Je, Tanzania tunatambulishwa kwa kipi? Nchi yangu inapoteza utambulisho

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Tanzania Yangu ya sasa imekosa alama yaani haina Identify kabisa. Je, ni nini alama ya Taifa letu kwa mgeni?

Kwa mfano mgeni akitoka Marekani, China, Hispania au Ufaransa je, atatambua vipi hapa amefika Tanzania?
Ukiingia China utakuta Maandishi ya kichina Kwenye Mabango, hivyo hivyo ukienda Korea utakuta Maandishi ya kikorea kwenye Mabango mbalimbali. Je, kwa Tanzania Identify yetu ni nini.

Leo hii ukiingia Tanzania utakuta Maandishi ya Kingereza kwenye Mabango mbalimbali na hapo utapata taabu kujua je, umeingia Wingereza au Tanzania maana Tanzania tumekosa Identify yetu Badala ya kutumia kiswahili kama Identify Tume badili na kutumia Kingereza kama Identify yetu.

Leo hii hata sanaa yetu Tumeitoloka Alama ya kitanzania na kuifuata alama ya nje Badala ya kuimba Nyimbo za Kigogo, kisukuma zenye mchanganyiko mbalimbali na majina kama Ngoma ya ukae, mdundiko, charanga, Wigashe na aina mbalimbali za melody mixture Singeli.

Hivi zaidi ya makabila 120 Wakitengeneza Melody tunawezaje kuiga Ngoma za South Afrika yaani Mapiano au ngoma za kongo, Nigeria na kwingineko.

Hata issue ya Mavazi leo hii ukivaa kiasili kama Masai na kuingia mjini utachekwa na watu walio valia suruali za kubana (model) kisa wao wanajiona Wameendelea na kusahau kuwa wanapoteza Identify yetu na mtu anapata Tabu kujua kama ameingia Tanzania au Wingereza.

Hakuna Mzungu anae jiita Ngh'wana Malunde ila leo sisi ndio tunajiita akina Da' Vinc Na hata majina mengine Yaani tunaita Watoto akina Thomas, Edison, Maulid, Johnson, Maximilian na majina mengine wakati hakuna wazungu wanao jiita akina Mazengo, Massawe, Mollel, Masanja, Mwakibete, Sanga, Mboya, Kisendi, Chacha, Mwita, Nyanyama, na majina mengine.

Tumesahau kuwa tunapoteza Identify yetu na hata tukiwa Mtaani watu watakushangaa endapo ukianza kuongeza Kimbululu, Kidendeule, kinyakyusa, kimanyema, kisafa, kipogoro, kibena au kizinza na eti utaonekana mnyamwezi kwa kuongezea kingereza, kifaransa au kichina lini ulienda Ufaransa ukawakuta wanaongea hata Kihaya?

Tanzania yetu tunashindwa kumsikiliza Mrisho mpoto tunamskiliza na kujivunia Jason Derulo, yaani hatumkubali Budagala, Saida karoli, na waimbaji wa asili tunakimbilia akina nikki Minaj, Beyonce, Akon na wengine.

Mitahara ya Elimu tunashindwa kuamini vitabu vya Nyambali Mariba Chacha Nyangwine na kuamini Machapisho ya Marekani ya watu wao kama Garland N.M, Dietsch.

Hatuamini hata vitabu vilivyo chapwa University of Dar es salaam press (UD Press), Mzumbe university na kuamini Machapisho ya Oxford ya Marekani, Longman ya Wingereza, Hill Book company ya Marekani, Cambridge university press na mengine.

Watanzania Tulipende Taifa letu Tulinde vya kwetu na hiyo ndio Tunu yetu.
 
Wamawia hatupo hivyo mkuu
Nchi zote kubwa kubwa duniani zinatambulishwa nguvu ya uchumi na kijeshi pamoja na teknolojia walizonazo siyo mambo lugha. Waambie viongozi wako wa nchi wakuze nchi kiuchumi, achana na sijui vazi la Taifa, lugha, ngoma za kienyeji, unyago.
 
Umelalama bila solutions
 
ID inayokuja kwa kasi ni Sukuma gang. Naomba mamlaka ziendelee kuidhibiti kabla haijaota mizizi.
 
Nchi zote kubwa kubwa duniani zinatambulishwa nguvu ya uchumi na kijeshi pamoja na teknolojia walizonazo siyo mambo lugha. Waambie viongozi wako wa nchi wakuze nchi kiuchumi, achana na sijui vazi la Taifa, lugha, ngoma za kienyeji, unyago.
Tutakuza uchumi kwa kutegemea nchi zingine yaani kwa mikopo tutegemee kukuza uchumi kweli.
 
Tanzania Yangu ya sasa imekosa alama yaani haina Identify kabisa. Je, ni nini alama ya Taifa letu kwa mgeni?

Kwa mfano mgeni akitoka Marekani, China, Hispania au Ufaransa je, atatambua vipi hapa amefika Tanzania?
Ukiingia China utakuta Maandishi ya kichina Kwenye Mabango, hivyo hivyo ukienda Korea utakuta Maandishi ya kikorea kwenye Mabango mbalimbali. Je, kwa Tanzania Identify yetu ni nini.

Leo hii ukiingia Tanzania utakuta Maandishi ya Kingereza kwenye Mabango mbalimbali na hapo utapata taabu kujua je, umeingia Wingereza au Tanzania maana Tanzania tumekosa Identify yetu Badala ya kutumia kiswahili kama Identify Tume badili na kutumia Kingereza kama Identify yetu.

Leo hii hata sanaa yetu Tumeitoloka Alama ya kitanzania na kuifuata alama ya nje Badala ya kuimba Nyimbo za Kigogo, kisukuma zenye mchanganyiko mbalimbali na majina kama Ngoma ya ukae, mdundiko, charanga, Wigashe na aina mbalimbali za melody mixture Singeli.

Hivi zaidi ya makabila 120 Wakitengeneza Melody tunawezaje kuiga Ngoma za South Afrika yaani Mapiano au ngoma za kongo, Nigeria na kwingineko.

Hata issue ya Mavazi leo hii ukivaa kiasili kama Masai na kuingia mjini utachekwa na watu walio valia suruali za kubana (model) kisa wao wanajiona Wameendelea na kusahau kuwa wanapoteza Identify yetu na mtu anapata Tabu kujua kama ameingia Tanzania au Wingereza.

Hakuna Mzungu anae jiita Ngh'wana Malunde ila leo sisi ndio tunajiita akina Da' Vinc Na hata majina mengine Yaani tunaita Watoto akina Thomas, Edison, Maulid, Johnson, Maximilian na majina mengine wakati hakuna wazungu wanao jiita akina Mazengo, Massawe, Mollel, Masanja, Mwakibete, Sanga, Mboya, Kisendi, Chacha, Mwita, Nyanyama, na majina mengine.

Tumesahau kuwa tunapoteza Identify yetu na hata tukiwa Mtaani watu watakushangaa endapo ukianza kuongeza Kimbululu, Kidendeule, kinyakyusa, kimanyema, kisafa, kipogoro, kibena au kizinza na eti utaonekana mnyamwezi kwa kuongezea kingereza, kifaransa au kichina lini ulienda Ufaransa ukawakuta wanaongea hata Kihaya?

Tanzania yetu tunashindwa kumsikiliza Mrisho mpoto tunamskiliza na kujivunia Jason Derulo, yaani hatumkubali Budagala, Saida karoli, na waimbaji wa asili tunakimbilia akina nikki Minaj, Beyonce, Akon na wengine.

Mitahara ya Elimu tunashindwa kuamini vitabu vya Nyambali Mariba Chacha Nyangwine na kuamini Machapisho ya Marekani ya watu wao kama Garland N.M, Dietsch.

Hatuamini hata vitabu vilivyo chapwa University of Dar es salaam press (UD Press), Mzumbe university na kuamini Machapisho ya Oxford ya Marekani, Longman ya Wingereza, Hill Book company ya Marekani, Cambridge university press na mengine.

Watanzania Tulipende Taifa letu Tulinde vya kwetu na hiyo ndio Tunu yetu.
Tanzania tunatambulishwa na vitu vingi, mbuga za wanyama,mlima Kilimanjaro, bendera ya taifa, pamoja na msanii Diamond Platnumz.
 
Diamondi Anae imba Mapiano? Tutawaambia Nini kwa mfano waitaly kuwa Diamondi Platnumz si Msouth Afrika tuwaaminishe kuwa mtanzania
 
Back
Top Bottom