Je, Tanzania tunadhamiria kuwa na demokrasia ya kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Tanzania tunadhamiria kuwa na demokrasia ya kweli?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Edwin Mtei, Aug 15, 2012.

 1. E

  Edwin Mtei JF Gold Member

  #1
  Aug 15, 2012
  Joined: Dec 13, 2008
  Messages: 181
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Niliandika wiki chache zilizopita juu ya wasiwasi niliokuwa nao kama Watanzania, hususan Serikali na Chama tawala wanadhamiria kwa dhati kuwa na demokrasia ya kweli.

  Nilitoa mifano ya Wabunge wa Upinzani walivyokuwa wanaburuzwa Bungeni na kukemewa na Spika akisaidiwa na Mhe. Werema, Mwana Sheria Mkuu. Kwangu ilionekana kama uongozi wa Bunge hautambui kuwa Wapinzani nao pia wamechaguliwa na wananchi; na kwamba mchango wao unatoa changamoto kwa Serikali kuwa makini zaidi kiutekelezaji.

  Leo hii nimesoma katika magazeti jinsi Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Slaa, alivyonyimwa fursa ya kuhutubia na kufedheheshwa na kudhalilishwa huko Morogoro katika juhudi za kueneza sera na kuelimisha umma juu ya mabadiliko ya kuleta maendeleo endelevu. Polisi na viongozi wa wilaya wanaonekana kana kwamba hawatambui mabadiliko ya Katiba ya 1992 ya kuingiza vyama vingi vya siasa. Hili ni jambo la kusikitisha kweli.

  Ubaya zaidi ni kwamba jinsi Chama tawala kinavyoporomoka na wanachama wake kukikimbia na kuingia vyama vya upinzani, ndivyo hivyo viongozi wake mbumbumbu (naive) na wang'ang'anizi, wanaongeza kubuni mbinu katili wakishirikiana na Polisi hasa wilayani, kuwaburuza wapinzani na kuwasweka mbaroni.

  Nikiona jinsi wananchi wanavyofurika kwa wingi katika mikutano, kupata ujumbe wa mabadiliko ya kweli, napata faraja kwamba ushindi ni hakika.
   
 2. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 874
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 60
  Edwin Mtei

  Ndugu yangu bado mapambano ya demokrasia ni makubwa sana, hayawezi kurekebishika kwa muda mfupi kwa spika wa bunge kukubali serikali kuwajibika.

  Kuna mambo mengi yanayoweka rehani mabadiliko ya kidemokrasia kisheria kama madaraka makubwa ya raisi, matumizi mabaya ya vyombo vya dola kama kigezo cha usalama wa taifa, na intelijensia ya polisi kuzuia maandamano, mikutano, makongomano kwa kisingizio chakuhatarisha amani nk.

  Sheria ya wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya shighuli za kisiasa kuwawajibisha watendaji wa kisiasa ka kigezo cha kuwa ni walinzi wa usalama na amani.

  Kwa sasa ma-DC na ma-RC wanaweza kuzua mkutano wowote wa kisiasa kwa sababu zao.

  Uwajibikaji wa watendaji wabovu kama mhimili wa demokrasia imekuwa tatizo. Si suala la leo wala kesho demokrasia bongo bado safari ndefu sababu ya sheria zetu kupitishwa kiimla bila kuzingatia maslahi ya umma.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #3
  Aug 15, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Skikamoo mzee Mtei, kwa kifupi nakuombea kwa Mungu azidi kukupa uzima ushuhudie anguko kuu la joka kijani wa zamani
   
 4. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #4
  Aug 15, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Aiseee baba yangu hapa ngoja niseme ukweli kunabaadhi na si wote wa CCM wanafanya hii nchi ya kwao binafsi hasa kwa kutetea mambo ya kijinga...

  By the way huyo menaja wa TANESCO na huyo wa hiyo geaust watakuwa wageni wa nani Dr akiingia madarakani 2015?
   
 5. E

  Edwin Mtei JF Gold Member

  #5
  Aug 16, 2012
  Joined: Dec 13, 2008
  Messages: 181
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kuzuia wapinzani kufanya mikutano kwa kuagiza TANESCO wakate umeme, ni juhudi za kijinga. Sasa nashauri vijana wa Chadema wawe wakienda na stand-by jeneretas, hata katika sehemu zenye umeme unaotolewa na Tanesco.

  Pia ni jambo la kukithiri kwa umbumbumbu kujaribu kuzuia mikutano, eti kwa kumnyima kiongozi mhutubiaji chumba cha kulala, kama ilivyotokea huko Morogoro!! Vijana wetu ni wabunifu zaidi: Watakuwa wakisafiri na mahema kuanzia sasa. Hakuna kulala, Mpaka Kieleweke!!!!

  Nataka kuwaonya wanaozuia juhudi hizi za amani kwamba kwa kufanya hivi wanaandaa mazingira hatarishi, ambayo yanaweza kufanya nchi yetu iwe na makundi yasiyovumiliana.

  Narudia kuwa hii nchi ni yetu sote. Mungu Ibariki Tanzania!!!!
   
 6. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  kupelwa

  Umenena lakini lugha yako inaelekea ni ya mtu aliyekata tamaa huwezi kusema mwanamke hajapata ujauzito wakati mimba inaonekana ni ya miazi minane, tena madaktari wamemwambia abadili ratiba ya clinc kwa kuhudhuria kila wiki.

  Hapo utasema unawasiwasi kama ana ujauzito. Usitumie lugha ya kukatisha tamaa. Tumia maneno ya watu wa SOWETO SA SARAFINA, kwamba FREEDOM IS COMING TOMMORROW!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #7
  Aug 25, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 874
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 60
  mantiki ya hoja yangu si kukata tamaa, na wala si kwamba sioni dalili za kuelekea kwenye demokrasia , la hasha , bali napenda kukupa kisomo kama ifuatavyo:
  demokrasia inayo mihimili , ambayo nguzo zake ni kama ifuatavyo;uwajibikaji, haki ya kuchagua na kuchaguliwa,elimu sitahiki ya demokrasia, na haki ya kupata maendeleo.
  katika kutekeleza nguzo hizo , lazima tuwe na mifumo bayana, halisia, sitahiki, na tekelezi inayokubalika na umma yote kikatiba.Pia mifumo hii, ni vyema ikapata sheria na kanuni sahihi na bayana ili kukidhi matakwa ya umma kiutekelezaji.nachelea kusema , hapa bongo mifumo ni mibovu, sheria nyingi ni mbovu, kandamizi kutetea watawala ambao hoja na maudhui yao kulinda maslahi yao, kama ifutavyo;
  leo hii hatuna sheria nzuri ya uchaguzi , hivyo nguzo ya kuchagua na kuchaguliwa ipo kukidhi haja ya kikatiba na kisheria lakini uhalisia wake kiini macho.vyama vya upinzani vimekuwa vilipigia kelele muda mrefu kuwe na tume huru ya uchaguzi, lakini siku zote tume huwa kwa masilahi ya raisi aliyepo madarkani, hivyo kulinda masilahi ya ccm.Sheria ya uchaguzi na sheria matumizi ya fedha za uchaguzi pia ni kizungumkuti, zinajichzngznya kiasi mpaka leo ni kama itungwa itumike kama iini macho lakini utekelezwaji wake butu.sheria hiyo ya uchaguzi inatamka bayana kuwa raisi akishatangazwa na tume ,hatapingwa kwenye chombo chochote cha sheria, je kama atatangazwa raisi akiwa mwendawazimu itakuwaje?je haki ya kidemokrasia kupinga iko wapi?
  pia kwa leo niambie, ni wapi mbunge anaweza kuwajibika?hata kama alifanya madudu bungeni kama akina lusinde na wengine kulala na kusema imeafikiwa, hawezi kuwajibika asilani, sasa hapa hii nguzo ya uwajibikaji ipo wapi?mara ngapi tunaona wabunge wanakuwa wasemaji wa serikali hata kama si wasemaji ili kujipendekeza au kulinda masilahi ya ccm?mara ngapi tunaona bajeti mbovu zisizokidhi kiwango, lakini wabunge wengi waccm wanapitisha bila kujali masilahi ya umma?
  leo hii, lini ulisikia, si serikali wala tume ya uchaguzi imekuwa msitari wa mbele kuelimisha umma elimu ya uraia na demokrasia katika kiwango kikubwa?tunaona viNGO vya mijini na forum za mijini ndo huhangaika kupata visenti kuendesha visemina, vimakongamano, je vijijini wanaenda?leo hi,i kinapojitokeza chama cha upinzani kuendesha mikutano makongamano maandamano kwa ajili ya kuelimisha umma kuhusu uwajibikaji na elimu ya uraia, hupigwa vijembe, vita, kebehi na hilla nyingi hufanyika.
  si kweli kwamba nimekata tamaa kuhusu ustawi demokrasia hapa nchini, bali mazingira yameghubikwa na vizingiti isisitawi ili kuwezesha chama tawala kupata mtaji mkubwa kama kutakuwa na ubutu huu wa usitawi wa demokrasia.Juzi kule NGARA na karagwe kuna vijiji walililalamikia wahamiaji haramu kupewa maeneo ya kuchungia mifugo yao, mbona waliishia rumande?haya ndo mapungufu ya nguzo ya kidemokrasia kuwawajibisha watendaji.bado bongo safari ni ndefu kusitawisha demokrasia ya kweli
   
Loading...