulaya pia kuna shida nyingi na kuna wazungu wengi omba omba huku ulaya, na wanaomba kila mtu anaepita njia hata mwafrika!

Wakati umefika sasa tunahitaji kuwafundisha watoto wadogo mashuleni mila na desturi zetu na hayo ya slave trade na colonialism wakasome University wakiwa matured!

Ni vizuri pia tukisoma kwa kiswahili kuanzia msingi hadi chuo ili tuelewe tunachokisoma! ni hayo tu! naomba kuwasilisha!
Sorry utanisamehe kwa kutomalizia post yako kusoma had mwisho...
Lakini nimegundua kitu..
Hujui na Kama unajua lipo unalotaka kulifunika !! Wewe huna tofauti na dini flan hiv ukiwambia Waarabu walitutawala na kutufanya watumwa wana deny history!! Coz wamekua brainwashed ...au umewaamini wazungu hadi kufikia hutaki kujua walichotufanyia au hutaki kusikia and you are living abroad !! Yeah sure washakutenda kwenye hyo brain yako
1.How can you live without knowing your enemies while they exist in real sense??

2.Unatakaje kujua unakoenda wakati hujui ulikotoka

3.Mi nafikir ni nzuri kwetu hizi mambo the thing is ' hatuna mikakati ya kuchange history ,tunajifunza tu Kama hadithi laiti kweli tungekua tunaitumia ipasavyo tungekua Kama China au Korea,labda tungekua Kama America BT tumekosa vision na mission we just focus on negativity and inferiority

4. Kwa anaejua history vizur can't take Arabs and White as friends or someone to trust!! But we do trust them most while they are our enemies since then!! And these are only happen in African continent!!
 
Back
Top Bottom