Je, TFF imeamua kuudanganya Umma kwa makusudi?

LENGISHO

Senior Member
Sep 15, 2017
169
245
Kwa hizi takwimu TFF Watueleze inamaanisha uwezo wa uwanja wa Mkapa ni mkubwa kuliko Estadio Camp Nou F.C. Barcelona ambayo inabeba mashabiki 99,354 au Rungrado May Day Stadium wa huko Korea ya kaskazini wenye uwezo wa kubeba mashabiki 150,000 au uwanja wa Wembley wa nchini Uingereza ambao unashika nafasi ya nane 8 Kwa ukubwa dunian kwa takwimbu za october 2020 yaani kwa Afrika imeupita hata Uwanja wa Soccer City unabeba washabiki 94,736?

Yaan Benjamin Mkapa National Stadium inabeba mashabiki 274,273 yaani Laki mbili elf sabini na Nne mia mbili sabini na tatu. Tafadhali TFF tuelezeni hizi takwimu wamezipataje?

NB: MKIWA WA TAALAMU WA KUPIKA TAKWIMU BASI MUWE MAKINI SANA

Reference





FB_IMG_1632324917580.jpg
 
Umekurupuka soma tena uelewe wanamaanisha mechi zote zilizochezwa mwaka 2020/21 vilivyoko chini ya bodi ya ligi ndiyo hao watu walioingia
 
Jamaa amejiona mjanja kumbe uwezo wake wa kuelewa ni mdogo mno.

Au sijui amepumbazwa na hisia za ushabiki.?
 
Umekurupuka soma tena uelewe wanamaanisha mechi zote zilizochezwa mwaka 2020/21 vilivyoko chini ya bodi ya ligi ndiyo hao watu walioingia
Iv msimu mzima kuna timu imeingiza mashabiki 65 tu kwenye uwanja wao ?
 
Mimi ngoja nicheke tu Buhahahahaaaaa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚
πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚
πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚
 
Back
Top Bottom