Je tuendelee kuwaamini walimu wa watoto wetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je tuendelee kuwaamini walimu wa watoto wetu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Aug 12, 2011.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,427
  Likes Received: 22,347
  Trophy Points: 280
  MWALIMU wa Shule ya Msingi ya Kwamaksau
  iliyopo Useri, Wilaya ya Rombo, mkoani
  Kilimanjaro anatuhumiwa kuwalawiti
  wanafunzi sita wa kiume kwa nyakati
  tofauti baada ya kuwarubuni kwa kutumia
  vishawishi mbalimbali.
  Vishawishi hivyo ni pamoja na kuwapa
  fedha, kuwatafutia ada na wengine akiwapa
  chakula kingi cha mchana wawapo
  shuleni.Hata hivyo Kamanda wa Polisi Mkoa
  wa Kilimanjaro, Absolom Mwakyoma alisema
  uchunguzi wa awali wa polisi unaonyesha
  kuwa kitendo wanachodaiwa kufanyiwa
  wanafunzi hao si kulawitiwa bali
  kushikwashikwa korodani zao.
  “Tusiwe wepesi wa kuwalaumu polisi bila
  kuwa na uhakika na kile tunachowalaumu
  nacho, mimi nimefika mwenyewe shuleni
  hapo na nimezungumza na daktari
  aliyewafanyia uchunguzi na vipimo
  havionyeshi waliingiliwa,” alisema.
  Mwakyoma alifafanua kuwa tuhuma kuwa
  kila mara mtuhumiwa huyo anapofikishwa
  polisi huachiwa si sahihi kwani amekuwa
  akifikishwa mahakamani na anapopewa
  dhamana na mahakama, wananchi
  wanadhani ni uamuzi ya polisi.
  Mzazi wa mmoja wa mtoto wanaodaiwa
  kulawitiwa alidai mtoto wake ambaye yuko
  darasa la saba shuleni hapo alifika
  nyumbani na kumweleza kuwa mwalimu
  alimpa Sh500 na kumwingiza ‘stoo’ na
  kumfanyia kitendo hicho.
  Mzazi huyo, alidai mtoto wake alikuwa na
  rafiki yake ambapo wote walipewa Sh500
  kwa ajili ya kufanyiwa kitendo hicho na
  kuwa mwalimu huyo alipomaliza kumfanyia
  mmoja alimchukua mwingine na kuanza
  kumfanyia.
  “Mtoto wangu alikuja nyumbani akiwa
  anachechemea huku akiwa hawezi
  kutembea vizuri na nilipomuuliza ndio
  akaanza kunielezea kilichomtokea na
  nikampeleka hospitali Ngoyoni ambapo
  alilazwe siku mbili kwa kuwa alikuwa
  amevimba sehemu za siri,” alidai baba huyo.
  Aidha alidai hali ya mtoto huyo bado ni
  mbaya kwa kuwa bado ana maumivu
  makali, ambayo yamesababishwa na
  kuvimba kwa sehemu za siri kutokana na
  kufanyiwa kitendo hicho kwa muda mrefu.
  Kwa mujibu wa mzazi huyo alidai kuwa
  mwalimu huyo aliwachukua wanafunzi
  wawili na kuwafanyia kitendo hicho kwa
  kuwapa kiasi cha Sh1,000 wote wawili na
  kwamba mtoto wake hali yake ni mbaya
  lakini mwenzeke anaendelea vizuri.
  Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa Wilaya
  hiyo, Peter Toima alithibitisha kuripotiwa
  kwa matukio hayo na kwamba tukio hilo
  lilitokea Julai 27 mwaka huu ambapo
  mwalimu huyo alilawiti watoto wawili kwa
  wakati mmoja.
  Toima alisema kuwa mwalimu huyu alilawiti
  tena watoto wengi wawili mwezi Mei na
  wengine mwezi Aprili mwaka huu.
  Mkuu huyo alisema kitendo hicho
  kilisababisha wakazi wa eneo hilo
  kuandamana na kufika shuleni hapo ili kwa
  lengo la kutaka kumchoma moto ila polisi
  waliwahi na kumwokoa na kuweza
  kumpeleka katika kituo cha polisi.
  “Hili ni jambo la kusikitisha kwa kuwa
  mwalimu huyo amekuwa akihamishwa
  hamishwa shule kutokana na kitendo cha
  kulawiti watoto wa shule na huwa
  anawafanyia watoto wa madarasa
  mbalimbali,” alisema Toima
  Alisema wazazi hao waliandamana shuleni
  hapo Agosti 2, kwa lengo la kutaka
  kumchoma moto mwalimu huyo ila polisi
  waliwahi na kumwokoa mwalimu huyo na
  kwamba mwalimu anashikiliwa na polisi .
  Toima alizitaja shule za msingi ambazo
  mwalimu huyo amewahi kufundisha na
  kudaiwa kufanya matukio hayo kwa
  wanafunzi kuwa ni ni shule ya msingi
  Kimwingeni, Kiserini, Keni Mengeni na
  Ubetu.
  Mkuu huyo alisema mwalimu huyo akiwa
  anafundisha shule ya msingi alimlawiti
  mtoto mmoja ambaye alijulikana ambapo
  alikunywa sumu baada ya kufanyiwa
  kitendo hicho na mwalimu huyo na hivi sasa
  ni marehemu.
  Wazazi wa watoto hao wameiomba Serikali
  kumchukulia hatua kali mwalimu huyo na
  hata ikiwezekana kufukuzwa kazi hiyo kwa
  kuwa hafundishi bali anawaharibu watoto.
   
 2. Vmark.

  Vmark. JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2011
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 1,361
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Yesu na maria! Aisee huyu ticha akiachiwa tu labda ahame na mkoa kabisaa! La cvyo lazima apigwe fire au naye afanyiwe hako kamchezo! To hell wit him!
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,427
  Likes Received: 22,347
  Trophy Points: 280
  watoto badala ya kufundishwa taaluma wanafundishwa ushoga
   
Loading...