Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,440
- 113,449
Wanabodi,
Yule Mwandishi Julian Asange wa WikiLeaks, ametiwa nguvuni nchini Uingereza kwa kutakiwa na Marekani, sasa sisi Tanzania, tujifunze kwa kitachompata, tukitumie kama shamba darasa la kujifanyia tathmini ya Press Freedom yetu, usikute sisi tuna press freedom kubwa kuliko UK na US, zaidi ya magazeti kufungiwa na vituo vya TV kutozwa faini, kwa hivi karibuni, ukiomuondoa Mkuu Maxence Melo wa jf, anayesubuliwa na kesi lukuki mahakamani, sijawahi kusikia Mwandishi mwingine yoyote wa habari wa habari wa Tanzania kukamatwa na kushitakiwa kwa alichoandika, ukiondoa enzi zile za Adam Mwaibabile "Mwana".
Japo Media za Tanzania tuna kilio kikubwa cha kulalamikia kuminywa kwa uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza, "freedom of the press" and "freedom of expression" , kiukweli ni sisi media wenyewe na waandishi wa habari, tunaoshindwa kuutumia kikamilifu uhuru tulionao, hivyo kupelekea wananchi wetu wanakosa haki ya kupata habari, "the right to information" mfano kuyajua mahela ya vote 20 ambayo kila Ripoti ya CAG ikiibuka, inaibuka nayo, na kila siku tunawaangalia waandishi wa nchi za wenzetu haswa UK na US jinsi walivyo sharp kuyaibua madudu na kuwaona kama wenzetu wako huru zaidi, sisi media zetu, nini kinatushinda?!.
Baada ya Asange kudakwa, Marekani inaitaka Uingereza iwakabidhi Asange ili wao ndio washughulike nae, somo kubwa la kujifunza hapa ni kufuatilia kwa makini, nini kitamkuta Asange, jee Uingereza itamkabidhi kwa Marekani washungulike nae au itamkingia kifua katika kulinda na kutetea uhuru wa habari?.
Kwa upande wa sisi media ya Tanzania, tunalalamika kuwa hatuko huru wakati waandishi wenyewe wa type ya Asange, wa kuibua ma vitu kama Stan Katabalo, hatuna!. Sisi wengi wa waandishi wetu, tunakalia kuandika habari za mikutano, warsha, seminar, na makongamano na kuzikunja zile naniliu za little brown ..., (naomba nisimalizie kwa heshima ya waandishi wenzangu), kazi yetu sasa ni badala ya kuandika habari za uchunguzi, investigative stories, sasa media zote, waandishi wote tunaishia kufanya reportage tuu, na sana sana kwa habari za kusifu, shangwe na kuomba mapambio ya kumsifu mfalme na vazi lake la ajabu!. We have totally no critical media in Tanzania, no news analysis, sisi media tumekwama wapi na kupigia kelele hatuna uhuru wa uhuru wa habari, wakati ni sisi wenyewe tunashindwa kutimiza wajibu wetu, huo uhuru tunaoutafuta ni uhuru gani?!..
Ripoti ya CAG imetoka ikiibua madudu kibao, ya matumizi mabaya ya fedha za umma, tungekuwa na serious media, by now, tungeishajua for sure ile 1.5B ilikwenda wapi na imefanyia nini!, au hata kujua tuu hizi fedha zinazochotwa kila siku hazina bila idhini ya Bunge na kutumbukizwa kwenye Vote 20, mule ndani ya vote 20, humo huwa zinakwenda kufanyia nini?!. Inamaana hiyo Vote 20, wao hawana mpango kazi, kila siku wanafanya kazi kwa zimamoto?!. Huu ni uthibitisho kuwa Tanzania hatuna any serious media ingeonyesha basi hata hayo majivu tuu ya huo moto, unaozimwa na fedha za zimamoto ndani ya vote 20, uliozimwa, ili kuthibitisha ni kweli kulikuwa na moto, isije kuwa ni mchwa tuu anatafunia hiyo Vote 20?.
Kama UK inayojitapa kwa Press Freedom sasa inamshikilia Asange, sisi kwetu kuna Mwandishi gani amewahi kushikiliwa kwa maandishi yake ukimuondoa Max wa JF?. Na tukiachana na kifo cha Daudi Mwangosi, na kupotea kwa Azory Gwanda na Ben Saanane wetu humu jf, jee kuna Mwandishi gani mwingine au media gani inaripoti investigative stories za kuhalalisha kutaka uhuru zaidi?.
Somo la kukamatwa kwa Asange kutupe funzo usikute sisi Tanzania tuna press freedom kubwa kuliko ya UK na US ila tumekosa media na waandishi mahiri wenye na ability, capacity and capability ya kuitumia hii freedom iliyopo kikamilifu, na kuisaidia jamii!. Nikisema media ya Tanzania ni hopeless media, nitakuwa niwaonea?.
Jumamosi Njema
Paskali

Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari mjini Morogoro, JamiiForums ndani ya Nyumba
Wanabodi, Mei 3 kila mwaka, ni siku ya kimataifa ya kusherehea siku ya Uhuru wa Habari, Media Freedom Day, ambapo hapa nchini, kitaifa siku hii inasherehekewa kwa muda wa siku 2, mjini Morogoro toka katika hoteli ya Nashera ambapo Jamiiforums pia inashiriki, na tayari nimeishamuona Mkuu Max...
www.jamiiforums.com
Serious Media inaweza kuwabaini "wasiojulikana" Deo Masakilija
Wanabodi, Naangalia kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari kinachorushwa na Star TV, ambapo mwandishi Mkongwe, Deo Masakilija, amealikwa. Dotto Bulendu ameanza kwa hoja 'Je media imetimiza wajibu wake ipasavyo katika kuwabaini hawa watu wasiojulikana wanaohusika na matukio ya utekaji, utesaji...
www.jamiiforums.com
Media kuikosoa Serikali: Je, Tanzania tuna Strong Media au Strong Journalists wenye Uwezo huo?
Wanabodi, Declaration of Interest: mwanzisha mada ni mwandishi wa habari mstaafu ambaye amehudumu kwenye tasnia hii as active media kwa zaidi ya miaka 27, hivi sasa ni mstaafu akiendelea kuhudumu as passive media kama mwandishi/mtangazaji was kujitemea kupitia kampuni ya PPR. Serikali zote...
www.jamiiforums.com
Uhuru wa Habari Tanzania: Je, Vyombo Viko Huru? Je, Waandishi wa Habari wako huru? Wanathaminiwa?.
Wanabodi Leo ni Siku ya Kimataifa ya kuadhimisha Uhuru wa Habari. Kwa Tanzania, maadhimisho rasmi yanafanyikia jijini Mwanza, katika kuadhimisha siku hii kwa Tanzania tunaadhimisha nini haswa?. Wakati tukiadhimisha hicho tunachoadhimisha, hakuna ubaya tukitafakari baadhi maswali haya... 1.Jee...
www.jamiiforums.com
Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa
Mkuu The Boss, bahasha ni dunia nzima mpaka Ikulu inatembeza bahasha, hiyo PCCB yenyewe na mpaka Polisi wanatembeza bahasha halali kama wanavyotembezewa!. dunia nzima kivipi? waandishi wa kenya wanapokea bahasha? marekani? uingereza? south africa?????
www.jamiiforums.com