Je, Tanzania tuko kwenye vita na nani?

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,605
8,744
Hivi karibuni tumekuwa tukielezwa hasa na wanasiasa kwamba nchi yetu iko kwenye vita ya uchumi na mabeberu. Lakini wananchi wetu tunahitaji tuelezwe tuko kwenye vita na nani na mabeberu ni wakina nani hasa. Maana beberu ni dume la mbuzi.

Je, ni ubeberu wa miaka ya 1970's wakati wa vita ya ujamaa na ubepari ambayo vita hiyo imeshaisha? au ni kitu tofauti.

Je, ni vita na wawekezaji wetu wenyewe ambao sisi wenyewe ndiyo tumeingia mikaba hiyo kwenye mafuta na madini miaka ya 1990's.

Je, kuna sehemu ya Tanzania imechukuliwa hatujui?. Je ni mfumo wa bank ambao sasa bank zetu zinakufa kwa wafanyabiashara kupeleka pesa nje wakikimbia kodi na sheria mpya?

Watanzania tunaomba maelezo ya msingi ili wazalendo tuweze kusaidia kwenye vita. Au tujue moja hakuna vita ni siasa pekee.

Mimi ni mtaalamu wa Finance na kwa mawazo yangu kama ni kutangaza vita ni vita ya kusaidia vijana wetu na Serikali inatakiwa kuona haya kama ni vita na sio hao mabeberu ambao wengi wetu hatuwajui. Mimi kama Mtanzania naona vita kubwa ni kwenye haya hapa

1. Tanzania tuna vijana asilimia 66% chini ya miaka 24. Je tumewaandaa vipi hawa vijana kwenye dunia mpya ya uwazi, ushindani

2. Umeme je tufanya vitu tuwe na umeme wa kutosha na uhakika. Umeme ni suluhisho ya matatizo mengi kama maji, viwanda etc. Umeme nafuu

3. Mfumo wa bank> Kwenye mfumo huu wa dunia tufanyaje tuweze kuwa na banks ambazo zinachangia na kusaidia ajira kwa kusaidia biashara ndogo ndogo hasa vijijini.

4. Land tutabadilisha vipi mfumo wetu uendani na mfumo wa uchumi bila kuleta matatizo kwenye jamii. Mfumo wa mtaji unahitaji mfumo mzuri wa land

5. Je tutatumia vipi technologia kwa maendeleo mfano siku hizi watoto wanapewa simu zenye data pekee na wanaweza kusoma vitabu bure popole duniani. Je tunatumia vipi technologia kuweza kushindana hasa kwa vizazi vijavyo.

6. Tutapunguza vipi siasa kwenye shughuli za maendeleo mfano je ni kwanini hatutafuti mfumo kutoka consulting companies ambao unaongeza ufanisi na kupunguza gharama kwenye serikali. Kwanini sijawahi kusikia kampuni imepewa tender ya kuchunguza ufanisi wa serikali na idara zake kama kwenye kampuni za binafsi. Hatuna utaratibu wa ufanisi kila kiongozi anaendesha sehemu yake kwa kibinafsi zaidi badala ya kufuata blue print. Sera za kisiasa ni tofauti na utendaji mfano kama unataka uongeze uwezo wa watoto kielimu ukiacha madara je kuna mbinu gani mpya za kifanisi zinafanyika kufanikisha hilo.

7. Afya Je tuna ubunifu gani mpya kwenye Afya. Mimi nipo kwenye kampuni za Afya nashangaa mfano kwanini Tanzania, Kenya , Uganda na Rwanda wasikae pamoja wakatengeza group kama MSD lakini iwe ya nchi zote na wakaenda kununua vifaa vya hospitali, dawa, na hata wakachangia madaktari na wataalamu matatizo ya Afya hayana mipaka malaria, kisukari, pressure ni ile ile Kenya, Tanzania, Uganda na Rwanda. Lakini kikubwa group hii itasaidia kupunguza gharama za ununuzi kwasababu wataenda kununua vitu kama mtega mmoja.

8. Je, nchi yetu itapunguza vipi siasa bila kuleta matatizo mfano mdogo tu tumeambiwa sasa ni kazi tu lakini kwenye mitandao hapa ni lissu tu. sasa tujiulize siasa zimepungua au kuongezeka..... na tukiendelea hivi kuna mtu mwenye akili zake anafikiri zitapungua kwa mwenendo huu!!.

Serikali hajapata dawa ya kupunguza siasa bado. Serikali ichukuwe mfano wa Botswana chama kimoja kimetawala muda lakini sio kwa kupigana wa upinzani ni kwa kuleta maendeleo. Ukileta maendeleo hautahitaji kuongea kila siku unachofanya maana wananchi wataona wenyewe. Lakini serikali yetu ni kama inalazimisha watu

Tujiulize maswali haya
1. Je kwanini Nyerere alishidwa kuleta mfumo wa China Tanzania.
2. Kwanini Nyerere alifikiri vyama vingi ni vizuri kwa nchi yetu
3. Kwanini Nyerere alifikiri umoja wa nchi kama EAC ni mzuri
4. Kwanini Nyerere alifikiri kubadilisha viongozi ni kitu kizuri

Ukiangalia vizuri alijua huwezi kubadilisha utamaduni wa Tanzania ukawa wa China au Rwanda. Watanzania hawana utamaduni wa namna moja, hatuna dini moja, hatuna kabila moja au mbili na tuna nchi kubwa sana. Hivyo maendeo ya nchi yatatokana na utotauti na utamaduni tofauti tofauti tulionao na hautafanikiwa kama utawaambia watanzania wasiongee, wasibishe au kutishia kuwafunga.

Pascal Mayalla , Mwanakiji mtiifu waandishi wa habari chukueni maswali hapo kwa viongozi wetu
 
Bashite na babake wanasemaga tupo kwenye vita ya kiuchumi, binafsi sijui huo uchumi ni upi. Subiri nifunge mdomo maana hawachelewi kuagiza waletewe mkojo wangu. Sina mkojo wa mchezo mchezo Mimi!
 
1550673273761.png

Mfano hii kampuni wamewekeza Tanzania wamesema watatoa $300M , wanaongea na kufurahia na Raisi wetu. Je hawa ndiyo mabeberu? Je hii ndiyo vita wanasiasa wanayoongea. Je mikataba mibaya ambayo sisi wenyewe tumeingia ni tatizo la mwekezaji au ni tatizo letu?. Leo ukienda kununua galoni la mchele kwa shilingi elfu mbili halafu muuzaji akasema nitakupa mawili kwa elfu mbili mia tano je hapo umemnyanyasa muuzaji? au ni biashara.
 
Tuko kwenye vita ya kujikomboa kiuchumi toka kwenye kakocha ya mabeberu na vibaraka wao wanaotutundulisu (wanaotusaliti) kwa manufaa yao binafsi ya kisiasa na kuchumia matumbo yao. Hakika tutashinda vita hiyo.
 
..vita ya kiuchumi tumeua maadui wangapi?
..na diplomasia ya uchumi iliishia wapi?
Haya maneno hayaeleweki, ni kauli mbiu tu.

Tanzania haiwezi kuingia katika vita ya uchumi na mabeberu hata siku moja

Mfumo wetu wa uchumi hauna impact katika dunia, vita inatoka wapi?

Mabeberu wakitaka kupigana vita hiyo itachukua miezi 3 tunakwisha.

Mfumo wetu wa fedha, uuzaji, uagizaji n.k unategemea mifumo ya magharibi.
Wao wameshika mpini sisi makali

Mdororo wa uchumi uliotokea miaka michache ulionyesha nafasi yetu katika uchumi wa dunia
Hatukuathirika kwasababu ile 'network na intertwining' ya uchumi wa dunia sisi hatukuwepo

Kilichotokea ni sisi kupokea madhara ya mdororo bila kushiriki kutengeneza au kuharibu.

Ukitazama Bretton wood institute utaelewa kwanini hatuwezi vita hiyo

Pengine vita ya rushwa ingekuwa kauli muafaka. Hao wanaoitwa mabeberu wamekaribishwa, wameandikiwa mikataba na wamepewa fursa na wazawa kwa gharama za rushwa

Hivi tumesahau ule mktaba uliondikwa kwa mama Ntilie kule London na waziri wetu?

Diplomasia ya uchumi imefeli kwasababu haina maandalizi na haiungwi mkono kikamilifu

Kama ''tumejitoa'' kushiriki mikutano nani anatuchukulia serious?

Ukitaka kumjua adui yako kaa naye karibu, sasa Davos hatuendi, G20 tumesahaulika, SADChoi n.k. katika mazingira hayo tunaendelezaje diplomasia ya uchumi?
 
Watanzania hatuna vita (ya uchumi au nyingineyo) na mtu yeyote mpaka sasa. Vita iliyopo ni ya rais na chama chake dhidi ya demokrasia na vyama vya upinzani. Hayo mengine siyo vita, ni sarakasi za kujikosha baada ya CCM na vibaraka wake kulikoroga kwa kuuza kila rasilimali ya nchi kwa njia za kifisadi. Kama kweli wanapigana vita mbona hatuoni utaifishaji wa rasilimali zetu kama alivyofanya Hugo Chavez alipoamua kupigana vita ya uchumi dhhidi ya US?

Kwa hakika kabisa, kinachoendelea ni usanii tu, hakutakuwa na long term impact kwenye hii iliyoitwa "vita ya uchumi" zaidi ya kuiumiza zaidi nchi na wananchi kwa kujaribu kuwasumbua watu tuliowauzia rasilimali zote za nchi kwa ridhaa ya CCM.
 
Back
Top Bottom