Je Tanzania kuwa na hatma kama ya Haiti? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Tanzania kuwa na hatma kama ya Haiti?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Keynez, Jul 4, 2012.

 1. Keynez

  Keynez JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 640
  Likes Received: 297
  Trophy Points: 80  JokaKuu,

  Nimeichukua hiyo post ya Mkandara kwa sababu kwa kiasi kikubwa inashabihiana na uelewa wangu wa mambo haya dunia yanavyokwenda. Nilikuwa nahangaika kidogo juzi kuweka mawazo yangu sawa lakini hii post yake itanisaidia sana kuweza kujieleza kwa ufasaha kwa sababu naamini kabisa alichosema ni kweli, ingawa sina uhakika kama atakubaliana na mimi kwa nitakachosema. Itabidi nimsukumie hii post yangu ili nione anafikiria nini.


  Kwa kuanzia ningependa kusema kwamba katika dunia ya sasa kuna pande mbili zinazopingana. Naamini wote mnajua hilo, ingawa wengi wanafikiri haya mambo yamekwisha toka miaka ya 80. Hii ni rahisi kujua, si tu kwa kuangalia siasa ya dunia inavyoendeshwa sasa, lakini hata uchumi.

  Naamini wewe uelewa wako ni mpana zaidi kuliko baadhi ya watu, wengine ninaowaona humu, wanaodhani JK kauza nchi kwa t-shirts za kampeni na masuti. Ningependa kuamini hivyo la sivyo hii post yangu itakuwa kupoteza muda.

  Nikiendelea, vita ya sasa kwa kiasi kikubwa ni muendelezo wa vita za miaka ya 60-70, tofauti kubwa ni kwamba China siyo tena nchi masikini, Afrika tuna kete zenye nguvu zaidi ya wakati ule ingawa wanajaribu kutupuuza kwa sababu tunafanya mlinganyo wa mbinu (strategic equation) za magharibi kuwa mgumu sana kwao, na kwamba siasa za ndani ya Marekani zinatumika kwa kiasi kikubwa katika mchezo huu mpana.

  Kingine, ni kwamba siasa, uchumi na mambo mengine NJE ya marekani vinashawishi kwa kiasi kikubwa tabia, fikra na maamuzi ya wapiga kura wa marekani kwa sasa kuliko wakati mwingine wowote (nitalielezea hili kwa upana baadaye).

  Nimewahi kukaa chini na kuzungumza na watu kadhaa wenye upeo tofauti kuhusu haya mambo. Zamani tulikuwa tunaishia kwenye malumbano na sababu kubwa ni kwamba 'mentality' ya watunga sera, hasa kuhusu mambo ya nje ni tofauti kabisa na, tuseme, watunga sheria, ukiacha hata watu wa kawaida.

  Kujua sheria kwa kiasi kikubwa kunasaidia kuwa mtunga sera mzuri wa mambo ya nje kwa sababu unajifunza jinsi ya kuzivunja hizo sheria baadaye, na kwa kisi kikubwa hiyo ndiyo inakuwa kazi yako. Kwa kifupi, hivyo ndivyo sera ya mambo ya nje ya marekani inavyoendeshwa, na China inaelekea imenakili na kufanisi mbinu hiyo.

  China haitumii mbinu hiyo kwenye mahusiano yao na nchi zinazoendelea (Africa, Caribbean, Latin America), na hata kwa majirani zake kwa sababu lengo lao ni moja. Kwa kifupi, nchi rafiki hazitumii mlengo huo baina yao. Kwa kusema hivyo, bila kuwepo kwa uhasama wa waziwazi, watu wanaweza kuangalia mambo madogo madogo (watalii, viongozi kutembeleana, misaada mbalimbali na hata mawasiliano kati ya jeshi na jeshi) katika uhusiano baina ya nchi mbili zilizo na ushindani wa siri na kudhani zina uhusiano mzuri.

  Nchi zilizoweza kujenga mihimili ya sera zao sawasawa zina uwezo wa kuendesha sera 2-3 tofauti zisizoshabihiana kwa wakati mmoja bila sera hizo kugongana. Ndiyo maana naamini miaka ile walipotuchukua watumwa, na baadaye kujigawanyia Afrika, kwa kiasi kikubwa wananchi wa ndani wa nchi zile walikuwa hawajui military adventurism (zizimizi za kijeshi??) nchi zao zinazofanya nje ya nchi. Hata leo hii, mbinu hizo bado zinawezekana na zinaendelea, ingawa inakuwa ngumu sana kuzitekeleza kwa sababu ya vitu kama mtandao.

  Kama umesoma hadi hapa, unaweza kuwa unajiuliza, haya yote ninayoongelea yanahusiana vipi na meli za mafuta za Iran kubeba bendera ya TZ. Naomba niendelee (niwie radhi, itanichukua posts kadhaa kuweza kuelezea yote ninayotaka kusema)........
   
 2. Keynez

  Keynez JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 640
  Likes Received: 297
  Trophy Points: 80
  Mbinu za vita za Mnyonge :


  Mimi ni mfuasi mkubwa wa Mwalimu Nyerere. Mwalimu alitumia muda wake mwingi katika miaka 20 ya mwisho ya uhai wake kusukuma wazo la 'Kusini-Kusini' na kwa wakati huohuo akisukuma wazo la 'Angalia Mashariki'. Nimewahi kusoma mahali fulani kwamba, Nyerere alitembelea China mara nyingi baada ya kustaafu kuliko wakati alipokuwa madarakani.

  Kuja kwa makundi kama BRICS, Shanghai Cooperation, Mercosur na mengine, ikiwemo makundi ndani ya afrika ni zao la moja kwa moja la jitihada hizo. Kufanikisha lengo hilo la 'Kusini-Kusini' na 'Angalia Mashariki', nchi changa zililazimika kujenga mbinu mpya zitakazowawezesha kufikia malengo hayo ukizingatia upinzani mkali waliokuwa wanategemea kutoka nchi tajiri.

  Wakati huo huo, hizi nchi hazikutaka, na labda zisingeweza hata zingetaka, kukata kabisa mahusiano ya kiuchumi baina yao na nchi za magharibi, sababu kuu ikiwa kuwepo kwa ndugu zetu kwenye nchi hizo, hapa nikiwa naongelea wale waliotoka kwenye koo za kitumwa.

  Sababu hiyo, siyo tu ilipanua wigo la mbinu hizo kuweza kufanya kazi, lakini pia wakati huo huo ili-'complicate' mambo kwa pande zote mbili. Huu ni mjadala mrefu ambao naweza kuja kuuelezea siku za mbele, lakini niliwahi kuanzisha makala hapa miaka ya nyuma niliyoiita 'Deeper than Rap' nikigusia hili suala.

  Bwana Mkandara katika post yake niliyoinukuhu aligusia hii mbinu ninayoiongelea, inawezekana bila kujua kwamba anachoongelea ni mbinu ambayo nchi, au kundi la nchi linaweza kuitumia kufikia malengo yake. Wengi mnaweza msiamini nchi inaweza kufanya uovu kama huo aua hata viongozi wetu wanaoitwa dhaifu wanaweza kujenga mbinu inayohitaji uelewa wa hali ya juu. Kuelewa hii mbinu, ni muhimu kubadilisha jinsi unavyojenga fikra zako katika maisha yako ya kila siku.

  Kuna kitu kwenye mbinu za kivita kinaitwa 'Asymmetric Warfare' (nimekosa tafsiri ya kiswahili). Hii mbinu, kwa uelewa wangu, haiishii tu kwenye uwanja wa vita. Mtu binafsi, makampuni ya biashara au nchi inaweza kutumia mbinu hiyo kufanikisha malengo yao mbalimbali, iwe ya kipelelezi, kiuchumi, kisiasa, kibiashara au kijamii.

  Tanzania, kwa historia yake, hasa ya miaka ya '70 mpaka mwanzo mwa '90 (na baadaye, DR Congo) iliposhiriki kikamilifu katika ukombozi wa mwafrika imejiweka katika kundi dogo la nchi ambayo hawa wakubwa wana chuki nazo lakini kwa sababu mbalimbali hawawezi kuweka wazi.

  Nchi nyingine ninayoweza kuifikiria kwa haraka haraka yenye historia kama hiyo ni Haiti (baadhi yenu itabidi muangalie historia ya Haiti, kutoka mapinduzi hadi leo hii raisi wao kutekwa nyara na kutupwa CAR kujua ninachokiongelea).

  Ni historia hiyo inayonifanya niamini suala la meli za Iran ni moja ya mara chache tutakazobaatika kuona waziwazi dalili za kuwepo kwa mchezo mkali unaochezwa zaidi kisirisiri na pande zote mbili. Juzijuzi tu wanajeshi wa kimarekani walikuwa TZ 'wakifundisha' wanajeshi wetu kuhusu mambo ya usalama wa baharini.

  Nyerere aliwahi kusema ukiwakaribisha Wamarekani kuja, hawaondoki tena, naamini hiyo imebaki kuwa ndiyo sera ya TZ na itabaki hivyo kwa muda mrefu. Nadhani kwenye kambi za kidiplomasia, TZ imekuwa inapewa shinikizo kubwa kupitia misaada, propaganda za ugaidi, na huku wakijaribu kukubana kwa kupitia mikataba ya kibiashara (angalia Korea Kusini au Japan wanavyohaha kufanya maamuzi yenye maslahi yao).

  TZ ili kulegesha shinikizo hizo inalazimika kukubali haya mafunzo ya kitoto huku ikijaribu kuwa-'frustrate' hawa wakubwa kwa vitu kama hivi vya bendera. In a sense, TZ is trying to get the monkey off her back.

  Mwalimu Nyerere amewahi kuongelea suala la AFRICOM miaka ya mwisho wa '60, wakati huo Ufaransa ndiyo alikuwa analisukuma. Nitakuja kuweka hapa msome alichowahi kusema kwa sababu ukiyasoma maelezo yake utafikiri yamesemwa leo.

  Nitakuja kuendelea.........
   
 3. Keynez

  Keynez JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 640
  Likes Received: 297
  Trophy Points: 80
  Afrika iko katika harakati kubwa sasa hivi za kujitutumua kutoka katika minyororo ya kibeberu. Wakubwa bado wanatoa upinzani mkali (fanya utafiti kuhusu mgogoro wa Ivory Coast uelewe ni umbali gani wako tayari kwenda kulinda maslahi yao). Watu humu naona wanaongelea sheria za Muungano na kwamba Zanzibar itumie bendera yake.

  Hivi unadhani muonevu akiamua kukusakama anajali sheria ulizojiwekea? Kama wako tayari kupindisha, na hata kuzivunja sheria nyingi za kimataifa walizoshiriki kuziandika kwa jinsi wanavyotaka, unadhani watakaa wasikilize malumbano yenu ya ndani ya kisiasa na kidini kabla hawajaamua kuanza kutuma makombora?

  Pamoja na kusema hivyo, kuna mambo yanafanya uamuzi wa kuiwekea vikwazo au kuishambulia TZ iwe mgumu sana kwa hizi nchi, sasa na hata baadaye. Sababu moja ni ya kiuchumi (kupitia mikataba TZ iliyokubali kwa makusudi kuingia nayo ili kuwabana). Ndiyo maana serikali ya TZ leo inafanya inavyotaka, ndani na nje ya nchi bila kipingamizi chochote.

  Tunawapa wasikie ladha ya dawa zao. Ndiyo, kwenye mambo haya makubwa, kuna misitari hauwezi kuiruka, hasa kwa ghafla, lakini taratibu, ukiendelea kulegeza kamba, chochote kinawezekana. Uamuzi wowote mbaya unaweza kupelekea kupoteza maslahi yao mengi ikiwemo ya kiuchumi, si tu TZ, bali hata sehemu nyingi tu za Afrika, ikiwemo Djibout walipo na kambi.

  Lakini sababu kubwa itakayofanya uamuzi huo kuwa mgumu ni kwamba, tofauti na wengi mnavyofikiri, TZ bado ina ushawishi mkubwa katika Bara zima la Afrika. Ndiyo maana naiita TZ a 'sleeping giant'. Juzi nilikuwa nasoma makala moja iliyokuwa inasema TZ ndiyo nchi muhimu kuliko zote kwa China barani Afrika (Sikushangazwa kwa sababu tayari nilikuwa najua hivyo).

  Kwa maana hiyo, TZ itaendelea kusukuma na kuchokoza, wakati mwingine kwa nia ya kubughudhi tu, wakati mwingine kwa nia ya kusoma mbinu za magharibi (mfano, kwa kutumia watu waliopo kwenye kambi ya upinzani), lakini wakati mwingine kufanya maamuzi mazito na ya maana, ya kiuchumi, kijeshi na kisiasa, ndani na nje ya nchi huku ikijua waonevu hawawezi kufanya kitu kwa sababu kuu mbili nilizozisema. Nakumbuka wakati mgogoro wa Z'bwe ukipamba moto, JK alifanya kikao Dar es Salaam cha wakuu wa SADC, huku wakiwepo kina Mugabe, Kabila n.k.

  Nakumbuka sana hotuba yake hasa alipoongelea jinsi Afrika ilivyoweza kushinda mapambano siku za nyuma 'against all odds'. Mkutano huo uliishia kwa kutaka vikwazo dhidi ya Z'bwe kuondolewa. Siku zote nimekuwa nawaambia watu, matatizo ya kiuchumi ya Z'bwe yatakuja kupungua kirahisi bila vikwazo kuondolewa, lakini hayatakwisha hadi hapo Afrika Kusini itakapokuja kufanya maamuzi sawa na ya Mugabe (nitakuja kuelezea watakavyofanya)...........
   
Loading...