Je! tumechukua hatua gani kukabiliana na Ajali za barabarani

jisanja

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
1,077
2,000
Kumekuwa na ajali nyingi sana barabarani zinazomaliza maisha ya watanzania wengi. Ajali nyingi zimekuwa zikisababishwa na

i)mwendo kasi

ii)ubovu wa magari

iii)uzembe wa madereva

Kwangu mimi imekua ikiniumiza sana kiasi kwamba muda mwingine hadi mtu unaogopa kusafiri maana kila siku lazma usikie ajali mbaya zaidi ya tatu Je!

i)serikali imechukua hatua gani kukabiliana na tatizo hili?

ii)sisi abiria tumekua na mchango gani katika kukomesha ajali hizi?

iii)kuna kipindi nilisikia mabasi yote yanafungwa spid governer...nn kilitokea mpaka zoezi hilo likashindikana?

iv)kazi ya matrafik n nn maana kama gari wanazikagua na kuziruhusu kwamba znaweza kusafir..lakin mbele ya safar gar inapata ajali then uchunguzi ukifanyika wanatuambia chanzo cha ajali ni ubovu wa gari !

Kiukwel hali ni mbaya sana maana sasa hivi ukitaka kusafiri lazma ufikirie mara mbili mbili.
 

Dafugwadu

JF-Expert Member
Dec 24, 2012
3,726
2,000
Dawa ni kuacha kusafiri kwa kutumia magari. Ni mwendo wa kupanda punda tu.
 

jisanja

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
1,077
2,000
Watanzania wengi tunategemea usafir wa mabasi .....lakin sasa hivi hata unapotembea pembezon mwa barabara...unakuta gar inakufuata huko huko....
 

mtarato

New Member
Oct 14, 2014
3
0
watu wafate sheria za usalama barabarani kuovateki kwenye kona madereva waache kunywa huku wakiendesha vyombo vya moto.
 

Descartes

JF-Expert Member
Jul 24, 2013
2,766
2,000
Hatua moja wapo:Kufuta kabisa ile kauli ya "ajali haina kinga".

Madereva wengi husababisha ajali kutokana na uzembe ila wanajifanya ni bahati mbaya.Kwa kutaja sababu chache:

  • Miundo mbinu-barabara iboreshwe pia.
  • Askari usalama barabarani watimize wajibu wao.Magari mabovu yasiruhusiwe kusafirisha abiria (wasiyageuze mitaji ya kuoteshea vitambi vyao) .
 

Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,063
2,000
Matrafik wenyewe wanajificha kichakan kugegedana ghafla unawaona wanaibuka vichakan na kukupiga mkono
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom