Je, Tumekuwa nchi maskini kwa kuwa hatukuwa tukifanya kazi?

maganjwa

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
2,774
2,297
Wanajamvi naamini hamjambo wote.

Nimetafakari sana huu wimbo wa awamu hii kitu kidogo hapa kazi tu, shughuli za siasa watu waachwe wafanye kazi, hivi tumekuwa maskini kwa kuwa hatukuwa tukifanya kazi?

Je ni kweli umaskini wetu umetokana kwa kuwa watu walikuwa hawafanyi kazi na sasa inabidi wafanye kazi tuondokane na umaskini?

Hebu nisaidieni mimi siwaelewi kabisa hawa jamaa.

Karibuni.
 
sasa ni shida mpaka wanaingia kwenye magesti kutoa watu eti tufanye kazi
 
mfano watu wamelima sana tu nyanya tenga mpl elfu saba, unalima mazao yako ukitaka ku export serikali inakuzuia wakati kulima hawakukusaidia nadhani serikali ya ccm kwa kiasi kikubwa inawatia umasikini wananchi ili iendelee kuwatawala
 
Wanajamvi naamini hamjambo wote.

Nimetafakari sana huu wimbo wa awamu hii kitu kidogo hapa kazi tu, shughuli za siasa watu waachwe wafanye kazi, hivi tumekuwa maskini kwa kuwa hatukuwa tukifanya kazi?

Je ni kweli umaskini wetu umetokana kwa kuwa watu walikuwa hawafanyi kazi na sasa inabidi wafanye kazi tuondokane na umaskini?

Hebu nisaidieni mimi siwaelewi kabisa hawa jamaa.

Karibuni.
Kama kweli logic ni kuwa kufanya kazi kwa masaa mengi ndiyo kutoka kimaisha, hebu tujiulize swali moja tu dogo, kuna watu wanaenda 'vibaruani' alfajiri na kurejea majumbani kwao usiku mkali..........

Sasa kama kigezo kingekuwa kufanya kazi kwa masaa mengi ndiyo kuwa milionea, basi hawa wanaojihimu alfajiri sana kuwahi kwenda kuchapa kazi na wanashinda huko makazini kwao mpaka usiku wa manane wakifanya kazi, ndiyo wangekuwa maBill Gates wetu hapa TZ.......
 
Wanahisi kuwa watanzania hatufanyi kazi kwa hiyo wametugeuza sisi ni tatizo la taifa kwa ujumla lakini tatizo wanalo wao wenyewe SERIKALI HAIJAWEKA MAZINGIRA WEZESHI KWA WANANCHI WAKE ILI KUWEZA KUFANYA HIZO KAZI NA KUSHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA KIMAENDELEO. Mfano mkulima kalima nyanya na hivi sasa zinawaozea huko mikoani,serikali haina kiwanda cha kusindika nyanya wala hakuna mwekezaji ambaye serikali imemleta kwa kazi hiyo,na hyo sio kwa nyanya tu hata ukiagalia msimu wa Parachichi,Nanasi,Machungwa, Ndizi,hata embe kwani Bakheressa naye huwa anazidiwa na msimu wa embe ,Alafu unataka vijana wakalime baada ya kuhitimu vyuo vikuu ,hivi wanafikiri kuwa vijana hao hawaoni changamoto za kilimo nchini? Kijana msomi huwa anafanya kitu kinachoitwa SWOT analysis na kugundua kama changamoto na fursa zipi ziko nyingi kisha kufanya maamuzi.Hii ni nchi ya watanzania ambao kila kukicha wanaamka na kujituma katika shughuli za kiuchumi na uchumi unakuwa kwa kiwango cha asilimia 6 mpaka 7 kila mwaka lakini wanaoukuza huo uchumi wana hali duni kimaisha ,Je serikali haioni kama kuna haja ya kukutana na wadau wa kilimoni na watu wa chini ili kutafakari kwa pamoja hali hiyo?
Serikali yetu na hasa hii ya awamu hii SIO SHIRIKISHI KWA WALENGWA ANGALIA WADAU WA mafao ya kujitoa katika shughuli ya kutafuta kipato au kazini walivyokuja na tamko lao.
SERIKALI HII NI SERIKALI YA VIPOFU.Naomba tuanzishe usemi huu KUIELIMISHA SERIKALI NI KULIKOMBOA TAIFA.
SERIKALI YETU INAHITAJI ELIMU NA MAARIFA KUPAMBANA NA HALI YA UCHUMI NCHINI.
HAIWEZEKANI UCHUMI UKUE KWENYE MAKARATASI TU,CHA AJABU ZAIDI TAARIFA HIYO UTOLEWA NA MAMLAKA ZA NJE KUJA KWETU SISI AMBAO UCHUMI WETU UNAKUA,HII INAMAANISHA KUWA HATA WAPI TULIPO HATUPAJUI.
 
mfano watu wamelima sana tu nyanya tenga mpl elfu saba, unalima mazao yako ukitaka ku export serikali inakuzuia wakati kulima hawakukusaidia nadhani serikali ya ccm kwa kiasi kikubwa inawatia umasikini wananchi ili iendelee kuwatawala

MCHAWI WA UMASKINI WETU NI CCM
 
Wanahisi kuwa watanzania hatufanyi kazi kwa hiyo wametugeuza sisi ni tatizo la taifa kwa ujumla lakini tatizo wanalo wao wenyewe SERIKALI HAIJAWEKA MAZINGIRA WEZESHI KWA WANANCHI WAKE ILI KUWEZA KUFANYA HIZO KAZI NA KUSHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA KIMAENDELEO. Mfano mkulima kalima nyanya na hivi sasa zinawaozea huko mikoani,serikali haina kiwanda cha kusindika nyanya wala hakuna mwekezaji ambaye serikali imemleta kwa kazi hiyo,na hyo sio kwa nyanya tu hata ukiagalia msimu wa Parachichi,Nanasi,Machungwa, Ndizi,hata embe kwani Bakheressa naye huwa anazidiwa na msimu wa embe ,Alafu unataka vijana wakalime baada ya kuhitimu vyuo vikuu ,hivi wanafikiri kuwa vijana hao hawaoni changamoto za kilimo nchini? Kijana msomi huwa anafanya kitu kinachoitwa SWOT analysis na kugundua kama changamoto na fursa zipi ziko nyingi kisha kufanya maamuzi.Hii ni nchi ya watanzania ambao kila kukicha wanaamka na kujituma katika shughuli za kiuchumi na uchumi unakuwa kwa kiwango cha asilimia 6 mpaka 7 kila mwaka lakini wanaoukuza huo uchumi wana hali duni kimaisha ,Je serikali haioni kama kuna haja ya kukutana na wadau wa kilimoni na watu wa chini ili kutafakari kwa pamoja hali hiyo?
Serikali yetu na hasa hii ya awamu hii SIO SHIRIKISHI KWA WALENGWA ANGALIA WADAU WA mafao ya kujitoa katika shughuli ya kutafuta kipato au kazini walivyokuja na tamko lao.
SERIKALI HII NI SERIKALI YA VIPOFU.Naomba tuanzishe usemi huu KUIELIMISHA SERIKALI NI KULIKOMBOA TAIFA.
SERIKALI YETU INAHITAJI ELIMU NA MAARIFA KUPAMBANA NA HALI YA UCHUMI NCHINI.
HAIWEZEKANI UCHUMI UKUE KWENYE MAKARATASI TU,CHA AJABU ZAIDI TAARIFA HIYO UTOLEWA NA MAMLAKA ZA NJE KUJA KWETU SISI AMBAO UCHUMI WETU UNAKUA,HII INAMAANISHA KUWA HATA WAPI TULIPO HATUPAJUI.

mimi mkuu naseme kusema hapa kazi na kuanza kusumbua watu njaa ikija siwapi chakula hamfanyi na mengine ni matusi kwa watanzani na kukosa adabu kwa serikali yetu kujenga taifa ni kushirikiana wala si kutishana
 
Kama kweli logic ni kuwa kufanya kazi kwa masaa mengi ndiyo kutoka kimaisha, hebu tujiulize swali moja tu dogo, kuna watu wanaenda 'vibaruani' alfajiri na kurejea majumbani kwao usiku mkali..........

Sasa kama kigezo kingekuwa kufanya kazi kwa masaa mengi ndiyo kuwa milionea, basi hawa wanaojihimu alfajiri sana kuwahi kwenda kuchapa kazi na wanashinda huko makazini kwao mpaka usiku wa manane wakifanya kazi, ndiyo wangekuwa maBill Gates wetu hapa TZ.......

hili ni jambo kubwa sana mkuu mambo yanaenda hovyo sana awamu bado natamani lumumba waje watupe mwajbu
 
Back
Top Bottom