Je, Tanzania sio salama? Hizi bunduki za nini?

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,934
3,805
Wakuu nauliza enzi zile zetu tukijipanga na kumpokea raisi tokea aiport hadi anapofikia hatukuona haya ya leo Rais anapokwenda huwaga na mambo ya kutisha .

Sina haja ya kuwachosha sana lakini tupeni ufafanuzi Je Tanzania sio salama tena,hata hatukuyaona wakati wa Nyerere,Ali Hassan,Mkapa wala Kikwete ,Yalianza wakati wa Magu na sasa yanaendelea.

Kusema kweli haipendezi, Raisi Samia ondoa hivi vitu Mwenyezi Mungu yupo na anakulinda .

1637394187493.png
 
Raisi amezuru Uganda Kenya Misri hatujaona vituko kama vyetu hapa, Je wanashindwa kuwa na mbinu ya kuficha au kuweka nyuma ya pazia vitu hivi ?
Labda mpaka viwadhuru wenyewe. Yule aliyeondoka alikuwa na maadui kibao chamani, huyu sijui adui yake nani!? Au wale jamaa wanaoshitakiwa kwa ugaidi kule gerezani!?
 
wakuu nauliza enzi zile zetu tukijipanga na kumpokea raisi tokea aiport hadi anapofikia hatukuona haya ya leo Raisi anapokwenda huwaga na mambo ya kutisha . Sina haja ya kuwachosha sana lakini tupeni ufafanuzi Je Tanzania sio salama tena,hata hatukuyaona wakati wa Nyerere,Ali Hassan,Mkapa wala Kikwete ,Yalianza wakati wa Magu na sasa yanaendelea.
Kusema kweli haipendezi, Raisi Samia ondoa hivi vitu Mwenyezi Mungu yupo na anakulinda .

View attachment 2017194
Wanajua kuwa wanayo yatenda kwa wananchi hayafai hata kidogo.
 
Labda mpaka viwadhuru wenyewe. Yule aliyeondoka alikuwa na maadui kibao chamani, huyu sijui adui yake nani!? Au wale jamaa wanaoshitakiwa kwa ugaidi kule gerezani!?
Labda kwa kuogopa huo ugaidi ndiyo maana wanatumia ulinzi wa hali ya juu kujilinda.

Kuna siku nilikuwa kibiti nikaona msafara wa huyo mama hadi nikaingiwa na hofu kuu.

Chini magari kibao juu angani madege makubwa kama tupo uwanja wa mapambano.
 
Raisi amezuru Uganda Kenya Misri hatujaona vituko kama vyetu hapa, Je wanashindwa kuwa na mbinu ya kuficha au kuweka nyuma ya pazia vitu hivi ?
Wanafanya makusudi ili nchi yetu ionekane kuwa tupo vizuri kwenye nyanja za kujilinda.
 
Labda mpaka viwadhuru wenyewe. Yule aliyeondoka alikuwa na maadui kibao chamani, huyu sijui adui yake nani!? Au wale jamaa wanaoshitakiwa kwa ugaidi kule gerezani!?
Atakuwa anawajua ndo maana anajikinga
 
Hua kuna silaha zinahesabiwa ni standard issue kwa kila idara. Mfano labda utaambiwa SMG ni standard issue kwa mlinzi wa getini wa waziri mkuu.

Au ukakuta katika presidential convoy standard issue weapon ni AR 15. Over time kutokana na teknolojia, threat level standard issue hua updated pengine ilikua updated tangu enzi za Marehemu Magufuli.

Hivyo inatakiwa tuzizoee tu wao ndiyo wanajua kwanini wanazunguka na mijegeja ya hivyo.
 
Kila zama na kitabu chake,misamiati kama Bwanyenye,Kupe,Mirija haipo tena.

Muda unafikiri uko salama ndiyo huwa wa hatari zaidi.

Rais mstaafu Mwinyi alipozabwa makofi kwenye Baraza la Idd 2009 watu walihoji kazi ya mlinzi wake.

Vichaa wengi mno zama hizi so si Rais tu,hupaswi kutembea kama loose cargo kwenye warehouse za Silent Ocean.
 
wakuu nauliza enzi zile zetu tukijipanga na kumpokea raisi tokea aiport hadi anapofikia hatukuona haya ya leo Raisi anapokwenda huwaga na mambo ya kutisha . Sina haja ya kuwachosha sana lakini tupeni ufafanuzi Je Tanzania sio salama tena,hata hatukuyaona wakati wa Nyerere,Ali Hassan,Mkapa wala Kikwete ,Yalianza wakati wa Magu na sasa yanaendelea.
Kusema kweli haipendezi, Raisi Samia ondoa hivi vitu Mwenyezi Mungu yupo na anakulinda .

View attachment 2017194
Haini kajiongezea urinzi ...aka most wanted
 
Ni ushamba au ni kitu gani,kwani intelijensia katika misafara ya raisi ina faida gani,J.F.Kennedy kilichomkuta kinajulikana ,so uovu hauwezi kuzuiliwa kwa kuwekwa ulinzi wa zana nzito wazi kama tunavyozoezeshwa,ambazo zingeweza kuhifadhiwa nyuma ya pazia.Au walinzi husika wabeba zana hizo kuvaa yale makoti makubwa ya kiulinzi.
Canal Gadafi yeye alikuwa na walinzi zaidi ya mia moja,escort yake si ya kawaida ,hao ni watu wenye migogoro au migongano ya Kimataifa ,Tz tuna ugonvi na mtu ? failure ya kumlinda raisi haitokani na kutoonyesha silaha nzito ni jinsi gani mnajipanga kumlinda na sio kuzuia kitu gani kisimfike hilo ni gumu.
 
Dhana ya kulinda viongozi hasa Rais ni lazima kwani kuna hatari za kiusalama zinaweza kutokea wakati wowote.. Hivyo lazima walinzi wachukue tahadhari.
Sweden walikuwa na mfumo wa kutowapa ulinzi wa kutosha viongozi wao wajuu hali hiyo ilibadilika alipouwawa Waziri wao mkuu Olof Palme akitoka Cinema.
Hao hao wanaolalamikia ulinzi wanaathirika vipi kwa Mkuu wa Nchi kupewa Ulinzi?Au ulinzi umeanza na Rais Samia mpaka iwe nongwa?
 
Back
Top Bottom