Je, Toyota IST itanifaa kwa urefu wangu wa 6. 1 feet?

Joel360

JF-Expert Member
Sep 21, 2013
981
631
Habari za saa hizi members wa forum ya magari.

Najua humu kuna wazoefu wa Gari aina ya Ist. Ndio gari yangu ya kwanza nnayotaka kuinunua kwa sababu tatu.
I. Utumiaji mdogo wa mafuta (nachukua yenye cylinder ya 1300)
II. Nimeambiwa Haichemshi kwa safari za Dar - Moshi.
III. Upatikanaji rahisi wa spair na mafundi ni rahisi.

Tatizo mie mrefu wa 6.1 feet, wasi wasi wangu ni je, ntaweza kutoshea mule ndani kwa kuzingatia nafasi ya miguu na nafasi ya kichwa ?

Nimeona niulize kwa kuwa nimekosa mtu mwenye ist nijaribie kuingia. Ntashkuru sana kwa majibu yenu.

Au pia unaweza kunisaidia kama una ist na unaishi mwenge au sinza, basi nije nijaribu kuingia kwenye gari lako ni-assume kama naendesha vile ili nione kama natoshea.
 
Unatoshea bila shida, binafsi nina futi 5.8 kama sio 5.9...na niliendesha ist ya rafiki yangu nikatoshea feshi tu wala sikuona taabu....ila atakaye pata taabu ni abiria wa kiti cha nyuma ya derwva endapo ninmrefu, halafu ikutw mnasafiri kwenda mbali, aisee ataisoma namba...
 
Tatizo magoti akiadjust seat kusogea na stealing, Au hata akikirudisha nyuma mikono itauma maana atakuwa anatumia nguvu kunyoosha due to distance

Warefu waone hivi hivi wanaumiaga kwenye hivo vigari ila wanauchuna
Nashkuru sana Diana. Mi najua una nia njema sana dada yangu ila unanifanya nisielewe cha kufanya, maana wengine wananitia moyo wewe unanipa ukweli mchungu sasa najikuta nipo katikati. Mwishowe ela yenyewe NTAILA sasa😂
 
Nashkuru sana Diana. Mi najua una nia njema sana dada yangu ila unanifanya nisielewe cha kufanya, maana wengine wananitia moyo wewe unanipa ukweli mchungu sasa najikuta nipo katikati. Mwishowe ela yenyewe NTAILA sasa


Ongezea ongezea mkuu mwaya uchukue SUV
 
Back
Top Bottom