Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,435
- 5,404
Ndugu zangu,
Kuna mambo kadhaa ambayo yanaendelea katika uchaguzi huu ambayo naona ni hatari sana kwa mustakabali wa demokrasia yetu. Wagombea wengi sana wameenguliwa na tume kwa vigezo mbalimbali ikiwamo swala la idadi ya wadhamini, kukosea kujaza fomu katika maeneo machache na sababu nyingine nyingi ambazo kimsingi hazina mantiki hasa ukizingatia kwamba kazi ya tume sio kuwachaguliwa wananchi viongozi kwa kutumia vigezo vyao bali kazi yao ni kusimamia uchaguzi.
Binafsi naona tatizo kubwa sana ambalo tume inalileta ambalo athari yake hatutaiona sasa hivi bali tutaiona baada ya uchaguzi huu. Kama tume haitachukua hatua madhubuti mambo mengi sana ambayo hatuyataki yatokee yanaweza kutokea katika nchi hii.
Maoni yangu kwa tume ni haya:
Kwanza, tume itambue kwamba kipindi cha uchaguzi ndo kipindi ambacho wananchi wanaweza kuwa na mijadala ya wazi kuhusu mustakabali wa nchi yao bila kujali kiwango chao cha elimu n.k. Hivyo basi kuwanyima wagombea kushiriki katika uchaguzi ni sawa na kuwanyima fursa ya kuwa sehemu ya mjada huu muhimu. Je, tume inafanya haya kwa maslahi ya nani?Inataka kuharibu uchaguzi kwa maslahi ya nani? Kwani tume inawalipia hao watu gharama za kampeni?Kuna gharama zozote tume inazipunguza kwa kuwakata?
Tume iache hili suala liende kwa mujibu wa haki za raia na wale wote waliotia nia kugombea bila kujali kama walifikisha vigezo au la waruhusiwe kugombea kama kweli wanathamani amani ya nchi yetu.
Haya ni maoni yangu binafsi na tunaweza kuyajadili kwa pamoja na kukubaliana au kutokubaliana.
Asante