Je Tatizo La Ukeketaji Litamlizika Lini?

Mhache

JF-Expert Member
Jun 20, 2008
345
24
Nilipata bahati ya kutembelea Arusha na kujionea mji huo ulivyokucha kwa shughuli za kitalii. Pia nilielekea maeneo ya Kisongo eneo lililopo mbali kidogo na mji wa Arusha kama kilomita 30 hivi. Nilibahatika kuongea na vijana kadhaa. Niliwauliza kuhusu hali ya kukeketa wanawake katika eneo lao ipo je? Mmoja wao alikiri limepungua kwa kiasi kutokana na elimu wanayopatiwa.

Niliendelea kuwauliza ni kwa nini tatizo hilo haliishi. Walikiri ni kwa sababu ni mila na ni jadi ya watu wa eneo hilo. Wakati nikiendelea kuwahoji vijana hao alikuja dada mmoja kuungana nasi baada ya kusikia maongezi yetu. Nilimwuliza kama anajua suala la ukeketaji katika eneo hilo. Alikiri na kusema analijua na ni tatizo kubwa katika eneo hili. Kivipi? Kwa sababu usipokeketwa hutapata mume. Nani unataka asiolewe. Muda wa kuolewa ukipita unaanza kuitwa bibi. Na ni rahisi kujua fulani amekeketwa au la. Kwani hufanyika kwa uwazi na huambatana na sherehe kubwa ambayo ni ufahari kwao.

Inaonekana kwamba watu walio wengi wanajua matatizo yanayowapata wanawake waliokeketwa hasa wakati wa kujifungua na kutokupata raha wakati wa tendo la ndoa. Tatizo ni kukwepa aibu ya kutokupata waume. Alisema jibu ni wanaume kukubali kuoa mwanamke asiyekeketwa. Swali: Je kuna sababu nyingine zaidi ya hizo nilizozianisha hapo juu. Wana Jamiiforums naomba mchango wenu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom