Je tanzania tutafaidika vipi na soko la pamoja la eac? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je tanzania tutafaidika vipi na soko la pamoja la eac?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by anania, Jul 2, 2010.

 1. anania

  anania Member

  #1
  Jul 2, 2010
  Joined: Jul 2, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  NIMEULIZA HIVYO KWANI WATANZANIA WENYEWE TUKIENDA KUNUNUA VITU VYA KUTUMIA NYUMBANI TUNAULIZA VITU VYA KENYA.MFANO WA VITU HIVYO NI SABUNI PANADOL,SUFURIA YAANI VILE VITU VINAVYO TUMIKA KATIKA MAISHA YA KILA SIKU.NA ASILIMIA KUBWA YA WATANZANIA WAMEKUWA NA WASIWASI HATA WALE WENYEVIWANDA AMBAO SISI AKINA KAJAMBA NANI TULIFIKIRI WATACHEKELEA.jE NINI KIFANYIKE WAKUBWA?
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Jul 2, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu uko eneo gani la nchi hii ? Mimi niko moshi sasa hivi na kila ninachotumia kila siku nanunua toka viwanda vya Tanzania idadi hiyo imekuwa inaongezeka kila siku hata nilipokuwa Nairobi siku 3 zilizopita niliweza kupata mahitaji haya haya ninayoyataka kwa kununua bidhaa za Tanzania nikiwa kwenye nchi ile , kwasasa viwanda vyetu vinajitahidi sana na uchumi wetu unakuwa kwa kasi ya ajabu labda miaka 10 inayo Tanzania inaweza kuwa kinara kwenye soko la pamoja na afrika mashariki kama hali ikiendelea kuwa kama ilivyosasa hivi .

  Na kwa msisitizo unachoweza kufanywa kwa urahisi zaidi kwenye shuguli za soko hili ni mfano

  Wewe uko njombe unashona vikapo vile vikapo sasa vitaweza kuuzwa Kenya au Rwanda bila masharti na sheria zingine ambazo zilikuwa zinazuia bidhaa kama hizo toka nchi moja au nyingine kama huwezi kuuza wewe basi kuna vyama vya wafanya biashara vinavyonunua vikapo hivyo na kuvipeleka kwenye masoko mengine ya nchi jirani kama kungekuwa na tatizo kwenye jumuia kitu kama hicho ni ngumu kufanya hilo ni moja

  Lingine ni kwamba kuna baadhi ya vitu vitafanyika kutokana na sheria za nchi husika kama masuala ya ardhi na zingine zingine
   
 3. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  hatuna viwanda, sasa tuulizie biashara za kihindi? si bora vya majirani zetu?

  Kwa taarifa yako tunasupport viwanda vyetu vilivyopo sana. Viwanda vilivyopo ni vya:
  1- Vinywaji +sigara - Bia, soda, maji na sigara - watu wanakunywa bia na soda sana hata serikali inajua na ndiyo maana hata bajeti ya serikali inategemea eti kukuzia uchumi huko.
  2-kuchapa magazeti - Tz ina magazeti mengi pengine kuliko africa yote. Shigongo peke yake ana magazeti mengi kuliko idadi ya jozi za viatu ulivyonavyo.
  3-iceream na unga wa ngano na mahindi - nadhani ikiwa wewe ni mkazi wa dar unajua. kamuulize bahkresa
  4-vitenge na kanga - Nida, Karibu and Urafiki.
  5-Foma gold????????

  Pia ujue inawezekana wazalishaji wetu wanazalisha chini ya kiwango. Huwezi kumlazimisha mtu anunue kwa mfano Panado ya TZ ambayo inawezekana imechakatuliwa kiwalani au manzese wakati anataka apone na ili apone lazima apate dawa iliyo bora na iliyo bora anajua ni ya Kenya.

  NEED I SAY MORE?????
   
 4. Kottler Masoko

  Kottler Masoko Senior Member

  #4
  Jul 2, 2010
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 179
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  This is our challenge. there is no more a room for blur blur.
  We need to be serious on our makings, offerings and mindset.
   
 5. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280
  hakuna tutachofaidika nacho maana we produce even less than our local demands...ndio maana unakuta kuna bidhaa za kichina zimejaa hadi milangoni kwetu...sana watafaidika wachina kwa kutuuzia bidhaa zao na sie kuzipeleka rwanda kenya na burundi plus uganda...ile sie kama nchi hatutafaidika na hili soko la ea...

  sana naona mitafaruku ya kijamii ikiongezeka hasa maeneo ya mipakani kama hatutapata kundi la upinzani la kijeshi la banyamulenge watakaodai kuwa ngara na biharamulo ni nchi yao...kina kony wengine watakaodai kagera ni yao na kina kamau watakaodai moshi na namanga na serengeti ni yao SIJUI...ila mie NAMWACHIA MUNGU NA HAYA MAAMUZI MABOVU YA VIONGOZI WETU
   
 6. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wenye viwanda wanatoa sababu gani kuzalisha bidhaa chini ya viwango? kwa sasa hawana cha kusingizia kama hawataki kubadilika na kuzalisha bidhaa zenye viwango ni wao ndio watakaoathirika na sio wananchi.

  Isitoshe suala la umiliki wa viwanda linazidi kuwa tata maaana wenye viwanda wengi wala sio waBongo na ktk mazingira haya ya soko huru wenye viwanda wa nchi jirani wanaweza kuamua kuja kujenga viwanda vyao bongo ili kuwa karibu zaidi na soko.
   
 7. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  RED: Hongera... kama mtanzania mwenye uchungu na nchi yangu nimependa unachokifanya!!
   
 8. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #8
  Jul 2, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kuna tatizo hapa kwamba wengi wanaochangia mada hii sio waelewa wa masuala haya na bahati mbaya hawajawahi hata kuishi nchi jirani kujaribu kuona maisha na vitu kule vinaendaje kulinganisha na vyetu hata kidogo hili ni tatizo kubwa sio kweny nyie wachangiaji tu bali ni janga la kitaifa kuwa na wananchi mambumbumbu kazi kungoja propaganda na ngojera zingine zisizokuwa na msingi zinazofanya wananchi wanazidi kuwa waoga na kutotaka hata kujiendeleza zaidi hili ni tatiso sugu ndugu zangu .

  Tukiacha hayo hapo juu naamini serikali yetu haina watu wasiofikiria kwenye idara mbalimbali za utendaji hata inapoamua kuingia kwenye mashirikisho kama haya inakuwa imeshaona faida Fulani hata kama sio sasa hivi hata huko mbeleni sio lazima iwe miaka 2 au 4 ijayo hata 50 ijayo angalia nchi kama marekani zimejengwa kwa miaka mingapi mpaka sasa hivi tena kwa ushirikiano kati ya nchi zaidi ya 20 sasa kwanini hilo lishindikane hapa kwetu tena tunauelewano mkubwa kuliko walivyo wao siku zilizopita

  Jamani sasa hivi dunia inazidi kuwa kikiji kimoja kila nchi na jamii duniani inataka kujikomboa na kujenga ushirika na majirani zake ili kuleta maendeleo kwa watu wa maeneo hayo kwahiyo hata sisi ni sehemu za jamii hizo tunataka maendeleo lazima tuungane tumalize tofauti zetu tujenge nchi zetu kama ilivyo umoja wa ulaya , USA na muungano wa nchi sehemu mbalimbali duniani .
   
 9. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145

  Soko hili ni dawa mojawapo ya WAFANYAKAZI WAVIVU, MATAPELI na WAFANYABIASHARA waliobweteka... ushindani utaongezeka... muhimu:
  -Mzawa apewe kipaumbele kila tasnia iliyopo ndani ya makubaliano ya soko la pamoja
  -Mfumo wa elimu ya juu uboreshwe kutoa maingira bora ya ajira kwa wahitimu.
  - Serikali ipunguze zaidi ajira za umma na kuwalipa vema wale wataobakia waboreshewe maslahi(ili watu wajitume na mamwinyi watoke)
  -Iwekeze na iongeze wigo wa kukusanya mapato katika sekta binafsi(Mf. Viwanda, Utalii) na sekta zisizo rasmi.

  TANZANIA YENYE MAISHA NA UCHUMI IMARA INAWEZEKANA.
   
 10. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145


  Tanzania ina kizazi cha watu walioelimika, wasomi na wanaofikiri..Tunalemazwa na mfumo mbovu wa elimu amabo haumwandai mzawa kukabiliana na ushindani. Wachache wanaomudu ni kwa jitihada zao binafsi.
  -Tuache kubweteka tukisuburi fursa za maendeleo zitufate
  - tuache kulalamika na tufanye kazi
  -Serikali iheshimu taaaluma za waajiriwa wake na kuacha maamuzi ya kisiasa katika mambo ya msingi katika kujenga taifa hili!

  Nakubali kusahihishwa!
   
Loading...