Je, tofali 2800 zinatosha kujengea nyumba ya vyumba 3 na kila kitu ndani?

Mimi hata elfu 10 hamna kabisa na nyumba imesimama vyema fundi nilimuita nikamueleza nataka hivi na hivi na hivi na yeye akaongezea duuuh MBONA MAMBO MAZURI IMESIMAMA MPAKA JIRANI KANIULIZA HII RAMANI MBONA BEI SANA!!! Nilimwambia ndio 500k kumbe BURE TU

ila mwisho wa siku kila mtu ana njia zake mimi nilienda kwa kampuni kabisa nanilikua najenga ghorofa so nilikua muoga wa kuharibu mambo
 
Unatafuta uhalali au unatafuta market price?
Market price 10 to 50 Gs unapata michoro ya manispaa. Thats a fact, na inapitishwa.....
Wanakiuka taratibu na sheria za ujenzi,kilicjopitishwa ndicho kinatakiwa kujengwa na si upuuzi wa hivyo kuharibu soko la wasomi wa architecture kwa ajili ya kupata vimapato vya Halmashauri
 
Michoro ya manispaa huku mitaani tunamaanisha architectural na structural drawings za kuombea building permit.
They are like 80% recycled.
And 80% ya nyumba zinazojengwa hazitumii michoro.
Mimi nafahamu Halmashauri fulani wanafuatilia kila inavyotakiwa ndio upewe kibali cha ujenzi sio hiyo ya kutoa photocopy
 
Kwan ukubwa wa vyumba upoje (aina tofauti ya ukubwa wa vyumba ktk nyumba ni nyingi ) vipimo vyake vipoje
 
Unaenda mbali sana, ramani siku hizi tunapata kwa 10K.
Kadri siku zinavyoenda ndio umuhimu wa ramani zenu unapungua, watu waliosoma Civil Eng nao wanachora ramani siku hizi, architects nao wanachora unakuta mpaka masela wangu wa electrical nao wamo. Yaani ilimradi vurugu tu.

Auto CAD na zinginezo zimekuwa kimeo, kuna jamaa yangu kasoma account naye saiv anachora ramani tena za hali ya juu.

Sikukatishi tamaa ila hiyo bei umeweka kwa matarajio makubwa sana
Aisee pale Kamanga (mwanza) kuna jamaa amechora ramani zake kwa mkono (kwenye karatasi za A3) anakuuzia kwa 10K na hesabu anakupa kuanzia tofali, bati, mifuko ya cement, kokoto, mbao na mazaga mengine yote. Wewe unasema tu unataka ramani iwe na nini na nini
 
Aisee pale Kamanga (mwanza) kuna jamaa amechora ramani zake kwa mkono (kwenye karatasi za A3) anakuuzia kwa 10K na hesabu anakupa kuanzia tofali, bati, mifuko ya cement, kokoto, mbao na mazaga mengine yote. Wewe unasema tu unataka ramani iwe na nini na nini
So Hizo hesabu anafanya bila kuona kiwanja, of which kama kiwanja kina slope tayari ni utapata hesabu tofauti,
Na vipi kama kiwanja kipo sehem ambayo ni damp au water table ipo juu hato kuwa na kitu cha kurecomend kwenye michoro, na vipi kuhusu stability ya ardhi/udongo ya eneo husika. Na hiyo michoro haitokua na ‘site plan’ yako kulingana na kiwanja husika so ni ishu kwenye kupata vibali maana hapo hakutakua na calculated builtup area ....n.k
 
Nyumba ya vyumba vitatu kwa wastani ina urefu wa mita 15 na upana mita 10. So mzingo ni kama (15x4) + (10x4) = 100 meter.
Hii ina maana kuta zote za nyumba ukizijumlisha na kuziweka kwenye mstari mnyoofu zitachukua urefu wa mita mia. Kila mita ina kula tofali mbili. Nyumba itahitaji urefu wa tofali kumi. So kwa ujumla matofali yatayotumika ni 100x2x10 = 2,000. Kwa kusimamisha.
Uki adjust uwepo wa milango na madirisha, 2,000 x.75 = 1,500.
Iwapo msingi zitaingia kozi 6 kwa wastani, 100x6x2 = 1,200.
So 1,500 + 1,200 = 2,700.
Hapo kuna kozi tatu baada ya linta: 100×2×3 = 600.
In total utahitaji tofali around 3,300.
 
Inavyotakiwa ndiyo ipi hiyo; Hebu
Inavyotakiwa ndiyo ipi hiyo; Hebu tuelezee
Kuna mdau kaeleza aina zote za michoro inayohitajika. Kwa kuongezea ni kuwa kwenye mchoro wa site plan ambao ndio unaonesaha namna nyumba itakavyokaa kwenye kiwanja husika ambapo wao wataangalia setbacks za jengo kwenye kiwanja (mara nyingi haitakiwi kupungua 1.5m), na plot coverage (kuna kiasi wanachotaka kifikiwe na kisipungue inatofautiana kulingana na eneo unalojenga) pia builtupa area ndio wanatumia kukuchaji kiasi cha kulipia kwenye vibali na kama kiwanja kimepimwa baadhi ya halmashauri huhitaji kuonesha block plan pia
 
5F5FC0A7-0B22-4CA9-A72B-EC9072A8D7EA.jpeg


Hiyo ni moja ya ramani ambayo ipo very economic but classic and modern. Inachukua tofali 985 kwa kozi sita za msingi na tofali 1,590 za juu (jumla tofali 2,575) na bati 65 tu. Unaona area coverage yake ilivyotumika vizuri.

Watu wengi wanafikili kuwa ramani huchorwa in just one take then kitu kimekamilika anakbidhiwa mteja
Kumbe ukweli ni kwamba baada ya mtaalamu kufika site kuona eneo husika then mnashauliana kisha kinatolewa kitu relevant na mteja anatoa comments zake kisha zinafanyiwa marekebisho kwa kushauliana baina ya pande mbili, na mteja akiwa very specific and directional basi mnaweza kufanya marekebisho mpaka mara tano ili kupata kitu ambacho kinampendeza mteja (inaweza kuwa mume na mke) na kina kizi matakwa ya kitaalamu based on site features. Then hizo ramani ndio wakiziona watu huko hupapatika na kuzitaka kwa Tsh elfu kumi, yani hata haujui ni nini kilichopelekea mpaka kufikia hiyo final design unayoiona. Mtu alie wahi kujenga kwa ramani (iliyochorwa kwaajili yake kwa kuzingatia kiwanja) sio rahisi sana akaja kujenga bila ramani na ndio maana hata katika kazi hizi wateja wengi tunawapata kwa connection za wateja wetu wa zamani. Suala la professionalism bongo bado sana ndio maana hata mtaani watu wanalizwa mamillioni kisa uliona ni expensive kumpa mwanasheria laki mbili akuchekie ishu yako kisheria, au mtu anaamua kumeza tu madawa kisa anaona hospital ataongeza gharama...etc, We are still very far........
 
Hiyo 10K unamaanisha 10,000 au 100,000? Kama ni ten basi huo ni uongo ulikithiri labda kwa wanafunzi wa chuo

Pia unless ni ramani za kujenza kwenye slums ila kama ni ya kujenga kwenye plots zilizopangwa hakuna kitu kama hicho
We jamaa ramani za bure zipo nyingi tu na zina vipimo na kila kitu, na ukitaka kuchorewa kwa sasa vijana wanachora hata kwa 10,000/ Autocad na archcard sijui master series saihi had wadada wana stationery wanazijua na wanakuchorea ramani safi kabisa hata kwa 10,000/= floor plan na elevations za pande zote ha 3D
 
FAHAMU MAKISIO YA GHARAMA ZA UJENZI WA NYUMBA YAKO (+255-657-685-268)

Fahamu gharama ujenzi wa nyumba yako kwa kila steji kama MSINGI, KUTA, PAA, RANGI, DARI, MAJI, UMEME... ili uweze fanya tathimini ya uwezo wako kama upo chini au juu sanaaa na uanze kuweka mipango mikakati vyema ya kuweza kufanikisha ujenzi wa nyumba yako!
20210529_124307.jpg
 
[ Suala la professionalism bongo bado sana ndio maana hata mtaani watu wanalizwa mamillioni kisa uliona ni expensive kumpa mwanasheria laki mbili akuchekie ishu yako kisheria, au mtu anaamua kumeza tu madawa kisa anaona hospital ataongeza gharama...etc, We are still very far........

Kuna wengine wanamaliza kujenga alafu wanakuja humu kuomba jinsi ya kuziba ufa.

Nakuunga mkono, swala la utuliwaji wa wataalamu Tz bado ni shida sana.
 
Hadi za bure zipo, ramani siku hizi sio ishu labda usiwe mjanja au labda Kama unataka kujenga ghorofa! Ila kikawaida tu ramani sio ishu, nazungumza hivyo cause hata Mimi ramani sikununua...

Kkoo kuna mtu kamwaga chini anauza 20000 na makadilio yake kabisaa ya ujenzi
 
Back
Top Bottom