Je tunahitaji katiba mpya au bora?

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Mar 1, 2016
12,686
31,470
Habari wana JF

Nimesoma digest ya matamshi ya Muheshimiwa Raisi kuhusu mchakato wa katiba mpya. Kwangu mimi sijawahi kuwa muumini wa katiba mpya bali wa katiba bora. Ni mawazo yangu kwamba, Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tangayika na Zanzibar ya mwaka 1977 ifanyiwe marekebisho kwenye vipengele vifuatavyo:

1. Tume ya uchaguzi kwa kuifanya kuwa huru na shirikishi;

2. Mihimili ya mingine ya dola (Bunge na Mahakama)kuifanya kuwa huru na yenye nguvu sawa na Serikali;

3. Kuongeza uhuru wa kushiriki siasa, ikiwa pamoja na kuruhusu mikutano ya siasa 24/7, mgombea binafsi, na kulinda haki na mali za wanasiasa;

4. Kuruhusu uraia zaidi ya mmoja (multiple citizenship) siyo tu dual citizenship, potelea mbali ata kama mtu anataka kuwa raia wa somalia, afganstan na Tanzania kwa wakati mmoja;

5. kuweka kwenye katiba sera za nchi na kuondokana na mfumo wa kutumia election manifestos za vyama kuongozea nchi, ili vyama vya siasa vibishanie ni kwa namna gani zitatekeleza masharti ya sera za nchi; na

6. Kuruhusu maamuzi ya tume ya uchaguzi ya kumtangaza mshindi wa kiti cha uraisi kupingwa mahakamani.

Baada ya hapo ibadilishwe rangi kutoka zambarau iwe ya kijani kama vile timu yangu ya Yanga. Asanteni
 
Back
Top Bottom