Je, Tanzania imewahi kuwa na Rais mwizi?

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,930
3,803
Inawezekana Samia si katika hao na ndio ikawa shida kwa viongozi wa serikali ambao wameota mizizi ndani ya serikali tokea tupate Uhuru na hata marais wastaafu wanaonekana wakijichomeka kung'ang'ania serikali na sio serikali bali Raisi mpya anaeingia madarakani.

Hisia zinaonyesha kuna magenge ambayo mazoea yao yanaonekana kukatika au kukatwa na sasa wanafanya juu chini ili kutafuta mbadala wa Samia ili wizi uendelee kama kawaida.

Ndio nikauliza Tanzania imewahi kuwa na Raisi kibaka?
 
Ndiyo
  1. Alifilisi pesa zote katika mashirika ya hifadhi ya jamii
  2. Alianza kuchungulia katika account za watu na kuchota pesa zao
  3. Wakuu wa wiaya wengine nao walianza kuwa wezi akawa anawaangalia tu hadi wengine wamekamatwa na kufikishwa mahakamani na kufungwa
  4. Alitaifisha michango ya wananchi kwa wananchi wenzao waliopatwa na maafa ya tetemeko la ardhi huko Bukoba alizipeleka fedha hizo kusikojulikana
  5. Mkaguzi na mdhibiti wa fedha za serikali alikuta kuna upotevu wa shs tillion maja na nusu alivyotoa taarifa aliondolewa madarakani kinyume na taratibu
 
Kama hujui unasema sijui. Mwizi ni yule anayekimbilia kumnawilia mwenzake wakati aliiba hadi twiga kapandisha ndege. Fedha za viroba, Richmond, Epa, Kagoda, China, akaweka na waziri asiyesoma kuwa waziri wa elimu, elimu ikafa, hadi baraza la mawaziri likvunjwa kwa maana pm alijiuzuru ili kumlinda yeye. Fedha zote hizi ni ufisadi na wizi wa hadharani. Alikopa mikopo isiyojulikana ni ya nini na ilifanya nini. Nchi ilikuwa inachuzwa kama peremende. Nani asiyejua? Acheni dhambi za kuficha uharifu kwa sababu ya partialities.
 
Maraisi wawili tu ukimtoa huyu aliyepo sasa, walioongoza nchi yetu na nimeona uongozi wao na nikiwa na akili timamu ya kuchanganua mambo, yule wa awamu ya NNE,

Huyo anabeba

Sifa hizo zoote za uwizi na ndiye anayeongoza kwa kuruhusu nchi yetu iibiwe na kuliwa sana, kiasi hata cha wanyama wetu kupelekwa ughaibuni wakiwa hai hivihivi
 
Ndiyo
  1. Alifilisi pesa zote katika mashirika ya hifadhi ya jamii
  2. Alianza kuchungulia katika account za watu na kuchota pesa zao
  3. Wakuu wa wiaya wengine nao walianza kuwa wezi akawa anawaangalia tu hadi wengine wamekamatwa na kufikishwa mahakamani na kufungwa
  4. Alitaifisha michango ya wananchi kwa wananchi wenzao waliopatwa na maafa ya tetemeko la ardhi huko Bukoba alizipeleka fedha hizo kusikojulikana
  5. Mkaguzi na mdhibiti wa fedha za serikali alikuta kuna upotevu wa shs tillion maja na nusu alivyotoa taarifa aliondolewa madarakani kinyume na taratibu
Yule alikuwa ni zaidi ya shetani kabisa
 
Kama hujui unasema sijui. Mwizi ni yule anayekimbilia kumnawilia mwenzake wakati aliiba hadi twiga kapandisha ndege. Fedha za viroba, Richmond, Epa, Kagoda, China, akaweka na waziri asiyesoma kuwa waziri wa elimu, elimu ikafa, hadi baraza la mawaziri likvunjwa kwa maana pm alijiuzuru ili kumlinda yeye. Fedha zote hizi ni ufisadi na wizi wa hadharani. Alikopa mikopo isiyojulikana ni ya nini na ilifanya nini. Nchi ilikuwa inachuzwa kama peremende. Nani asiyejua? Acheni dhambi za kuficha uharifu kwa sababu ya partialities.
Lakini hata huyo aliyemsema jamaa hapo ni mwizi mpaka alitumia MaDC kufanya wizi.
 
Una ushahidi? Miradi aliyokuwa anajenga, inamtetea. Yule wa nne ndiye muasisi wa watu wasiojulikana kama hamjui. Watu walitekwa, wakang'olewa meno na kucha bila ganzi, vifo vya kina Dr. Mvungi na wengineo. Jamaa amekimbilia kujifanya mentor ili aendeleze umfia wake bila kuguswa. Jamani Wtz iweni na tahadhari badala ya kuongea tu kwa sababu za kujiburudisha. Jamaa ni balaa.
 
Sawa yule alikua mwizi...na yule wa March 17 alikua mwezi pia visasi na roho mbaya vilitamalaki...kuthibitisha kua alikua mwizi CAG aliposanua upotevu wa 1.5trilioni akamfanyia zengwe akatolewa..

Kubali kataa alikua mwizi
 
Yule alikuwa ni zaidi ya shetani kabisa

Huo ni uwenda wazimu tu,hakuna cha zaidi.
Unamchukia mtu kwasababu ya matatizoyako mwenyewe.
Vyeti feki na mafisadi wakwepakodi tu ndio mnaweza kutoka kauli kama hizo za kumuita binadamu mwenzenu shetani.

Huyo kasha kufa,hata ukiwa na mahasira kiasi cha kujisaidia haitakusaidia kitu.
Kama kunakitu alikukwaza, Ukisamehe tu akilizako zitarudi kuwa sawa.
vinginevyo utabaki kuwa mnara mbaka siku unafukiwa chini.
 
Inawezekana Samia si katika hao na ndio ikawa shida kwa viongozi wa serikali ambao wameota mizizi ndani ya serikali tokea tupate Uhuru na hata maraisi wastaafu wanaonekana wakijichomeka kung'ang'ania serikali na sio serikali bali Raisi mpya anaeingia madarakani.

Hisia zinaonyesha kuna magenge ambayo mazoea yao yanaonekana kukatika au kukatwa na sasa wanafanya juu chini ili kutafuta mbadala wa Samia ili wizi uendelee kama kawaida.

Ndio nikauliza Tanzania imewahi kuwa na Raisi kibaka ?
Mgagagigikoko ni jizi likubwa
 
Sawa yule alikua mwizi...na yule wa March 17 alikua mwezi pia visasi na roho mbaya vilitamalaki...kuthibitisha kua alikua mwizi CAG aliposanua upotevu wa 1.5trilioni akamfanyia zengwe akatolewa..

Kubali kataa alikua mwizi
Hayo ni majungu, na hayana proof kwamba ni yeye alihusika moja kwa moja. Alimlipiza nani visasi? Alimfanyia nani roho mbaya? Wewe unawezaje kujua zil 1.5t, ziliibiwa na yeye mwenyewe kwa maslahi yake binafsi? Naomba uwe specific. Sisi wanaume wengine hatupendi sana mitaarabu na mipasho isiyokuwa na grounds. Jitahidi kutusaidia msingi wa hoja.
 
Una ushahidi? Miradi aliyokuwa anajenga, inamtetea. Yule wa nne ndiye muasisi wa watu wasiojulikana kama hamjui. Watu walitekwa, wakang'olewa meno na kucha bila ganzi, vifo vya kina Dr. Mvungi na wengineo. Jamaa amekimbilia kujifanya mentor ili aendeleze umfia wake bila kuguswa. Jamani Wtz iweni na tahadhari badala ya kuongea tu kwa sababu za kujiburudisha. Jamaa ni balaa.
Wa nne alifanya miradi mingi kuliko huyo jambazi #5,so. Wote walikwara,ila huyu #5 alikuwa mkora katili,afadhali yule #4 alikwara akawaachia na nyie kidogo mkala mkashiba,huyu wa juzi kati hapa alitamani watu wafe atawale maiti.
 
Naomba acha matusi, andika hiyo miradi bayana. Uzushi na uswahili hatutaki.
 
Hayo ni majungu, na hayana proof kwamba ni yeye alihusika moja kwa moja. Alimlipiza nani visasi? Alimfanyia nani roho mbaya? Wewe unawezaje kujua zil 1.5t, ziliibiwa na yeye mwenyewe kwa maslahi yake binafsi? Naomba uwe specific. Sisi wanaume wengine hatupendi sana mitaarabu na mipasho isiyokuwa na grounds. Jitahidi kutusaidia msingi wa hoja.
Unataka uthibitisho gani tena boss? Wakati hata yule DC wa Hai mahakamani alisema aliyokua akifanya alitumwa na huyo mzee,pia hata CAG alisanua hiyo ishu wakamuondoa sasa unataka nini?

JPM miundo mbinu amejenga kwa kiasi chake lakini na yeye kwemye kundi la wapigaji huwezi kumtoa ndo maana utawala wake hakukua na uwazi hata kidogo sasa kama unaleta mapenzi shauri yako.
 
Kwa hiyo, mtu akisema ndio ushahidi? Huyo Sabaya alipokuwa anaiba alionyesha aliingiza kiasi gani kwenye account ya Magufuli au alimgawia kiasi gani cha pesa?

Ushahidi si maneno ndugu yangu. Mtu anaweza kusema chohocte na ili ushahdi uchukuliwe ni lazima athibitishe. Kasome sheria ya ushahidi.
 
Back
Top Bottom