Je, Tanzania tumepoteza nafasi ya kuwa " Wapatanishi" wa nchi zenye migogoro barani Afrika?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,558
Waziri wa Marekani yuko ziarani Kenya kuongea na mpatanishi wa mgogoro wa Tigray na Ethiopia Rais Uhuru Kenyatta.

Waziri huyo aliyetumwa na Rais Biden wa Marekani amesema atakwenda pia Nigeria na Senegal anakoamini wana ushawishi mkubwa katika siasa za Afrika

Ndio najiuliza Tanzania tumesahaulika?

Wakumbuke kuwa tulisaidia sana ukombozi wa bara la Afrika.
 
Tanzania na Ethiopia wapi na wapi?

Sisi ni Huku SADC na hapa East Africa.
 
Hayo ya Ethiopia na Somalia is THEIR problem sisi hayatuhusu na wasije kabisa.
 
Taifa limebaki na wasanii na wapigaji tu, habari ya kupatanisha ilishawashinda siku nyingi wakaamua kuwapa watu kesi za uongo.
 
Jikumbushe tambo za aliyekuwa waziri wa nje John Aidan Kabudi na 'kujifungia"ndani kwa Mwendazake kulivyouwa ushawishi wetu.
 
Hata mgogoro wa Msumbiji ilibidi Rwanda iruke juu ya Tanzania kwenda kuokoa jahazi.
Tanzania tumebaki kupambana na magaidi wa ndani wa shilingi laki 6.
Ama kweli hii ndo Tanzania yetu.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom