Uchaguzi 2020 Je, Tume yaUuchaguzi inaweza kushitakiwa Mahakamani kwa kukiuka Sheria za Uchaguzi au viongozi wake wanaweza kuwajibishwa na Kamati ya Maadili?

PAZIA 3

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
1,026
2,000
Kila mtu anashuhudia mambo yanavyoendelea, kwa uelewa wangu wa katiba ya nchi hii, mwenye kinga ya madaraka ni Rais pekee, He vipi kuhusu watendaji wa Tume ya uchaguzi, hawawezi kuburuzwa korotin kwa kukiuka Sheria na Kanuni za Uchaguzi zilizoweka kwa mujibu wa katiba ya nchi hii?

Nani mwenye mamlaka ya kuishtaki tume?

NB; Kama tume inaweza kushitakiwa, naomba wanasheria wa CHADEMA na vyama makini viwashtaki hawa watendaji katika mahakama ya katiba kabla hawajasababisha fujo zisizo za lazima
 

mshunami

JF-Expert Member
Feb 27, 2013
4,166
2,000
Sahihi kabisa
Swali la muhimu. Wamewaengua wagombea kwa dhuluma kabisa! Je hawawezi kushitakiwa? Wameonyesha wazi kukibeba ccm na wagombea wake. Je hilo linapita hivihivi bila kushitakiwa? Sheria yasemaje? Tume ipo juu ya sheria? Je, ni lazima anayeshitaki awe aligombea akadhulumiwa au kila mwananchi aweza kuifungulia tume kesi mahakamani? Yawezekana sasa au ni baada ya uchaguzi!
 

Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,562
2,000
JE TUME INAFUATA HAYA KAMA SHERIA INAVYO HITAJI !?.


4.0 Maadili kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
4.1 Yanayotakiwa kufanywa na Tume
Mambo yanayotakiwa kufanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni pamoja na-
(a) kupanga, kusimamia na kuendesha uchaguzi katika misingi inayowezesha uchaguzi kuwa huru na wa
haki;
(b) kuzingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, sheria za uchaguzi na
sheria nyingine za nchi;
(c) kuvipatia vyama vya siasa ratiba na taarifa za uchaguzi kwa wakati;
(d) kutoa elimu ya mpiga kura nchi nzima, kusimamia na kuratibu taasisi za watu wanaotoa elimu ya
mpiga kura. Aidha, utoaji wa elimu ya mpiga kura utazingatia mahitaji maalum;
(e) kutoa mafunzo ya kutosha kwa watendaji wanaohusika na uchaguzi ili kuwawezesha kusimamia na
kuratibu uchaguzi kwa ufanisi. Mafunzo hayo yatajumuisha elimu ya jinsia na namna ya kuwahudumia
wanawake, wazee na watu wenye ulemavu;
(f) kuvipatia kwa wakati vyama vya siasa kanuni, maelekezo ya Tume, nakala ya Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura na nyaraka nyingine za uchaguzi zinazotakiwa;
(g) kukemea vitendo vyenye nia ya kuharibu uchaguzi vinavyoweza kufanywa na viongozi wa vyama vya
siasa, wagombea na wafuasi wao, Serikali au vyombo vyake;
(h) kuratibu matumizi ya vyombo vya habari vya umma ili kutoa fursa sawa kwa wagombea Urais na
Umakamu wa Rais na vyama vyao;
(i) kuendesha zoezi la uchaguzi kwa uwazi na uadilifu;
(j) kuratibu kamati za kusimamia maadili ya uchaguzi pamoja na kusimamia utekelezaji wa maamuzi
yanayotolewa na kamati hizo;
(k) kukutana na wawakilishi wa vyama vya siasa mara kwa mara pale itakapowezekana kujadili masuala
mbalimbali yanayohusiana na kampeni za uchaguzi na uchaguzi wenyewe;
(l) kuhakikisha kuwa hakuna mtendaji wa uchaguzi atakayefanyiwa uonevu au kukoseshwa haki kutokana
na utendaji wake katika shughuli za uchaguzi anazozifanya kwa mujibu wa sheria;
(m) kuhakikisha kwamba watendaji wa uchaguzi wanatambua majukumu ya mawakala na wagombea na
haki yao ya kuwasilisha pingamizi au malalamiko iwapo ukiukwaji wa sheria na taratibu umetokea;
(n) katika kipindi cha uteuzi wa wagombea, upigaji kura na katika hatua yoyote ya mchakato wa uchaguzi,
watendaji wa Tume watatakiwa wakati wote kuwepo katika maeneo yao ya kazi; na
(o) kuandaa na kupeleka kwa wakati vifaa vya kutosha kwenye vituo vya kupigia kura.
4.2Yasiyotakiwa kufanywa na Tume
Mambo yasiyotakiwa kufanywa na Tume ni pamoja na-
(a) kupendelea chama chochote cha siasa au mgombea yeyote;
(b) kubadili ratiba za kampeni za uchaguzi bila kushirikisha vyama vya siasa;
(c) kuchelewa au kupeleka vifaa pungufu katika vituo vya kupigia kura bila sababu za msingi; na
(d) kuchelewa kutangaza matokeo ya uchaguzi bila sababu za Msingi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom