Je, Tanzania tupo katika mdororo wa kiuchumi?

Prof Decentman

JF-Expert Member
Jul 14, 2013
276
140
Wadau salaam?

Natambua humu jamvini wapo wataalam wa uchumi wabobevu. Sisi wengine si wachumi japo yapo maeneo yetu ambayo tupo vizuri.

Nirudi kwa wataalam wa uchumi, je hichi tunachokipitia sasa ni nini? Ukiniuliza mimi binafsi naona wapo watu biashara wamefunga na wengi wanadai biashara ngumu.

Mikopo katika mabenki utoaji wake ni kama umepungua maana ukienda benki kutafuta mikopo si rahisi kama zamani.

Soko la Hisa DSE tunaambiwa mauzo yameshuka toka bil 33 hadi bil 3.

Makusanyo ya kodi nadhani ni muda hayajasikika yakitajwa (tu-assume yapo vizuri). Sasa haya yanatia shaka kama hali ni shwari.

Bajeti iliyopitika inaonyesha pesa nyingi haijatolewa kama ilivyopitishwa na bunge. Hii pia ni dalili kuwa kuna shida sehemu.

Sasa kwa wajuzi wa uchumi hii hali tunayopitia kitaalam inaitwaje na nini kifanyike tuwe sawa? Je zipo nchi nyingine duniani zimeshawahi pitia uzoefu wetu??
 
Uchumi unakuwa kwa kasi ya km 270/saa! Ndiyo maana Rais wetu mtukufu anapendwa zaidi na mataifa ya nje!
 
Back
Top Bottom