WilsonKaisary
JF-Expert Member
- Apr 4, 2017
- 392
- 946
Kwa tafsiri fupi wasiojua maana designated survivor, huyu Ni mteule wa hatamu ya uraisi ambae huteuliwa na raisi au kamati kuu ya usalama ya nchi au bunge, huyu mtu huteuliwa Palo ambapo viongozi wakuu wa nchi wanapokutana mfano leo Bunge lilipokuwa linavunjwa tumeona viongozi wakuu wamekutana bungeni.
Huyu designated survivor huteuliwa kushika hatamu ya uraisi na kiti Cha uraisi haswa pale kutatokea shambulio la kigaidi na viongozi wote wakadhurika wakuu wa nchi wakafa au kuwa hoi maututi. Yani mfano Leo bungeni Dodoma lingetokea shambulio ambalo linge sababisha vifo au umaututi wa viongozi Hawa wakuu ( Raisi, Makamu, Spika, Naibu spika,Waziri mkuu).
Huyu designated survivor angeapishwa hapo hapo na kuwa raisi wa muda mpaka uchaguzi mkuu ambapo ungefanyika.
Designated Survivor huyu huteuliwa kisiri na hufichwa nje mbali na eneo, lile wanalokutana viongozi Hawa.
Mfano Kama Leo wamekutana Dodoma bungeni, Basi angepelekwa mkoa wa mbali Labda Shinyanga n.k kwa lengo tu asidhurike. Na hulindwa kikamilifu.
Kwa nchi Kama Marekani wanautaratibu huu, haswa pale wanapokutana kwenye Congress ya pamoja.
Je kwa nchi yetu ipo sababu kikatiba ya kuwa na Designated Survivor ataetambulika kikatiba? Na ambae janga Kama hili likitokea aweze kupewa hatamu ya uraisi kwa muda.
Maana tukisema hapana, vipi Kama Leo bunge lingesambalatishwa Leo na tungepoteza viongozi wote. Ni Nani angeshika hatamu ya uraisi? Na kwa misingi ipi au kwa sheria ipi?