Alexander The Great
JF-Expert Member
- Aug 28, 2018
- 4,502
- 23,581
Habari ndugu wana Jamii Intelligence,
Katika kupitia pitia vitabu vyangu siku ya jana, nikapitia kitabu cha mwanafalsafa mmoja aitwae "Walt Whitman Rostow" (Rostow's Stages Of Economic Growth, 1960 - Hatua za ukuaji kiuchumi za Rostow).
Kwa wanavyuoni waliosomea maswala ya Uchumi, Sheria, Biashara (baadhi ya Course), na Public Administration Course mtakua mmempitia huyu bwana na wengine wengi tu.
Kilichonivutia zaidi kuandika thread hii, ni kutokana na taarifa/habari nzuri tunazopata hivi sasa kuhusiana na ukuaji wa uchumi katika nchi yetu Tanzania, nikasema niwaletee ili tujadili uwiano na uhalisia wa principles (kanuni) na stages (hatua) za wafalsafa na wanavyuoni wa uchumi.
Pia wanajografia (Geographers) jinsi wanavyoweka matabaka ya nchi kimaendeleo na uchumi, wakiyapa matabaka kama vile; Nchi zilizo endelea (Developed Countries), Nchi zilizo katika hatua ya kuendelea (Developing Countries), Nchi za dunia ya kwanza (First World Countries - Yani nchi zilizo endelea), Nchi za dunia ya tatu (Third World Countries - Nchi zisizoendelea).
Wanatuachia maswali magumu sana kujibu, nini maana ya kuendelea kwa nchi? Na kwanini nchi nyingine zimeendelea na nyingine hazija endelea? (Hapa tutabishana sana na kila mmoja atatoa jibu lake).
Nirudi katika hoja ya msingi,
NB: AFDB imeripoti ya kua Tanzania inaukuaji wa uchumi kwa asilimia 6.7% kwa mwaka 2018.
Tuangalie katika uhalisia wa uchumi Tanzania, pamoja na uwiano wa wanafalsafa wa uchumi. (Tukimuangalia bwana Rostow).
Bwana "Walt Whitman Rostow" ni miongoni mwa wanafalsafa bingwa wa uchumi, na ameandika mambo mengi kuhusiana na hatua za kukua kwa uchumi. Miongoni mwa hayo maandiko ni yale ya mwaka 1960, nlioandika hapo juu (Rostow's Stages Of Economic Growth).
Hatua za ukuaji wa uchumi katika nchi, alizotaja mwanafalsafa huyu ni 5, kama zifuatazo;
1) Jamii za kale/jadi (Traditional Society Stage).
Hii hatua inatafsiriwa uchumi wa kujikimu kwa kutegemea kilimo, uwindaji, ufugaji na ukusanyaji wa mambo muhimu kwa matumizi ya watu. Kazi ngumu sana na biashara (trade) kua katika hali ya chini. Watu kutokujali maswala ya teknolojia ya kidunia (limited technology). Hakuna utulivu wa wananchi na wala system ya kisiasa (No centralized nation or political systems).
NB Hapa ndio taifa linaanza hatua ya kwanza katika ukuaji kiuchumi na kuingia ya pili.
2) Sharti La Awali La Kuondoka (Precondition To Take Off Stage).
Mahitaji ya mali ghafi kwa kina, kilimo cha biashara kwajili ya mauzo ya nafaka nje ya nchi (agriculture for export purpose), utengenezaji wa bidhaa muhimu, ukuaji wa kibiashara na ubadilikaji wa mazingira ya kuishi, utambulishwaji wa kitaifa na vitambulisho, ukuaji wa teknolojia na uhamasishaji wa ufumbuzi wa kiteknolojia.
3) Kuondoka (Take Off Stage).
Bwana Rostow ameelezea kua hii hatua ni ya muda mfupi sana na ukuaji ni waharaka sana (short period intensive growth). Hapa watu hushawishika sana katika kuwekeza kwenye sekta ya viwanda kwa kasi, na mtazamo wao ni kwenye viwanda.
4) Uendeshaji kuelekea kwenye Ukomavu (Drive to Maturity Stage).
Hatua hii huchukua muda mrefu, watu hubadilika kutoka katika kuwekeza kwenye biashara zenye faida kubwa/biashara zilizo katika uhitaji wa hali ya juu (Investment Driven Profit Goods) na kuwekeza katika viwanda/biashara nyingi na tofauti tofauti. Uanzishaji wa biashara/viwanda ni wa haraka kwa watu. Shule, hospitali, vyuo na maswala muhimu ya kijamii sio tatizo tena.
5) Umri Wa Matumizi ya Hali Ya Juu (Age of Mass Consumption).
Hapa viwanda ndio vinashikilia uchumi wa nchi, na si wananchi wa kima cha chini kutegemewa kukamata uchumi/kodi ya nchi. Viwanda vya magari (automobiles) na matumizi ya magari ni muhimu kwa kila mtu, vifaa vya bei za juu kutengenezwa kwa urahisi na wingi (viwanda kama vya simu za mkononi, television n.k). Vijiji hugeuka miji na watu hukimbilia kwenye miji mikubwa.
Baada ya hatua hio, wananchi hujikuta wakiishi katika nchi yenye utulivu wa kiuchumi, amani, usalama wa biashara zao na uongozi bora. Na kutegemea uvumbuzi wa vifaa/mambo/viwanda/upelelezi wa kisayansi wa miaka ya mbeleni badala ya hapo waliopo. (Future Researches). - BEYOND CONSUMPTION.
Mwana falsafa huyu alielezea nia na madhumuni ya kuandika hizi hatua, ili kusaidia taifa kujua ni mambo gani yanapaswa kuzingatiwa na hatua zipi kuchukuliwa ili kushawishi ukuaji wa uchumi.
Mfano,
Nchi ya Singapore, ipo mashariki mwa bara la Asia, taifa hili lilipata uhuru mwaka 1965, na lilitumia njia hizi kujikwamua kutoka katika hali duni ya kiuchumi mpaka kukua kiuchumi kufikia hatua ya kua miongoni mwa mataifa yenye uchumi imara na mataifa yanayo chochea uchumi wa dunia. Sasa ni miongoni mwa mataifa yalioendelea ki miji mikubwa na yenye kipato kikubwa kwa mtu kushinda hata baadhi ya nchi za ulaya (Higher Per-Capita Income).
Kwa mtazamo wa sisi raia tunaoishi ndani ya taifa letu, tunafanya kazi, tunasoma kusoma, na kufanya biashara.
1) Je, tupo katika hatua gani sasa ya kiuchumi?
2) Je, Tanzania tunachukua hatua gani kukuza uchumi wa nchi yetu?
3) Na hizo hatua tuazochukua, zinachochea ukuaji wa uchumi kwa kasi kama tunavyotarajia na kuona katika report?
4) Vikwazo gani unahisi vinazuia ukuaji wa uchumi nchini? (Mfano labda kodi, sheria si rafiki kwa biashara na uanzishaji wa viwanda n.k).
5) Mahusiano ya Tanzania na mataifa ya nje, yana akisi ukuwaji wa uchumi kwa taifa letu?
6) Utawala wetu una mikakati na mipango gani kukuza uchumi kwa sera na utendaji uliopo?
Pamoja tujenge taifa letu,