Uchaguzi 2020 Je, Tume ya Uchaguzi ya Tanzania haijandaa karatasi zenye majina ya wagombea za kupigia kura? Au zimeandaliwa za namna nyingi?

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,338
6,463
Leo asubuhi nemesikia kwenye redio ya East Africa, kwenye kipindi cha Supa Breakfast mambo ya tume ya uchaguzi ya kustaajabisha. Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi akiwa Mara na kusema wagombea wanaotumia lugha ya matusi na uchochezi kwenye kampeni wataondolewa kwenye karatasi ya kupigia kura. Yaani hakutakuwa na picha na majina yao.

Maswali:


1. Je, yale maandalizi ya asilimia 80% kufikia mwezi jana hayahusishi karatasi za kupigia kura?

2. Je, kama karatasi za kupigia kura zipo tayari, je wametoa aina tofauti tofauti kwa kulenga baada ya kutabiri kuwa baadhi ya wagombea watatumia lugha chafu?

3. Hizi karatasi zina ubora gani kutofautisha na fake? Hizi karatasi zinaandaliwa/ ziliandaliwa wapi?

4. Je, hii sio mbinu nyingine ya 'enguaengua'?

5. Je, haya ndio matumizi ya dola kubaki madarakani?
 
Hivi Huyu Mkurugenzi anajuwa anakoipeleka Tanzania?
Asubutu kutowa karatasi ambazo hazina kichwa cha Mtu wetu aone kiama chake, kama hatutagawana mbao na itakuwa ndio mwisho wake kwa kusababisha Vurugu lisilomithilika.

Tutayanukuu maneno yake haya ili tupate ushahidi wa kumfikishia the Hague-Mahakma ya kimataifa.
 
Watakuwa na makaratasi tofauti tofauti kulingana na hali itakavyowaendea tume. Kuna uchakachuaji wa ajabu unaendelea tusikubaliane na haya wananchi.
 
Ushamba tu huo kujadili na kulaumu mambo msiyo yajua, Kuna mashine za offset zinachapa documents 5000/30min sasa hapo hofu ya nini mashine ikiwashwa 18 hours ni documents 180,000.

Acha kukimbilia kutisha watu sijui mahakama za kimataifa hiyo kitu haipo na Serikali haifanyi kazi kwa shinikizo la watu.
 
Tulipokaa kimya wakati wa enguaengua ya wagombea wa upinzani tuliipa uhalali tume kufanya ushenzi kwenye mchakato wa uchaguzi.

Nilishasema na nitaendelea kusema ili tume itende haki tunapaswa kuilazimisha itende haki kwa vitendo siyo maneno ya kwenye keyboard.
 
Back
Top Bottom