Je, tuna Watu Jeuri (Kauzu) kama akina Nancy Pelosi katika Serikali (Tawala) zetu za Afrika hii ya sasa?

Labda niulize huku kwenye kijiwe chetu wanachoita bunge, yaani Tanganyika pamoja na koloni lake walilompora Sultani huwa wanagawa hotuba zilizochapwa?

Maana sijawahi kushuhudia mtanange wa aina hii kwenye hili genge letu huku.
 
Spika wa Bunge Marekani, Nancy Pelosi amechana hotuba ya Rais Donald Trump muda mfupi baada ya kumaliza kuisoma wakati akihutubia Bunge kwa kile kilichoelezwa kuwa kiongozi huyo wa Marekani hakumpa mkono wakati anamkabidhi nakala.

Chanzo Habari: Mwananchi Online

Hivi Yule Spika Mmoja hivi wa Afrika Mashariki ‘ Pua Kitenesi ‘ ana hata ‘ Ubavu ‘ kwa Kumuiga Mwanamama ‘ Shujaa ‘ Spika Pelosi pale na Yeye Siku moja ikitokea akaonyeshwa ‘ dharau ‘ kama aliyofanyiwa Spika Mwenzake kwa Rais Mwalimu Mkemia?

Naamini huenda hapa kukawa na Somo zuri, jema na kubwa sana tu Kwake Spika ‘ Pua Kitenesi ‘ wa Afrika Mashariki na Kati.

Nawasilisha.
Africa mtawala yuko juu ya sheria ni mungu kamili kapewa amri ya kufanya chochote
 
Kuna wanawake wanatabia za kiume, sio unakuta jitu lina sura nzito kama kifusi, halafu linatabia za kike yaani "dhaifu" kimtazamo na msimamo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Njia sahihi ilkuwa kutoka nje badala ya kuichana hotuba maana ujumbe umefika kwa wote hata kama aliichana! Kitendo cha yeye kubaki mle ndani hadi Trump anamaliza kulihutubia Bunge ni wazi alifuatilai hotuba yote na kujua yote yaliyomo!
 
Spika wa Bunge Marekani, Nancy Pelosi amechana hotuba ya Rais Donald Trump muda mfupi baada ya kumaliza kuisoma wakati akihutubia Bunge kwa kile kilichoelezwa kuwa kiongozi huyo wa Marekani hakumpa mkono wakati anamkabidhi nakala.

Chanzo Habari: Mwananchi Online

Hivi Yule Spika Mmoja hivi wa Afrika Mashariki ‘ Pua Kitenesi ‘ ana hata ‘ Ubavu ‘ kwa Kumuiga Mwanamama ‘ Shujaa ‘ Spika Pelosi pale na Yeye Siku moja ikitokea akaonyeshwa ‘ dharau ‘ kama aliyofanyiwa Spika Mwenzake kwa Rais Mwalimu Mkemia?

Naamini huenda hapa kukawa na Somo zuri, jema na kubwa sana tu Kwake Spika ‘ Pua Kitenesi ‘ wa Afrika Mashariki na Kati.

Nawasilisha.
Huku kwetu labd mtu kama Miguna Miguna au yule Jaji Maraga wa Kenya ambao walifanya mambo fulani bila kujali watukuwa salama au la! Lakini pia kuna mama mmoja ambaye aliwahikuwa Waziri wa UIngereza ambaye alisimamia ukweli juu ya ununuzi wa RADA, scandal iliyoibua vijisenti vilivyolipwa kwa Joka la Makengeza na genge lake! Nadhani anaitwa SARA COOKIE ni mfano mzuri
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom