Je tukubali Yaishe au tuendelee kuwahudumia wagonjwa...? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je tukubali Yaishe au tuendelee kuwahudumia wagonjwa...?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Gembe, Jul 11, 2008.

 1. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Baada ya jana Serikali kutoa yamko kwamba unga unga ulikuwa hauna madhara yoyote,na baada ya kusema pia kwamba hakuna mtu alikuwamo ndani,na kwa kuwa Chenge siyo aliyedhaniwa aliweka unga wa kimazingara.

  Tumeendelea kulazimishwa kufungwa bao la lazima bila sababu,tunazugwa kwa kisingizio siye mandondocha.na bado kuna ambo kama haya aliyoyasema Mzee Mwanakijiji kipindi cha nyuma

  Angalia matukio haya ya Lowassa alivyojiuzuru na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi yake,Pia angalia suala la Kina Karamagi walivyosaini mikataba huko Uingereza,Tume ya maadili iliwachukulia hatua zipi?Je kujizuru kunatosha?ina maana ni Ruhusa watu kuendelea kusaini mikataba nje?

  Wapo wengi tu,wale waliohusika na kamati ya RDC,hawa walituingiza katika hasara isiyosemekana naukiangalia tumelipa pesa nyingi sana ,million 152 kwa siku kwa zaidi ya mwaka ni mabilioni mangapi.Leo wanavunja Mkataba bila kusema kama pesa yetu inarudishwa au vipi?

  Nakumbuka ilifikia MWanakijiji Kutamka maneno haya
  Mie nimefikiria sana,nimekaa katika CCM kwa muda mrefu na sasa kama wanaendelea hivi wakati nikifikiria kukiacha chama changu ninachokipenda,Mwalimu alishwahi kusema CCM siyo mama Yangu na kikiacha misingi ya utawala wa haki na ulio bora nitakiacha.Chama kimekosa siasa bora,watu makini na leo nafikiria kukiacha....Mwanaakijiji naomba ushauri?Je niachane na siasa.

  Angalia Kesi ya wale wabunge wa CCM wa Arusha jinsi walivyopelekwa mahakamani na leo wameachiwa bila kuonekana na hatia,Je aliyewakamata kwamba wana Rushwa amechukuliwa hatu gani?Je aliwaonea?kwanini alifanya hivyo?Nataka huyu Kamanda wa PCCB ajiuzuru au atueleze ukweli kuhusu kilichotekea.

  Mwanakijiji ulishafunga Mjadala ila hapana leo naufufua na nakumbuka maneno haya uliyoyasema November 2007 wakati Jambo ikiwa inakamata kama sasa,wakati kada akiwa na shauku ya kutetea anachokiamini.Naurudisha na naomba watuambie mambo yote ambayo wanatuzuga.

  Mie naumia sana,na sasa naomba tuamue,Je tujiunge nao au tuendelee kuwahudumia wagonjwa kwa pesa zetu
   
Loading...