Je, tunaamini chama kimoja ni suluhisho la uzalendo na uchumi?

Tamapahi

Member
Feb 18, 2018
6
1
Wanajamvi tumekuwa na wimbi la Viongozi wa kuchaguliwa wa vyama vya upinzani kujiunga na chama tawala, na hali isiyo ya usawa kwenye chaguzi za marudio, hali inayoonesha dalili za kufuta upinzani, kwani naamini kwa nguvu hizi na hurka yetu ya woga hakuna hata chama kimoja cha upinzani TZ bara kitashinda chaguzi yeyote kuanzia za marudio zijazo na hata zile za serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020.Tujadili
 
Umesajili leo na kuja na pumba?! Hivi tumerogwa na nani?! Chama kimoja kimekuepo miaka nenda rudi nini kimeendelea zaidi ya uimla !!!.

Mshaurini huyo anayewatuma kuwa upinzani si uadui wala uasi. Hivyo yeye atimize wajibu wake wa leadership si lazima asifiwe na kuabudiwa!!
 
Kusajiri leo sio tatizo, tujadili bila mihemko lengo hapa ni kutafuta njia sahihi ambayo tunapaswa kupita ili Tz ibaki kuwa eneo salama kwa ustawi wa watu wake, hii ni kutokana na mabadiliki ya mfumo wa siasa Duniani. leo dunia inazungumzia siasa ya uchumi ndani yake kukiwa na fursa kwa watu wake, hivyo tunapo angazia hali ya kisiasa tanzania lazima tuone kwa mapana wanachotaka watawala kina tija kwa taifa? Chama tawala kinaweza ku accommodate watu wote kutoka vyama pinzani na wakapata fursa sawa?
 
Kuwa na chama kimoja ni kuhalalisha uharamia,wizi wa Mali ya uma,ufisadi na unyanyasaji wa RAIA,
Kwa sababu hakuna atakae hoji uchafu wowote hivyo basi watawala watavimbiwa huku wanyonge wakiendelea kukonda
 
Kukiwa na chama kimoja ni rahisi kudhibiti watu, na ni rahisi kupitisha chochote maana ni umoja wenye nia ovu. Kwa hiyo hiyo nia ya chama kimoja ni ili watu wale bila kelele.
 
Kusajiri leo sio tatizo, tujadili bila mihemko lengo hapa ni kutafuta njia sahihi ambayo tunapaswa kupita ili Tz ibaki kuwa eneo salama kwa ustawi wa watu wake, hii ni kutokana na mabadiliki ya mfumo wa siasa Duniani. leo dunia inazungumzia siasa ya uchumi ndani yake kukiwa na fursa kwa watu wake, hivyo tunapo angazia hali ya kisiasa tanzania lazima tuone kwa mapana wanachotaka watawala kina tija kwa taifa? Chama tawala kinaweza ku accommodate watu wote kutoka vyama pinzani na wakapata fursa sawa?
Je CCM anaweza kukubali kujifuta ili tuwe na chama kimoja cha kitaifa?! HAWAWEZI

Kwa hiyo maombi yako yasiwe dhidi ya vyama vya upinzani, Utakuwa unasumbuliwa na ukereketwa (ukada). Kwa kifupi hata mwehu hawezi kuunga mkono hoja hiyo, na hata ccm hawatapenda
 
Back
Top Bottom