Je tuna haki ya kusheherekea miaka 50 ya uhuru katika hali hii?

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,903
1,053
Wakuu pole kwa majukumu mengi ya kujenga taifa hili gumu.
Mie nimepata shida kidogo. Nimekuwa nikiona matangazo mengi kuwa kuna sherehe kubwa sana zaja za kusheherekea miaka 50 ya uhuru wetu.

Hata hivyo katika pita pita yangu nimekuta shule moja ya msingi huko Mkoani Kagera ikiwa katika hali hii tena mwaka huu wa 2011. Najiuliza na naomba niwaulize nyie ndugu zangu hivi tunayo haki ya kuteketeza pesa ya walipa kodi kufanya misherehe mikubwa mikubwa huku kuna watu wana shida hivi? Jamani watanzania priority zetu ni nini? Ni sherehe kwa kuwa tumefikisha tu miaka 50? mbona tunarudi enzi zile ambazo mababu zetu walikuwa wakifanya misherehe kwa kuwa tu msimu umewadia?, hata kama mavuno hayakuwa mazuri?

Jamani mie nachoka kabisa na viongozi wetu wanavyojali sherehe hata kama hazina umuhimu mkubwa kwa sasa. Nafikiri kwa sababu bado tuna safari ndefu ebu tuhahirishe sherehe hizo, tuitengeneze nchi vizuri ili ionyeshe picha ya kwamba kweli tumepata uhuru and then tutakuja kusheherekea baadaye.

Naomba kuwakilisha.

Ni mimi ndugu yenu,
KAA LA MOTO.

DSC09875.jpg



DSC09876.jpg


DSC09880.jpg


DSC09878.jpg
 
Bajeti zimetengwa kwenye mawizara na idara mbalimbali za serikali,
Lengo kuu ni kuwaelimisha wananchi juu ya haya mafanikio....
Halmashauri zote ni heka heka.. kujiandaa kwa sherehe kuu za mwaka huu..
Bado kuna maswali mengi ya kujaza juu hichi kizungumkuti katika nchi yetu
 
Back
Top Bottom