Je, tuanze kujadili uwezekano wa kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa/Mseto?

andoza

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
1,952
2,000
Habari za wakati huu,

Najua kwa wenye macho tayari wameanza kuona kitu hakiko sawa. Kwa wale waelewa tayari wameanza kuona dalili za nchi kupoteza uelekeo.

Nianze kwa kuelezea hali ya Upinzani. Upinzani wa mwaka huu sio sawa na wa miaka ya nyuma. Ni upinzani uliokomaa, na ulio tayari kwa lolote. Upinzani wa mwaka huu haujajengwa juu ya majina na haiba za watu bali umejengwa juu ya mawazo, matamanio na matarajio ya wananchi. Wananchi wengi wana hofu kubwa sana kuhusu uchaguzi wa mwaka huu kwani unagusa maslahi mengi sana kiasi kwamba ni vigumu kwa mwananchi wa kawaida kuamua hasa achague nini?

Kwa miaka mitano ya Magufuli kuna mambo yamefanyika vibaya sana na mengine vizuri. Ukiyaweka katika mizania inakuwa ni vigumu sana kuamua jambo ambalo ni bora zaidi kuliko jingine. Kwa mwananchi wa kawaida ambaye hajui takula nini leo ni vigumu sana kuamua kwa uhuru na uhakika kwani akitazama magumu aliyopitia kwa miaka mitano anatamani asimchague Magufuli na wakati huo huo akiona baadhi ya miradi michache iliyofanywa kwa kipindi hiki ambayo inapigiwa kelele sana anatamani amchague. Akimtazama Tundu Lissu anaona tumaini jipya na anatamani amchague na akifikiri kwamba ni upinzani anajikuta anapatwa na hofu kubwa.

Kwa ufupi mwananchi mpiga kura wa kawaida hawezi kufanya uamuzi wa uhakika katika uchaguzi huu. Ni uchaguzi mgumu kwa wagombea na wapiga kura na wasimamizi.

Swali la kujiuliza ni je, sasa ni wakati wa kuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu uhitaji wa kuunda serikali ya UMOJA WA KITAIFA amapo CCM na CHADEMA watakaa mezani na kuunda serikali?

Je, kama tutafikia hatua hio je nani atafaa kwa nafasi gani katika Serikali hiyo kwa upande wa Chadema? Je, uamuzi huo unaweza kuimarisha demokrasia na mshikamano wa kitaifa?

Haya ni baadhi ya maswali ambayo natamani sana tuyajadili katika misingi ya HAKI, USAWA na MAENDELEO ya taifa letu.

Karibuni kwa mjadala
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom