Je, Tuliwatuma Bungeni Kushukuru Familia, Jamaa na Marafiki au tuliwatuma kuwakilisha maoni ya wapiga kura?

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,099
Wanabodi, Mimi sio mtaalamu wa lugha ya mawasiliano"Communication skills".Ingawa natambua kwa kila neno utakaloongea au kuropoka (Transfering message) lazima usubiri mrejesho mzuri au mbaya( Feedback)

Mbunge umepewa dakika kumi za kujenga hoja na kutoa suluhisho la matatizo Bungeni, Unatumia dakika tano kumsifia Mkuu wa nchi kuwa ameshinda kwa kishindo wakati yeye mwenyewe Mkuu wa nchi alisema hataki kusifiwa kwani kama sifa alishasifiwa sana anahitaji kazi ionekane na dakika tano zilizobaki unatumia kuwashukuru watoto wako, Baba yako, Marafiki mliocheza nao rede, kombolela na wote ulioimba nao nzu nzu we Mama nyuki lia eeh, luka mbali kutafuta ua nzuri la asali na dakika kumi zinakuwa zimekwisha, Hii sio sahihi kabisa

Nakuomba ndugu Humprey Polepole natambua wewe unafahamu jambo hili na miezi michache iliyopita nilikuona pale udsm kwenye taasisi ya "Institute of Development studies" au IDS ukimalizia PhD yako .Naomba uwape semina hawa wabunge wetu kwa kutumia uwezo wako toka hapo IDS ambapo marehemu Prof. Mpangala alikuwa akishusha nondo miaka hiyo

Kwa dakika kumi yampasa Mbunge atumie dakika tano kuchambua tatizo na kulielezea nini chanzo na madhara yake kiuchumi au kijamii hapa akihusisha na mazingira ya jimbo lake au nchi kwa ujumla.Yampasa mbunge kushawishi wabunge wenzake juu ya ukubwa wa tatizo na athari kiuchumi au kijamii

Dakika tano za mwisho Mbunge yampasa atoe suluhisho jinsi ya kutatua tatizo hilo kwa mifano halisi au kwa nadharia. Nguvu yake ya ushawishi na suluhisho ndio hupelekea hoja yake kukubalika mbele ya Bunge na wananchi


Ni muhimu kabla ya kuingia Bungeni wabunge wakafanya utafiti hata wa kupokea takwimu na Data toka kwenye taasisi au Majimboni kwao. Kutumia dakika kumi kusifia na kushukuru bila kujadili mustakabali wa nchi yetu sio sahihi, Leo hii dunia inasonga mbele kwa teknolojia ni muda wa kujadili mambo yafuatayo

Mosi, Lini tutapeleka chombo chetu katika anga la juu. Tutatumia watu gani na kwa muda gani?

Pili, lini elimu yetu tutaifungamanisha na teknolojia ya kisasa ili kuzalisha watendaji na sio wasimamizi

Yote Dkt Charles Kimei alijitahidi sana kuelezea kuhusu ishu ya elimu yetu kuwa lazima iwe elimu ya kuwawezesha vijana kufanya kazi kwa teknolojia ya kisasa na Bodi ya mikopo iwekeze kwenye mfumo huo wa elimu

Mwisho, Wapiga kura na wasiopiga kura hatukuwatuma Bungeni kusifia na kushukuru kwa dakika zote unazopewa, Tuliwatuma kujenga hoja na kutoa suluhisho la matatizo
 
Wanatuona wajinga sana, ipo siku, wameligeuza lile jengo la Bunge kama ukumbi wa kufanyia send-off.

Hata hawaumizi vichwa kufikiria namna ya kuwasilisha matatizo ya wananchi wao na kuyatafutia ufumbuzi, wao wanajua wakiongea pumba, au wasiongee chochote mwisho wa siku posho ipo, na mwisho wa mwezi mshahara upo,

Pangekuwepo na namna ya kupima performance ya mbunge akiwa bungeni ili ku-determine kama next term arudi au asirudi ingesaidia sana, kina Tale wangejuta kukimbilia bungeni.
 
Wanajua walipata ubunge kwa namna ambayo wameupata hivyo lazima watoe shukurani kwa wale waliowawezesha kupata ubunge.
Ukiangalia bunge Sasa hivi lina ukakasi mkubwa.mm hilo swala la mbunge kuwashukuru wazazi,wake, Rais nk linanitia shombo Hadi muda mwingine naamua kubadilisha stesheni.

Wabunge wanautumia muda wao vibaya.wanaacha kujikita kwenye mada wanaanza kupongezana na mambo yasio na tija wakati sisi wananchi tuko ktk lindi la umaskini tukisubiria matokeo chanya ya suluhisho la shida zetu.
 
Ndio Wabunge wetu wengine Wanajisifu Kuzaa Watoto Wawili ndani ya Bunge kwa Miaka 5
 
Siwezi angalia hilo bunge hata kama sina kazi ya kufanya.
 
Wabunge sio watetezi wa wananchi,sana sana wanatetea posho zao.
Watetezi wa wananchi hawana majina makubwa wala hawajisufu,wako mitaani na vijijini, nyumba za ibada,mashuleni,viwandani,mashambani,majeshini,mahospitalini.n.k
Wabunge wetu kazi yao hasa wanapitisha miswaada ya serikali,ni mara chache kujadiri na kupitisha hoja binafsi.
Tusema ubunge ni kutafuta mlo mnene wa familia na kutafuta kinga ya kusumbuliwa na serikali.
Bila bunge inawezekana,tutapunguza gharama za wanaokula bila kunawa.
 
Ulitegea tofauti na unayoyasikia na kuyaona.
Wameokotwa hao majalani huko, na kukusanywa Dodoma. Pole yetu Watanganyika, kodi zetu zinatumika kiwendawazimu sana.
 
Wewe ndiye uliyekuwa unaandika hapa kila siku kuwa mtashinda kwa mbinu a.k.a SHIKWAMBI.

Sasa acha hao wapumbavu wenzio wakuoneshe SHIKWAMBI manaake nini.

ACHA UNAFKI WEWE LICCM SHANGILIA BUNGE LAKO KWA MBINU. (SHIKWAMBI)
 
Dr Gwajima alitumia dk 7 kati ya 10 kumsifu Magu,Mumewe na watoto wake na dk tatu zilizobaki aliongea utumbo kuhusu upatikanaji wa dawa
 
Wewe ndiye uliyekuwa unaandika hapa kila siku kuwa mtashinda kwa mbinu a.k.a SHIKWAMBI.

Sasa acha hao wapumbavu wenzio wakuoneshe SHIKWAMBI manaake nini.

ACHA UNAFKI WEWE LICCM SHANGILIA BUNGE LAKO KWA MBINU. (SHIKWAMBI)
Nimecheka sana yote maisha na kweli mbinu zilitumika tena zilizoboreshwa zaidi

Shikwambi

Shikwambi ni mbaya sana
 
Kabla sija comment lolote kwanza naomba nitoe shukrani kwa walionipa raha na furaha leo.
Shukrani ya kwanza naipeleka kwa mke wangu kwa utamu alionipa jana usiku na kunipikia chakula kizuri na kitamu mda wote wa siku ya Leo na nikapata nguvu ya kuingia hapa JF.

Shukrani ya pili naipeleka kwa mwanzilishi wa JF , shukrani ya tatu na ya mwisho naipeleka mwa alieleta uzi huu, na kumwambia kuwa vilaza Ni wengi Sana mjengoni, kazi yao Ni kusema mitano Tena.
 
Kwani hawa walitumwa na watu au walipelekwa na mtu wanayemsifia?
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom