#COVID19 Je, Tanzania ilifaulu au ilifeli kupambana na COVID-19

FATHER OF REALITY

Senior Member
Nov 3, 2014
122
99
Nilizingatia msimamo tuliokuwa nao COVID-19 ilipoingia nchini kwa mara ya kwanza, nilikuwepo wakati wa wimbi la pili la maambukizi, na nashukuru pia nipo kipindi hiki cha wimbi la tatu la maambukizi na hatua zinazochukuliwa.

Najiuliza je, tulifaulu au kushindwa awamu ya kwanza ya COVID-19, na je kwa sasa tumekuwa serious zaidi au?
 
Maswali haya hutajibiwa zaidi utaambiwa Rais anawajukuu hivyo watalia akifa
 
Ujinga haujali cheo ni kweli yeye ni mama na Rais
Ameweka muhuri wa kuikabidhi nchi hivyo historia utaikumbuka kwa hilo
'mimi ni mama wewe ni kijana ukinizingua tunazinguana'
 
Tatizo mnachanganya sana vitu Covid 19 imekuja kwa awamu, kama bongo ilishinda awamu ya kwanza kuna awamu ya pili na tatu ambayo ni Delta variant inaua kisilencer tu... chukua tahadhari vaa barakoa,.
 
Chini ya uongozi wa Magufuli ilifaulu ila chini ya huyu mama tumepigwa! Sijui kapewa nini na mabeberu
 
Kila zama na kitabu chake..........mwacheni bi mkubwa afanye kazi yake.
Kalamu ishaandika na wino ushakauka.
 
Kipimo cha kufaulu ama kufeli kinaendana na takwimu, kwa kuwa hakuna takwimu zozote hatuwezi kujua, sana sana tuliambiwa tu corona haipo ilikomea mbali, hata hilo wimbi la pili mnalilazimisha halikuwepo kwenye rekodi za serikali, hili tangazo lilizunguka sana kipindi nimonia na changamoto za upumuaji zimeshika hatamu
20210730_223203.jpg
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom