Je tanzania tunakosa nini kati ya hivi?

Mkombozi

JF-Expert Member
Feb 19, 2008
806
426
Ili tuendelee tunahitaji Ardi, Watu, Uongozi bora na Siasa safi.Tanzania tunakosa kipi kati ya hivyo?Tujadili jamani,Je nini kifanyike?Miaka 50 ya uhuru,matatizo ndio yanazidi tufanyeje?
 
Tunakosa uongozi bora, inaelekea hivi sasa tunao bora viongozi. Mi ninavyofikiri kinachotakiwa kufanyika na ambacho kinaendana na wakati ni kwa wananchi kukataa hali ngumu inayosababishwa na hawa bora viongozi.
Kila mtu anahitaji kutimiza wajibu wake kwa usahihi wa hali ya juu, wazembe wasivumiliwe kwa namna yoyote; wanasiasa wafanye siasa kwa haki na wasiwaingilie wataalam. Bali wakubali kushauriwa na hao wataalam; pia vita ya rushwa iwe ni ya kumaanisha anayesema anapambana na rushwa aanze kujikana mwenyewe kabla ya kuleta mazingaombwe - kamata rushwa ya Shs 200,000 na samehe ya Shs 94 billion. Hii hata shetani hajawahi kuiwaza kabisa.
 
Kwa kuwa tatizo safi, na kwa kuwa viongozi hutokana na watu, basi tatizo ni watu. Ina maana quality ya watu ndo tatizo. Kwa hiyo tatizo ni watu.
 
Tunahitaji uadilifu. Tusichanganye siasa na technical matters concerning nation's prosperity. A lawywer can't in any way translate an ectrical drawing in any way, that's Ngeleleja
 
Ili tuendelee tunahitaji Ardi, Watu, Uongozi bora na Siasa safi.Tanzania tunakosa kipi kati ya hivyo?Tujadili jamani,Je nini kifanyike?Miaka 50 ya uhuru,matatizo ndio yanazidi tufanyeje?

Hayo maneno yalisemwa na Nyerere kwa kuyatowa kwa wanafalsafa zilizoshindwa. Bahati, nzuri au mbaya nae alishindwa kuyatimiza hayo na yote yapo.

Tanzania, tukitaka maendeleo tulete wasimamizi na wafanyakazi wa nchi zilizoendelea au zinazoendelea kwa kasi.

Kwetu, exposure iligubikwa na Nyerere kwa miaka karibia 30.

Mfano mdogo ni huu wa wawekezaji wanaopitia TIC wanaruhusiwa kuleta baadhi ya wafanyakazi kutoka nje ya Tanzania. Na maendeleo ni mazuri tu.

WaTanzania kama waTanzania na urasimu aliotuwachia Nyerere umetujaa vichwani na kila mtu uwajibikaji wake ni mdogo sana.

Kichwa kimoja cha nguvu kazi kutoka nje ya Tanzania kina uwezo wa kuzalisha mara 50 au zaidi ya Kichwa kimoja cha kiTanzania.

Huo ndio ukweli, tumegubikwa na wigu la wizi, mishemishe, uvivu, uongo, fitina, majungu na roho mbaya.

Tukiachana na hayo kwa kujifunza kwa hao tutaowaajiri kutoka nje, tutafanikiwa. Bila hilo, bure tu.

Hata Nyerere katibu muhtasi wake alikuwa kutoka Uingereza, kwa nini?
 
Back
Top Bottom