Je Tuna mkakati gani kama Taifa wa kuendeleza vipaji na cream kama LUCYLIGHT MALLYA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Tuna mkakati gani kama Taifa wa kuendeleza vipaji na cream kama LUCYLIGHT MALLYA?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by George Maige Nhigula Jr., Jan 27, 2011.

 1. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #1
  Jan 27, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndugu wana JF,

  Nimevutiwa sana na habari na historia ya LUCYLIGHT MALLYA kama mwanafunzi bora katika matokeo ya kidato cha nne kitaifa, lakini sisi kama taifa tuna mkakati gani mahususi wa kuhakikisha vipaji hivi vinaendelezwa (to their God given potential) kwa udi na uvumba ili viweze kuwa na manufaa kwa taifa zima hapo baadae na kufanya mambo makubwa kwa taifa?

  Mataifa Mengi ya South east asia yaliweza kukusanya cream zao na kuzigharamikia kwenye institute na na shule maalumu duniani na wakaweza kupewa national building role ili ku spearhead transfer of technology and invetion to their respective country sasa sisi kama taifa tumejiwekea mkakati gani wa kuweza kuwezesha cream zetu to achieve mambo makubwa ulimwenguni, can we real dare to do that for future generation?

  SOURCE Mwananchi

  Aliyeongoza kidato cha nne ni yatima Send to a friend Wednesday, 26 January 2011 20:22 0diggsdigg

  [​IMG] Lucylight Mallya

  Mussa Juma, Arusha

  MWANAFUNZI aliyeongoza mtihani wa kidato cha mne kitaifa mwaka 2010, Lucylight Mallya (18), amebainika kuwa ni yatima ambaye wazazi wake wote walifariki dunia miaka minne iliyopita.

  Akizungumza katika mahojiano maalum, akiwa nyumbani kwa baba yake mkubwa kijiji cha Nguruma wilayani Arumeru, binti huyo aliyekuwa akisoma katika Shule ya Sekondari ya Marian, iliyoko Bagamoyo, mkoani Pwani alisema anamshukuru Mungu, walimu na walezi wake kwa kumwezesha kufaulu.

  "Sikutegemea kuwa wa kwanza namshukuru sana Mungu, walimu, walezi wangu hasa baba mkubwa na mama na wote walionifikisha hapa ikiwa ni pamoja na wanafunzi wenzangu....," alisema Lucylight.

  Lucylighty ambaye ni kwanza kati ya watoto, wanne walioachwa na marehemu wazazi walofariki dunia mwaka 2006 na (2007), alisema malengo yake ni kuwa daktari.

  Binti huyo alisema wakati anafanya mtihani huo, somo aliloona gumu lilikuwa ni fizikia, lakini anamshukuru Mungu kuwa amefaulu vizuri na kuwa wa kwanza hapa nchini.

  "Mimi nilikuwa napenda sana Kemia, Bailojia na Fizikia na nilikuwa nimejiandaa sana hivyo namshukuru Mungu kunisaidia kutimiza ndoto zangu," alisema Lucylighty.

  Baba Mkubwa wa Lucy ambaye ndiye anamlea, Dominick Mallya alisema anashukuru Mungu kwa binti yake huyo kuongoza kitaifa.

  Hata hivyo, Mallya alisema binti huyo amesoma katika mazingira magumu kwasababu hakuwa na fedha za kutosha hivyo alimwomba mmiliki wa shule hiyo, Father Valentine Bayo kumtafutia mfadhili.

  "Mamshukuru Father Bayo kwani tangu mtoto huyu akiwa kidato cha pili hadi kumaliza kidato cha nne alikuwa analipiwa na wafadhili,"alisema Mallya.

  Hata hivyo, aliomba wafadhili wa kumsaidia, ili aweze kuendelea ya masomo ya kidato cha tano hadi sita na chuo kikuu kwasababu yeye (Mallya) hanafedha za kutosha kuwasomesha watoto wote alionao.

  "Baba yake Lucy ambaye ni mdogo wangu alifariki dunia mwaka 2006 na mkewe alifariki mwaka 2007, waliacha watoto wanne na mimi nina watoto watano hivyo tunashindwa kumudu gharama za kuwasomesha," alifahmisha Mallya na kuongeza:

  “Tungependa kupata tena ufadhili wa Lucylight ili aweze kuendelea na masomo ya juu katika shule ambayo alikuwa akisoma”.

  Lucylight alizaliwa Jijini Dar es Salaam, miaka 18 iliyopita alisoma Shule ya Msingi St Mary's Tabata na baada ya alihitimu la saba mwaka 2006 alichaguliwa kwenda Shulea ya Sekondari ta Wasichana Tabora lakini aliamua kwenda Marian Girls alikohitimu kidato cha nne mwaka jana.

  Taarifa za maendeleo yake zinaonyesha kuwa akiwa kidato cha kwanza alishika nafasi ya tatu, lakini kuanzia kidato cha pili hadi cha nne alikuwa akishika nafasi ya kwanza
   
 2. Vitendo

  Vitendo JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2011
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 597
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kiuhalisia nchi haina mkakati maalumu wa kuendeleza watu waliofanya vizuri katika matokeo yao.
  Ingawa kwa mtu kama huyo najua atapata zawadi toka Wizara ya sayansi...pia huwa kuna nafasi za kwenda kusoma shule kama IST au United World Colleges(IB Diploma)..
  Ila zaidi serikali inaweza machagua tena kwenda shule ya "watoto wenye vipaji kiakili" ya Tabora wasichana,Kilakala au Msalato.
   
Loading...