Je Tumejifunza nini na Matukio haya

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Wakati mmoja nchini Burma kulikuwa na maandamano yaliyoandaliwa na wapinzani wa ndani kwa kushirikiana na wanaharakati wengine kipindi hicho hakukuwa na mitandao jamii kama facebook , tagged au twitter wanahabari na wadau wengine waliohitaji kutuma habari pamoja na picha sehemu zingine za dunia walilazimika kubeba taarifa zao kutumia vifaa vingine kwenda mpaka mpakani ambapo walipata huduma za mtandao kisha kuzisambaza kwenye vyombo mbalimbali vya habari pamoja na hayo kulikuwa na upinzani toka serikali ya nchi hiyo kuzuia yaliyokuwa yanaendelea kusambazwa duniani kwahiyo hata mtandao ulikuwa taratibu .

Kitu kama hicho kilitokea tena nchini iran lakini kwa bahati nzuri kipindi hicho kukawa kuna njia nyingi zaidi za kuwasiliana kuanzia blogu , mitandao ya jamii kama facebook , tagged na twitter tena kampuni iliyokuwa inaendesha mtandao wa twitter ulifanya matengenezo ya hali ya juu kwa wateja wao wa nchini irani ili waweze kuwasiliana na dunia ya nje bila matatizo ingawa kulikuwa na matatizo kidogo lakini dunia nzima iliweza kupata habari nyingi kwa mfumo wa picha na maandishi hata sauti ya kile kilichokuwa kinaendelea nchini iran hata kama sio moja kwa moja hata zikipita dakika kadhaa .

Kwa upande wa uchina ndio usiseme sera yao kuzuia baadhi ya vitu ukiwa ndani ya nchi hiyo kwa njia ya mtandao imekwepo kwa kipindi kirefu mpaka siku za moja ya kampuni kubwa za mawasiliano ya mtandao duniani google kutishia kufunga baadhi biashara zake nchini humo , hata pale unapotaka kusajili tovuti au kuendesha tokea nchini humo lazima ikaguliwe ndio ipitishwe sheria zimekuwa kali zaidi kwa watu ambao sio raia wa nchi hiyo lakini wanaendesha biashara zao za mitandao tokea nchini humo kwa mfano wa uchina kinachofanywa kimefanikiwa kwa asilimia kubwa ingawa kumekuwa na upanukaji wa teknologia mbalimbali zinazochangia watu kuweza kufanya baadhi ya vitu lakini hii ni kwa wale wanaojua nini wanafanya .

Na wiki kadhaa zilizopita kuna wanaharakati wa Nigeria waliopanga kufanya maandamano kwenye mji wa Kano muda wa maandamano ulipofika wanaharakati hao walipokea ujumbe mfupi kwenye simu zao za mikono kuahirisha maandamano hayo ilionekana kama ujumbe huo mfupi ulitoka kwa mmoja wa viongozi wa maandamano hayo , kumbe ilikuwa ni mbinu ya kuzima maandamano hayo , ni kweli maandamano hayakufikia malengo hii inahusiana sana na usajili wa namba za simu .

Mfano wa mwisho ni nchi jirani ya Kenya ambapo kuna mtandao wa ushahidi.com mtandao huu ulisaidia sana katika kutafuta habari za machafuko ya kisiasa yaliyotokea nchini humo kwenye uchaguzi uliopita hata kwenye taarifa ya wako baadhi ya nyaraka za ushahidi zimetengenezwa kutokana na ushahidi uliotokea kwa watu kuweka matukio waliyoyaona wao wenyewe kwenye mtandao huo .
Kwa sasa mtandao huo umechanua mpaka mashariki ya kongo kwenye vita ya wenyewe kwa wenye na baadhi ya maeneo mengine , nafikiri karibuni wanaweza kukubali kuungana na google haswa kwenye huduma yao ya google earth katika kuweka matukio na taarifa zingine mbalimbali duniani .

Ukiangalia mfano wa nchi kama burma ambapo tukio lake halikupishana miaka zaidi ya 5 tokea kufanyika tukio kama hilo nchini iran nchi yetu pamoja na wadau mbalimbali kwenye sekta ya mawasiliano kuna mambo mengi ya kujifunza haswa kutokana na kukuwa kwa sekta hii kwenye maeneo kadhaa na watu wengi zaidi kuweza kupata nafasi ya kufanya mambo yao kwa njia ya mtandao .

Hapa kwetu kuna tukio moja liliwahi kutokea huko nyuma nalo ni kuhusu blogu maarufu ya masuala ya habari binafsi za watu ZEUTAMU ni kweli hii tovuti ilifungwa kwanza kuonekana kwa watumiaji wa ndani je kwa kutumia sheria gani kwa sababu sera zetu za masuala ya mawasiliano haziko wazi sana , kuanzia wakati ule tukio lile lilivyotokea ilibidi wadau waende mbali zaidi au chombo kinachohusika n ausimamizi wa mawasiliano kije na sera zinazoeleweka .

Kilichotokea kwenye ZEUTAMU mpaka leo kinaendelea ingawa sasa hivi iko kwa vipande kwa vitu hivyo kuwekwa kwenye blogu mbalimbali au majukwaa mbalimbali kwa kupunguzwa vitu kidogo .

Kuna umuhimu sana kwa wadau wa teknohama kuanza kuangalia matukio ya nchi zingine kama matukio halisi ambayo yanaweza kutokea kwetu au ambayo yameshatokea au hayatangazwi kutokana na kutokuwa na waandishi wa kuweza kuchambua vitu kama hivi kwa lugha ya Kiswahili au watu hawapendi kusoma vitu vinavyohusiana na hivi .

Basi wakati tuko kwenye gia za EGOV hivi ni vitu ambavyo tunaweza kuvijadili kwa uwazi kabisa ni vitu ambavyo tunaweza kuandalia sera zake sasa kuna mitandao mingi inachipukia kila mara , kuna kampuni kibao zinafanya biashara kwa njia ya mtandao bila kufuata sheria zozote za ndani hata kulipia kodi serikali yetu inakosa mapato mengi sana , kuna tovuti za habari zinaibuka kila kukicha bila kufuata sera za habari za nchi hii .
 
Back
Top Bottom