Je, tanzania tunamkakati wa mkumiliki soko EAC?

UONGO MWIKO

Member
Aug 31, 2011
20
5
Habari wanajamvi!

Kuna mambo najaribu kutafakari sipati majibu hasa kwamba kama nchi tuna mkakati gani!
Mfano bidhaa tunazozalisha hapa nchini zina fursa gani katika soko la afrika mashariki?

1. Wakulima wa mazao mbalimbali wanayimwa fursa ya kuuza mazao yao mahali wanapopenda na kwa wakati waopenda (rejea sakata la kuzuia uuzaji wa mahindi nje ya nchi wakati soko la ndani halina bei nzuri). Kwa upande wangu naona hii haijakaa sawa kwani mkulima asipopata bei nzuri ataamua kutafuta biashara nyingine atakayoona inalipa (kumbuka lengo la kilimo ni pamoja na kujipatia kipato kizuri).

Kwa hiyo mtu anaweza kuamua kuachana na kilimo iwapo ataona hakilipi nakuanza umachinga wa vitu kutoka nje, sidhani nchi itanufaika kwa maamuzi hayo ya mtu huyo!

2. Wenye viwanda vya sukari kuzuiwa wasiuze kwenye nchi nyingine ikiwa ni pamoja na soko la EAC, najua nia ni kuhakikisha humu ndani panakua na sukari ya kutosha! lakini, je?

Serikali imewezesha vipi viwanda hivi kuzalisha sukari nyingi! hapa nashindwa kujua kwasababu kwenye zuio la kuuza mahindi nje ya nchi, moja ya sababu ilikuwa ni kuhakikisha mazao yanakuwa processed humu nchini ili kuongezewa thamani! utata ni kwamba, sukari inaqualify kuwa bidhaa iliyoongezewa thamani lakini ndio hivyo tena nayo inazuiwa isiuzwe!

Takwimu zinaonyesha kwamba mahitaji ni tani 500,000 kwa mwaka lakini viwanda vyote humu nchini kwa ujumla wake vinazalisha tani 300,000 kwahiyo kuna upungufu wa kama tani 200,000. Kwa haraka haraka unaweza kusema wanaozuia sukari isiuzwe nje ya nchi wako sahihi lakini utata unakuja unapojua kwamba ardhi ipo, nguvu kazi ipo, mitaji ipo (kumbuka viwanda ni asset tosha kuweza kupata mtaji kwenye vyombo vya fedha kama benki za biashara, n.k).

Suluhisho
1. Sera yetu ya kilimo na viwanda pamoja na sekta nyingine zinahitaji kufanyiwa mabadiliko ziendane na uhalisia wa mambo pamoja na mahitaji ya wakati tulionao.

3. Riba inayotozwa kwenye mikopo ipunguzwe, ili hivi wiwanda na wakulima wakopesheke!

2. Watoa maamuzi kwamaana ya viongozi wajiepushe na maamuzi yanayojichanganya! (rejea wito wa mara kwa mara kwa wakulima kwamba walime sana ili wapate ziada wauze na kujipatia kipato)!!!

Nawasilisha jamvini!!!!
 
Back
Top Bottom